Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mauaji ya Alptekin Zeynelabidin Aksoy, mwenye umri wa miaka 52, ambaye ni raia wa Tanzania mwenye asili ya Uturuki, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana alfajiri katika eneo la Makaburini, Kinondoni.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, tukio hilo lilitokea Julai 18, 2025, majira ya saa 11:30 asubuhi, wakati marehemu alipokuwa akielekea ofisini kwake.
“Alptekin Zeynelabin alishuka kwenye gari lake na kabla ya kuingia ofisini kwake alishambuliwa kwa risasi na kupoteza maisha”, imeeleza taarifa hiyo.
Jeshi la Polisi limeanzisha uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliohusika na limeonya vikali kuwa yeyote atakayebainika kuhusika, kwa namna yoyote ile, atachukuliwa hatua kali za kisheria.