Mtanzania mwingine apigwa risasi Afrika Kusini

Mtanzania mwingine apigwa risasi Afrika Kusini

Sahihi kabisa , ukiona hadi unaingia kwenye anga za hao washika bunguki , "ama 7 phezulu" jua na wewe sio msafi .
Wabongo tujifunze njia ndefu za kutafuta maisha , sio illigal shorcuts
Kweli mkuu, ni vizuri tubadilike maana tutaisha bure.
 
Mnaenda south nendeni, si Wala kufikilia na ndugu zetu wamendoka na makaburu toka mwaka 1993, wameondoka huku solomoni malangu wameolewa na kuzaa, wapo waliotelekezwa kuachwa kwenye mataa, na waliondoka nao, na mwezi wa sita ndugu zetu wanakuja Ila hatuwazi kwenda nao, tumezoea michunga kule unapata wapi.[emoji16]
Hahahaha umenichekesha sana mkuu. Sema ndo hivyo waafrika sote ni ndugu na maisha ni popote.

Wewe umechagua huko ukaona panakufaa, na wengine tumechagua huku tukaona panatufaa haswa kwa utafutaji. Ila huwa narudi bongo kila baada ya mwaka mmoja au sometimes miwili.

Sijazamia moja kwa moja kama wabongo wengine.
 
Wabongo Wana sifa mbaya Sana Sauzi, wezi, vibaka, wauza unga, nk. Awaaminiki zaidi ya kukata viuno na kufungua chupa za bia hawana kingine.
Wasomali waethiopia wakenya Nigeria dunia nzima wakienda ni kutafuta na kupeleka nchi mwao.
Yani tunatia aibu kaka. Tunashindwa hata na warundi wanaotoka nchi za vita.
 
Uyo jamaa ni msela angu tumekuwa naye mitaa ya sombetini tumeuza Sana bangi à.k.a mpepe au shada maeneo ya singida na mwanza wakati uo tunashafirisha kupitiya magari ya magazeti na mizigo.
Badae akapotea zake sauzi
R.I.P my G😭😭😭
Dah pole sana mwana kwa kupoteza mshikaji wako wa karibu.
 
Huyu dogo sijui nini kimemkuta maana Brother ake mkongwe hapo kitambo na nina uhakika ana ramani na address zote za J'berg.
Huenda ni kudhulumiana au madem mkuu. It's not easy someone to kill him without any reason.
 
Huenda ni kudhulumiana au madem mkuu. It's not easy someone to kill him without any reason.

inawezekana pia maana naona kuna wakati mpaka "hit man's" wanatumwa bongo kuja kumaliza watu waliodhulumu huko.

Shida vijana wengi wakibongo uelewa mdogo sana na ukosefu wa good primary education, unatoka kwenu bongo nakwenda kuwa mwizi wa mifukoni SA, na michongo mingine ya kifalafala ambayo hata hapa bongo inawezekana tu.

Vijana wengi wanataka kuishi SA kama sifa tu lakini hakuna wanachogain.
 
Hahahaha umenichekesha sana mkuu. Sema ndo hivyo waafrika sote ni ndugu na maisha ni popote.

Wewe umechagua huko ukaona panakufaa, na wengine tumechagua huku tukaona panatufaa haswa kwa utafutaji. Ila huwa narudi bongo kila baada ya mwaka mmoja au sometimes miwili.

Sijazamia moja kwa moja kama wabongo wengine.
Kuonewa onewa, kuishi kwa mashaka, hivi ukienda kufanya nao kazi uogopi kweli.
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Nikiwa natoka zangu kwenye shughuli zangu, nikaamua kupitia maskan fulani ya wabongo huko town. Nika stick kwa masela huku tukipiga story mbili tatu na kukumbushana mambo flan flan ya miaka kadhaa iliyopita (maana ni miaka sasa sifiki town kwa washkaji) ghafla linapita kundi la vijana wanne wakiwa na daftari la michango, na picha ya homeboy wetu flan ambae mimi siimfahamu.

Kwa vile mimi sio mgeni na mambo haya nikawa nimeshaelewa nini kinachoendelea kupitia daftari lile, ila kwa ku confirm ikabidi niulize kuhusu mchango ule kwamba ni wa kifo au ugonjwa. Jamaa wakanijibu kwamba ni kifo cha homeboy wetu alieuwawa kwa kupigwa risasi siku kadhaa zilizopita.

Basi mimi sikutaka maelezo marefu kwa sababu naelewa mazingira ya vifo vyetu, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa nilichojaaliwa kuchangia nikawapa jamaa (bila kujali kama kifo kile ni cha kweli au vijana wametengeneza mazingira ya kupiga pesa) maana dunia ishaharibika. Mnaweza kujikuta mnachangishwa mchango wa mtu aliekufa na kuzikwa tayari miaka miwili au mmoja uliyopita, au pengine picha ya mtu ambe alisharudi bongo kitambo ikatumiwa tu na vijana wasela mavi kujipatia hela za kulewea.

Sikitiko langu kubwa ni kwa hawa ndugu zangu au zetu ambao wameshindwa kuelewa uhalisia wa maisha ya nchi hii. Hii nchi ni kaburi na jahanam kwa watu waliozoea maisha ya kipanya road panya road kule bongo, na ni peponi au mahali pazuri kupata mafanikio kwa watu waliozoea maisha ya kutafuta kwa kupitia mikono yao na akili zao.

Nchii hii ina mchanganyiko wa watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia hii, na kila raia wanaishi kulingana na mazingira ya maisha waliyozoea kutoka nchini kwao. Kwa mfano Warundi wengi kazi zao hapa ni salon na gereji. Wakenya ni walimu, manesi, madaktari na wa wafanya biashara wa vinyago, maua nk. Waganda nao wamejitupa kwenye uganga wa kienyeji na wanapiga hela kweli kweli (sababu nchi hii watu wengi wanahitaji mafanikio ya haraka haraka kupitia njia za giza) Wakongo wao ni kazi za ulinzi, salon, wachungaji makanisani nk. Na nchi zote nilizotaja hapo juu huwa zina utamaduni au utaratibu wa kuletana huku kwa lengo la kuendelea na hayo wanayofanya wenzao na wanatusua.

Sasa ndugu zetu wabongo wengi wakija huku wanakuwa hawajui wanakuja kufanya nini. Wengi hawana elimu au ujuzi wa kuandika na kusoma hata kiswahili chetu wenyewe (achilia mbali English, Zulu na Afrikans) ambazo ni lugha muhimu zinazoongelewa hapa. Wabongo wengi hawana ujuzi wa kazi, biashara wala elimu, kwahiyo wakifika nchi hii lazima wafeli na kujiingiza katika mambo ambayo mwisho wa siku uhatarisha maisha yao.

Mtu unaweza kujiuliza inakuaje nchi yenye raia wa mataifa zaidi ya 50, ni wabongo tu ndio wawe wanauwawa, wanafungwa, wanateswa na kupigwa na polisi au makundi mengine ya kihalifu kila siku. Yan haipiti mwezi bila kusikia kuna mbongo kajeruhiwa, au kuuwawa aidha na polisi au mtu au kundi fulani la wahalifu. Ni muda sasa wa wabongo kuwa tunaambiana ukweli ili kupunguza haya matukio kuendelea upande wetu.

Wabongo mababu zetu kupitia serikali yetu (chini ya Nyerere) walipambana kuleta uhuru katika nchi hizi. Na zamani wakati tunafika fika katika nchi hii tulipewa heshima kubwa na raia wa nchi hii wakiwemo viongozi, lakini kwa kutokujitambua kwetu tukashindwa kuitumia fursa hiyo kujiendeleza na matokeo yake wenzetu kutoka Afrika Magharibi haswa Nigeria wakaja kuitumia fursa hiyo na kupata mafanikio makubwa. Maeneo mengi ya maduka ya nje yalikuwa yanamilikiwa na wabongo, ila kwa kuendekeza viuno na kukosa elimu na maarifa sehemu hizo tukaziuza kwa wingi kwa Wanigeria. Matokeo yake sasa wabongo wengi wanahangaika kwa kukosa kazi au sehemu za kufanyia biashara na mwisho wa siku wanafanya yale wasiotakiwa kufanya ili mkono uende kinywani. Namaanisha mbongo anaamua kuuza chochote hata kile ambacho si halali kuuzwa mtaani na kupelekea migogoro kati yao na serikali (polisi).

Wasomali na Waethiopia wanakuja nchi hii wakiwa hawajui lolote, hata kumsalimia mtu asubuhi "Good morning" wanashindwa. Lakini kwa vile wanakuwa wanajua malengo na sababu ya kilichowaleta hapa basi baada ya mwaka au miaka kadhaa wanatusua na kuwa na maisha mazuri kuliko raia wa nchi nyingi za Afrika.

Kwahiyo ndugu zangu wabongo na watanzania kwa ujumla, ni muda wa kujitafakari zaidi pindi tunapokuwa hapa au kabla ya kuja hapa kwamba tumekuja kufanya nini na tutarudi nyumbani na nini. Swala la viuno, tungi na mihadarati mingine haina tija kwa dunia ya leo. Tutaisha nchi hii.

Karibu tuchangie ndugu zangu.
Tamaduni zetu za kiswalihi na mazoea tunapeleka kwa jamii ambayo mazoea ni marufuku..

Lazima upigwe shaba.
 
inawezekana pia maana naona kuna wakati mpaka "hit man's" wanatumwa bongo kuja kumaliza watu waliodhulumu huko.

Shida vijana wengi wakibongo uelewa mdogo sana na ukosefu wa good primary education, unatoka kwenu bongo nakwenda kuwa mwizi wa mifukoni SA, na michongo mingine ya kifalafala ambayo hata hapa bongo inawezekana tu.

Vijana wengi wanataka kuishi SA kama sifa tu lakini hakuna wanachogain.
Wabongo wengi wanaokuja huku ni wale vijana wadogo wadogo ambao wengi wao ni vibaka wa mitaani kama vile panya road nk. Wanajua wakifika huku wizi wao utawasaidia kutoka kimaisha.

Kwahiyo wanakuja huku kwa lengo la kuja kuiba au kuuza madawa ili apate fedha, sio kufanya kazi au biashara kama wenzetu. Hakuna Mkenya anaekuja huku bila kujua anachokuja kufanya.
 
Kuonewa onewa, kuishi kwa mashaka, hivi ukienda kufanya nao kazi uogopi kweli.
Kama ilivyo kwa watanzania au hata kwenye familia mnaweza kuzaliwa baba mmoja mama tofauti. So ukakuta watoto wale wa mama tofauti baadhi wanapatana na baadhi wanachukiana.

Sio kila mtanzania, mkenya, mganda, msauzi nk ana roho mbaya au nzuri. Kote utakuta kuna watu wabaya na watu wazuri. So ninaofanya nao mimi kazi hawana tatizo kwa sababu wana kazi tayari ya kuwaingizia kipato cha uhakika. So anichukie mimi kwa lipi!
 
Tatizo la wabongo wengi wo huko bondeni ishu zao ni kuuza Powder, Bangi au ukabaji. Mukishauliwa munakuja kulalamika humu. Tunakosa nguvu hata za kuwalalamikia, Acheni kazi za kishenzi.
 
Tatizo la wabongo wengi wo huko bondeni ishu zao ni kuuza Powder, Bangi au ukabaji. Mukishauliwa munakuja kulalamika humu. Tunakosa nguvu hata za kuwalalamikia, Acheni kazi za kishenzi.
Mkuu umenisoma vizuri katika andiko langu na kujiridhisha kuwa mimi ni mmoja wa hawa uliosema katika comment yako?

Mimi sijalalamika bali nimeshauri ndugu zetu watanzania wale waliopo hapa Sauzi na wale ambao bado hawajaja, lakini wana ndoto za kuja.

Unaposema kabila fulan wako hivi, haimaanishi kuwa wote wako hivyo, bali kuna baadhi wanakuwa tofauti na wenzao.
 
Hahaha ulichoongea ni kweli. Hii nchi unafursa nyingi kama utajua kuzitumia vyema fursa zilizopo utatoboa tu. Mbona wasomali wanatoboa kwa biashara mbali mbali.

Sasa mbongo hataki kazi ya mikono, na ukimpa duka auze anakutia ndimu ya macho kwa kukimbia na msingi wa duka.
Hili ni tatizo kubwa sana mkuu.
 
Watoto wa magomeni, temeke na ilala ndo wapo SA kwa wingi. wengi wao shule hakuna. hata 4m4 mtu hakumaliza. Akina dula hao
Sasa hivi kuna wimbi la watoto wa mbagala aisee. Hawa ndo kabisa hawajui hata kuvuka barabara, ila ndo wanaojifanya wanajua kila kitu kumbe zero kabisa.
 
Back
Top Bottom