Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu.
Nikiwa natoka zangu kwenye shughuli zangu, nikaamua kupitia maskan fulani ya wabongo huko town. Nika stick kwa masela huku tukipiga story mbili tatu na kukumbushana mambo flan flan ya miaka kadhaa iliyopita (maana ni miaka sasa sifiki town kwa washkaji) ghafla linapita kundi la vijana wanne wakiwa na daftari la michango, na picha ya homeboy wetu flan ambae mimi siimfahamu.
Kwa vile mimi sio mgeni na mambo haya nikawa nimeshaelewa nini kinachoendelea kupitia daftari lile, ila kwa ku confirm ikabidi niulize kuhusu mchango ule kwamba ni wa kifo au ugonjwa. Jamaa wakanijibu kwamba ni kifo cha homeboy wetu alieuwawa kwa kupigwa risasi siku kadhaa zilizopita.
Basi mimi sikutaka maelezo marefu kwa sababu naelewa mazingira ya vifo vyetu, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa nilichojaaliwa kuchangia nikawapa jamaa (bila kujali kama kifo kile ni cha kweli au vijana wametengeneza mazingira ya kupiga pesa) maana dunia ishaharibika. Mnaweza kujikuta mnachangishwa mchango wa mtu aliekufa na kuzikwa tayari miaka miwili au mmoja uliyopita, au pengine picha ya mtu ambe alisharudi bongo kitambo ikatumiwa tu na vijana wasela mavi kujipatia hela za kulewea.
Sikitiko langu kubwa ni kwa hawa ndugu zangu au zetu ambao wameshindwa kuelewa uhalisia wa maisha ya nchi hii. Hii nchi ni kaburi na jahanam kwa watu waliozoea maisha ya kipanya road panya road kule bongo, na ni peponi au mahali pazuri kupata mafanikio kwa watu waliozoea maisha ya kutafuta kwa kupitia mikono yao na akili zao.
Nchii hii ina mchanganyiko wa watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia hii, na kila raia wanaishi kulingana na mazingira ya maisha waliyozoea kutoka nchini kwao. Kwa mfano Warundi wengi kazi zao hapa ni salon na gereji. Wakenya ni walimu, manesi, madaktari na wa wafanya biashara wa vinyago, maua nk. Waganda nao wamejitupa kwenye uganga wa kienyeji na wanapiga hela kweli kweli (sababu nchi hii watu wengi wanahitaji mafanikio ya haraka haraka kupitia njia za giza) Wakongo wao ni kazi za ulinzi, salon, wachungaji makanisani nk. Na nchi zote nilizotaja hapo juu huwa zina utamaduni au utaratibu wa kuletana huku kwa lengo la kuendelea na hayo wanayofanya wenzao na wanatusua.
Sasa ndugu zetu wabongo wengi wakija huku wanakuwa hawajui wanakuja kufanya nini. Wengi hawana elimu au ujuzi wa kuandika na kusoma hata kiswahili chetu wenyewe (achilia mbali English, Zulu na Afrikans) ambazo ni lugha muhimu zinazoongelewa hapa. Wabongo wengi hawana ujuzi wa kazi, biashara wala elimu, kwahiyo wakifika nchi hii lazima wafeli na kujiingiza katika mambo ambayo mwisho wa siku uhatarisha maisha yao.
Mtu unaweza kujiuliza inakuaje nchi yenye raia wa mataifa zaidi ya 50, ni wabongo tu ndio wawe wanauwawa, wanafungwa, wanateswa na kupigwa na polisi au makundi mengine ya kihalifu kila siku. Yan haipiti mwezi bila kusikia kuna mbongo kajeruhiwa, au kuuwawa aidha na polisi au mtu au kundi fulani la wahalifu. Ni muda sasa wa wabongo kuwa tunaambiana ukweli ili kupunguza haya matukio kuendelea upande wetu.
Wabongo mababu zetu kupitia serikali yetu (chini ya Nyerere) walipambana kuleta uhuru katika nchi hizi. Na zamani wakati tunafika fika katika nchi hii tulipewa heshima kubwa na raia wa nchi hii wakiwemo viongozi, lakini kwa kutokujitambua kwetu tukashindwa kuitumia fursa hiyo kujiendeleza na matokeo yake wenzetu kutoka Afrika Magharibi haswa Nigeria wakaja kuitumia fursa hiyo na kupata mafanikio makubwa. Maeneo mengi ya maduka ya nje yalikuwa yanamilikiwa na wabongo, ila kwa kuendekeza viuno na kukosa elimu na maarifa sehemu hizo tukaziuza kwa wingi kwa Wanigeria. Matokeo yake sasa wabongo wengi wanahangaika kwa kukosa kazi au sehemu za kufanyia biashara na mwisho wa siku wanafanya yale wasiotakiwa kufanya ili mkono uende kinywani. Namaanisha mbongo anaamua kuuza chochote hata kile ambacho si halali kuuzwa mtaani na kupelekea migogoro kati yao na serikali (polisi).
Wasomali na Waethiopia wanakuja nchi hii wakiwa hawajui lolote, hata kumsalimia mtu asubuhi "Good morning" wanashindwa. Lakini kwa vile wanakuwa wanajua malengo na sababu ya kilichowaleta hapa basi baada ya mwaka au miaka kadhaa wanatusua na kuwa na maisha mazuri kuliko raia wa nchi nyingi za Afrika.
Kwahiyo ndugu zangu wabongo na watanzania kwa ujumla, ni muda wa kujitafakari zaidi pindi tunapokuwa hapa au kabla ya kuja hapa kwamba tumekuja kufanya nini na tutarudi nyumbani na nini. Swala la viuno, tungi na mihadarati mingine haina tija kwa dunia ya leo. Tutaisha nchi hii.
Karibu tuchangie ndugu zangu.