Mtoa mada na wachangiaji wengi mnawalaumu vijana kujilipua kwanda SA na kufanya shughuli za kihalifu, lakini mmeshindwa kusema kiini cha tatizo, na kwa nini asilimia kubwa waliopo huko ni vijana wa kitanzania wanaotokea maeneo ya uswahilini Dar?
Tatizo limeanzia hapa nyumbani , maisha yamekuwa magumu kupitiliza, vijana wengi wamekata tamaa, wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza mbele ya macho yao...
Solution
________
Serikali itengeneze mazingira rafiki ya kujiajiri na kwa wawekezaji ili michongo iongezeke hapa nyumbani.
(boda boda sio ajira)
Mkuu acha kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi. Kama umeingia hapa kwa lengo la kuja kuleta siasa katika uzi basi ni bora uende zako katika jukwaa la siasa ukawashauri wanaofuatilia siasa kule.
Hili ndio tatizo kubwa la baadhi ya watanzania wenzetu, unakuta wanaingiza siasa au mambo ya kipuuzi kila sehemu.
Unailaumu serikali kwa ujinga, uvivu na uzembe wa watanzania wenyewe. Unataka serikali ikusaidiaje wakati wewe mvivu haupendi kufanya kazi.
South Afrika hapa au hata huko Ulaya kumejaa raia kutoka katika nchi masikini na zenye mifumo mibovu kuliko hata Tanzania, lkn kwa vile raia wa nchi hizo ni wachapakazi na wanaojielewa unakuta wanaishi maisha mazuri au ya wastan zaidi ya yale wanayoishi vijana wa kitanzania.
Congo, Burundi, Somalia na kwengineko ni nchi za kivita na zenye mifumo mibovu ya kimaisha. Lkn ukiangalia maisha yao wanapokuwa nje ni tofauti na maisha wanayoishi watanzania wanaotoka katika nchi ya amani na yenye mifumo nafuu kidogo ya maisha ukilinganisha na nchi hizo.
Tatizo lenu kubwa watanzania ni uvivu, hilo swala la kutokuwa na kazi kutokana serikalini mnalitumia kama kichaka cha kuficha udhaifu wenu.
Haya tuseme serikali ya Tanzania haitengenezi mazingira mazuri ya kazi, je huku ambapo kuna kazi mbona wanashindwa kuzifanya matokeo yake zinafanywa na raia kutoka nchi zingine masikini?
Kila inapotokea fursa za kazi watanzania huwaoni, utakao waona ni raia wa kutoka nchi nyingine tu za Afrika?
Je unataka serikali ya Tanzania ije huku iwaombee kazi ambazo hawataki kuzifanya?
Hapo hapo Tanzania kuna kazi kibao ambazo zinafanywa na wageni kutoka Burundi, Uganda, Rwanda, Kenya nk baada ya wenyeji au wazawa kushindwa kuzifanya.
Juzi uhamiaji walitangaza kuanza kutoa vibali vya uraia wa muda kwa wageni wote watakaotaka kuja kufanya kazi za uvuvi na ulimaji Tanzania baada ya kugundua kuwa wazawa wenyewe ni wavivu hawataki kufanya kazi hizo.
Yani ni afadhali mtu akimbilie Dar akawe omba omba katika mataa ya barabarani (trafiki light) kuliko kubaki kijijini alime na kuuza mazao yake sokoni.