Kwanza ieleweke kuwa mh Rais wetu mpendwa anatekeleza ilani ya CCM aliyoinadi katika uchaguzi wa mwaka 2020 na na chama Cha mapinduzi kupewa Ridhaa ya kuongoza nchi hii mpaka 2025, kwa hiyo ukitaka ujuwe katekeleza Nini nenda kasome ilani yetu ya CCM,
Pili CCM kwa kiasi kikubwa imedhamilia kupitia ilani kuhakikisha kuwa inainua maisha ya mtanzania mmoja mmoja, kwa kulitambua hillo mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani alitamka hadharani kuwa anataka kuona watanzania tunaondokana na Hali ya umasikini na kukuza uchumi wetu
Rais wetu alituahidi sisi wakulima kuwa serikali yetu anayoiongoza inakwenda kuboresha maisha ya wakulima, hapa mh Rais wetu ametekeleza kwa vitendo kwa kutoa Ruzuku ya billioni Mia moja hamsini, Hali hii imesaidia kupunguza Bei ya mbolea kutoka huko kwa laki na nusu Hadi elfu sabini tu, Na kwa Sasa mbolea hizo zimeshawasili na zinapatikana bila shida
Utekelezaji wa ahadi hii ya mh Rais wetu inakwenda kuleta mapinduzi ya kilimo lakini pia inakwenda kuinua maisha ya kundi kubwa la watanzania ambao kwao kilimo ndio pumzi yao na yetu Tulio wengi, kilimo Ni biashara na biashara hii imenufaisha watanzania walio wengi tangia mh Rais awe Raisi maana mkulima mwaka huu ameuza kwa Bei nzuri tangia wakati wa mavuno, maana miaka mingine Bei huwa inakuwa mbaya wakati wa mavuno na kumpa hasara mkulima
Mh Rais wetu mpendwa pia aliahidi kupambana na suala la mfumuko wa Bei ya nishati ya mafuta, suala Hilo amelitekeleza vizuri Sana kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi, hii imesaidia kupunguza makali ya Bei na Hali itaendeleaa kuwa nzuri Zaid mbele ya safari
Rais wetu aliahid pia kuboresha huduma za Afya,Elimu,maji,Miundombinu na hata umeme, vitu hivyo vyote kavifanya kwa kusogeza huduma hizo karibu kabisa na mwananchi, mfano kwa mwaka huu hakuna mwanafunzi aliyefauli ambaye alikosa nafasi ya kujiunga na Kuendelea na masomo, hii Ni kwa Mara ya kwanza kabisa katika historia mh Rais wetu alifanikiwa kumaliza tatizo hili na wanafunzi wote walikwenda kwa wakati mmoja, hata mwakani wanafunzi wote watapata nafas ya kwenda kwa wakati mmoja kwa kuwa tayari serikali inajenga vyumba vya madarasa karibu elfu nane na Zaid nchi nzima
Mh Rais wetu mpendwa pia ametimiza ahadi ya kuona hata watoto wa wanyonge wanapata Elimu, ndio maana unaona kwa Sasa Elimu Ni bure kutoka darasa la kwanza Hadi kidato Cha sita huku mikopo ikipatikana kwa wanaoendelea na Elimu ya chuo kikuu,
Mh Rais wetu pia ameendelea kutoa ajira kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na vya Kati lakini pia mikopo kupitia halmashauri imekuwa ikitolewa,
Mh Rais wetu mpendwa ameendelea kuimarisha demokrasia na utawala Bora ndio maana unaona nchi iko salama na tulivu huku kila mtu akijisikia fahari kuitwa mtanzania
Rais wetu pia ameimarisha diplomasia yetu iliyozaa matunda ya ongezeko la uwekezaji na hata utalii hapa nchi
Mambo alihoahid na kutekeleza mh Rais wetu Ni mengi hata siwez kumaliza hapa