Kuna Jamaa yangu anafanya Ubalozi wetu huko, aliniambia hakuna Ubalozi unaopata Changamoto kama Ubalozi Wetu Afrika Kusini.
Watu wengi sana wanauwawa na idadi kubwa sana wanafungwa jela. Wanazamia bila passport na kujiingiza kwenye maswala ya Unyang'anyi na Madawa ya kulevya. Wengi mno wanapigwa risasi.
Jamaa anasema acha wafe. Kwa sababu Kuna 'mentality' ilijengeka kuwa Jozi maisha mteremko. Kutoboa ni fasta. Ikawavutia vijana kujiingiza kiholela. Lakini kwa matukio yanayoendelea, watu watakoma kujiingiza na kufanya mambo haramu.