Mtanzania mwingine apigwa risasi Afrika Kusini

Mtanzania mwingine apigwa risasi Afrika Kusini

Nimezika washkaji wanne tena wawili madogo kwangu wamepigwa shaba yaani kweupe hakuna kesi wala nn tumezika ...Kingine hebu nendeni kule Facebook...
Tusikimbilie kuwalalamikia wenzetu kabla kwanza ya kujilalamikia sisi wenyewe. Maisha tunayoishi wabongo nchi za wenzetu laiti wangeishi raia wa nchi zingine hapa nchini kwetu tungelalamika sana kuwa raia hao wanakuja kutuharibia watoto wetu.

Juzikati kuna Mnigeria sijui na Mcameroon walikamatwa Tanzania kwa makosa ya kutengeneza pasi feki za kusafiria, mitambo, na karatasi za kutengeneza hela bandia.

Nikaona wabongo karibu wote wanalalamika kwamba serikali inaruhusu wanigeria kuingia nchini kwetu kiholela na matokeo yake ndo hayo ya kutengeneza pesa na pasi bandia.

Watu wakaomba serikali ipige marufuku wanigeria na raia wa nchi za magharibi kuingia nchini kwetu, lkn wakati huo huo hawalaumu au kulalamika juu ya kile wanachofanya raia wetu katika nchi za wenzetu.

Ni kwanini tuwafanyie wenzetu vile ambavyo hatupendi kufanyiwa kwetu?

Kuna raia wengi hapa kutoka Kenya, Ugand nk, mbona hawauwawi uwawi ovyo kama wabongo? Nafikiri jibu unalo mkuu.
 
Jamaa anaonekana ni mtu poa tu, shida ni nini wakuu...japo wanaume tunapitia maswahibu mengi sana.
Jamaa sijui imekuwaje?....

Tatizo south ukizinguana na mtu anakuwinda hakubali yaishe.
Yah anaweza kuwa mtu poa machoni, lkn kazi au biashara anayofanya ikawa tofauti na muonekano wake.

Kingine wivu wa mapenzi nao huchangia vifo hivi. Mtu anajua kama huyu ni demu au mke wa mzawa anataka apitie ili ionekane yeye jogoo. Sasa mwisho wa siku mwenye mke anakufumania au kupata taarifa na kukuuwa mchana kweupe.
 
Sio mafala bali hawapendi mafala. Wabongo nyookonyoko nyingi. Panya road wanakwenda kuishi south
Yah panya road anataka akifika huku aendeleze mtindo wake wa kupiga ndole kwenye mkusanyiko wa watu wengi, matokeo yake anakwenda kumpiga ndole mtu sio na kuishia kaburini.
 
Nimetoka Maitland -Cape Town mwaka 2012,niliporudi Bongo nikawa nawashauri madogo hasa wanaopenda Ubaharia wa Kisela wasiende Kaburu kwa kuwa hakuna maisha,wajaribu kuingia Namibia tena wakiwa na Leseni au ufundi wa nguo,

Kuna kitu kikubwa inabidi kifanyike katika nchi hii,vijana wengi wanapenda Utajiri lakini hawajui mbinu au maarifa ya kufikia Ndoto zao matokeo yake yanakuwa machungu kwao,

Ni rahisi kutajilika ukiwa Tanzania kuliko Afrika Ya Kusini,tufundishe mbinu na maarifa ya kutoboa kwa wadogo zetu ili kuwasidia kuondokana na stori za vijiweni.
 
Uliloongea ni kweli na wengi shughuli zao ndio hizi nilizoeleza hapa.

Bila shaka wewe ni mwenyeji unajua ninachoongea mkuu.
Kwa South Africa Cape Town naijua vilivyo maana nimeishi huko miaka 8. Japo niliishi kihalali sio kwa mazabe.

Asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania wanauza madawa rejareja (vipinchi) na hawa wengi wao huishia kuwa watumiaji wakuu wa madawa hayo kupelekea kuwa vibaka.

Wengi wanauza vitu vidogo vidogo (pipi, sigara nk) mabarabarani (ndau) wengi wao hivyo vitu vidogo vidogo huwa ni geresha ya kuuza vitu vya wizi (simu zaidi) na bangi.

Kazi nyingine kubwa ni vinyozi (bora hawa wanaishi kihalali japo wengi wao wakipata channel wanaingia kwenye kuuza madawa).

Kipindi nilichokuwepo huko kulikuwa na jopo kubwa la vijana matapeli kwa kupitia uganga feki na mchomoko (kurubuni watu kuwa wanaweza kuzalisha pesa zaidi kwa chemicals halafu wanakimbia na pesa za watu). Wengi sana waliuliwa na wale waliowaibia.

Kwa kifupi asilimia kubwa ya wabongo waliopo South Africa wana ndoto moja tu ya kuwa ma don wa kuuza unga na wengi wanaamini ili hili kutimia basi apate safari ya upunda kwenda brazil au pakistan kubeba unga. Wengi huishia kudhulumiwa na waliowabebesha au kukamatwa kuishia jela.

South Africa ina fursa nyingi mno ukiwa unaenda kimstari bila kona kona. Na unaweza hata usihisi kuwa upo ugenini.
 
Nimetoka Maitland -Cape Town mwaka 2012,niliporudi Bongo nikawa nawashauri madogo hasa wanaopenda Ubaharia wa Kisela wasiende Kaburu kwa kuwa hakuna maisha,wajaribu kuingia Namibia tena wakiwa na Leseni au ufundi wa nguo,

Kuna kitu kikubwa inabidi kifanyike katika nchi hii,vijana wengi wanapenda Utajiri lakini hawajui mbinu au maarifa ya kufikia Ndoto zao matokeo yake yanakuwa machungu kwao,

Ni rahisi kutajilika ukiwa Tanzania kuliko Afrika Ya Kusini,tufundishe mbinu na maarifa ya kutoboa kwa wadogo zetu ili kuwasidia kuondokana na stori za vijiweni.
Mkuu kwa aina hii ya maisha wanayoishi watanzania wenzetu hata waende Marekani hawawezi kutoboa. Kama ulivyosema kwamba wabongo wengi wanapenda maisha ya short cut, ila hawawezi kujishughulisha na kazi za mikono yao. Wengi wamefeli kwa sababu ya kutokujua au kujishughulisha na kazi.

Ndomaana mimi leo sishangai kusikia kuwa wizara ya mambo ya ndani kupitia uhamiaji wameamua kutoa vibali maalum na uraia wa muda kwa wageni watakaotaka kuja kufanyakazi za kilimo na uvuvi kwani wazawa wengi ni wavivu na kazi zinaelekea kuwashinda.

Pia mwezi uliyopita nilimsikia kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma akiwaasa watanzania waache uvivu na kufanyakazi, hii ni baada ya kamanda huyo kugundua kwamba maeneo mengi ya viwandani na mashambani wameajiri vijana kutoka Burundi, Rwanda na Congo baada ya wazawa wenyewe kushindwa kufanya kazi hizo.
 
Kwa South Africa Cape Town naijua vilivyo maana nimeishi huko miaka 8. Japo niliishi kihalali sio kwa mazabe.

Asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania wanauza madawa (vipinchi) na hawa wengi wao huishia kuwa watumiaji wakuu kupelekea kuwa vibaka.

Wengi wanauza vitu vidogo vidogo mabarabarani (ndau) wengi wao hivyo vitu vidogo vidogo huwa ni geresha ya kuuza vitu vya wizi (simu zaidi) na bangi.

Kazi nyingine kubwa ni vinyozi (bora hawa wanaishi kihalali japo wengi wao wakipata channel wanaingia kwenye kuuza madawa).

Kipindi nilichokuwepo huko kulikuwa na jopo kubwa la vijana matapeli kwa kupitia uganga feki na mchomoko (kurubuni watu kuwa wanaweza kuzalisha pesa zaidi kwa chemicals halafu wanakimbia na pesa za watu). Wengi sana waliuliwa na wale waliowaibia.

Kwa kifupi asilimia kubwa ya wabongo waliopo South Africa wana ndoto moja tu ya kuwa madon wa kuuza unga na wengi wanaamini ili hili kutimia basi apate safari ya upunda kwenda brazil au pakistan kubeba unga. Wengi huishia kudhulumiwa na waliowabebesha au kukamatwa kuishia jela.

South Africa ina fursa nyingi mno ukiwa unaenda kimstari. Na unaweza hata usihisi kuwa upo ugenini.
Asante mkuu kwa maelezo mazuri yaliojitosheleza. Kifupi ulichoandika ndio uhalisia wa kile kinachoendelea hapa.
Watanzania wengi hawakuja huku kwa lengo la kuja kufanya kazi ili watoke, bali wamekuja kwa lengo la kufanya biashara za kijinga jinga ambazo wengi wanaishia kufa, kuumia au kufungwa jela.
 
Watanzania wanaoishi Msumbiji hasa maeneo ya Nampula ni tofauti na wabongo wa Kaburu,hata Malawi na Zambia watu wanajiongeza sana,

Tatizo wengi wanaoingia miaka ya hivi karibuni ni madogo ambao akili na maarifa ya hii dunia bado,pili wanaowapokea na wao akili zimeshakuwa mbovu kutokana mfumo wa maisha wengi wauza madawa au beach boys kwa mitaa ya kule Durban,

Vijana wa sasa wa Tanzania tumelala sana,mitandao imetufanya tumekuwa wapumbavu badala ya kuitumia kuongeza maarifa ya kupata taarifa za kutusaidia maishani,

Kwa sasa maisha bora yanapatikana Africa na hasa Tanzania kwa sababu dunia ya viwanda imehamia China na malighafi zinapatikana kwetu,

Leo nilikuwa na Wanyarwanda wamekuja kuwekeza katika madini ya Kopa,hawa wajamaa wanatushangaa kweli nchi ilivyokuwa na rasilimali juu juu tu lakini watu wanapambana na boda boda au kuja huko Kaburu wakiamini watatoboa,

Tufungue vichwa na tuangalie maisha bora yanapatikanaje,na njia ipi itumike kuboresha maisha yetu kwa sasa na watoto wetu
 
Back
Top Bottom