Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #141
Hili ni janga la taifa. Watanzania wengi ni wavivu sana ndomaana fursa zilizopo nchini na nje ya nchi hatuzichangamkii.Bongo fursa nyingi sana ukilinganisha na nchi zote za maziwa makuu yanayotuzunguka, tatizo linaanzia kwetu vijana kwa kuamini kua utajiri au mafanikio upatikana kwenye mambo yasiyo na tija kama vile kubeti Uchawa na wengine wamepumbazwa akili na mitume feki, kundi lingine la vijana ambao pia ni nguvu kazi imehamia kwa MISHANGAZI wakiamini kulelewa na MISHANGAZI uleta utajiri
Kuna clip fulan niliifuatilia miezi miwili iliyopita huko Dodoma nikaona mkuu wa polisi fulan amewakusanya wazazi wa wilaya fulan anawaeleza namna ya kuwadhibiti watoto wao ili wasiendelee au kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu.
Kamanda huyo kuna sehemu amesema kwamba amekuwa akiwaona vijana kutoka Burundi na Rwanda wakifanya kazi kwenye mashamba na viwanda kibao vilivyopo Dodoma, huku wazawa wakiishia kushinda vijiweni wakipiga zogo na kuomba watu mia tano mia tano za kula.
Anakwambia hata wale wazawa waliokuwa wameajiriwa wengi wao wakishapata mishahara hutoweka kazini na kuonekana baada ya week mbili au tatu baada ya mshahara wao kuisha 🤣🤣🤣