Mtanzania Tarimo Nemes Raymond, afariki akiwapigania Wagner wa Urusi, kule Ukraine

Mtanzania Tarimo Nemes Raymond, afariki akiwapigania Wagner wa Urusi, kule Ukraine

Ngozi nyeusi kwa kujipendekeza hatari kweli ...

Hiyo ni vita ya warusi (wabaguzi wa rangi) acha wauane ili wapungue tujipatie mademu wa kirusi 😋😋😋

Acha wauane wakiisha sisi tuzamie na kula mbususu kimasikhara 🤪🤪🤪
 
Kama wiki imepita nilikuwa na classmate wake maeneo ya Mbezi kwa Msuguri ikaja taarifa kuwa mwamba kafia vitani hakuna aliyeamini labda kwa taarifa hii ndio tumethibitisha.
 
Ndio kusema wafungwa wanapelekwa kwenye vita huko urusi?
 
Pole sana tena kutolewa gerezani kwa kulazimishwa kwenda vitani, alikuwa hana namna ila awe Mamluki, RIP Tarimo.
1673963041676.png
 
kutolewa gerezani kwa kulazimishwa kwenda vitani, alikuwa hana namna ila awe Mamluki

Washington DC, Marekani
30 December 2022

Msemaji wa Baraza la Taifa la Usalama la taifa la Marekani , Bw. John Kirby anasema kundi la mamluki la Russia, Wagner Group, kama jeshi la Russia, linakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi na hivyo kuamua kuandikishwa wafungwa.

Kirby anasema mkuu wa Wagner Group, Yevgeny Prigozhin binafsi amekwenda kwenye magereza ya Russia kuandikishwa wafungwa kupambana katika mstari wa mbele.

John Kirby, Msemaji wa Baraza la Taifa la Usalama: “Inaonekana kama vile Bwana Prigozhin yuko tayari kuitupa miili ya warussia katika mashine ya kusaga nyama huko Bakhmut.

Kwa kweli, kiasi cha wapiganji elfu moja wa Wagner wameuawa katika mapigano katika wiki za karibuni, na tunaamini kwamba asilimia 90 kati ya hao wapiganaji elfu moja kwa kweli walikuwa wafungwa.”
FILE PHOTO: Kituo binafsi ya kundi la kijeshi binafsi chafunguliwa huko Wagner St Petersburg, Russia.

FILE PHOTO: Kituo binafsi ya kundi la kijeshi binafsi chafunguliwa huko Wagner St Petersburg, Russia.

Olga Romanova ni muanzilishi wa kundi la kutetea haki za kiraia la Russia Behind Bars.

Romanova anaeleza: “Hawana haja ya itikadi; wanachokijali ni uhuru. Wanataka kuwa huru ili kufanya wanavyotaka kama walivyokuwa wakiwa sehemu ya genge, kuwa huru kutoka gerezani, kutokana na nidhamu na mengine mengi.”

Kirby anasema ushawishi wa Wagner Group unaongezeka.

Prigozhin Amewakosoa hadharani majenerali wa kijeshi wa Russia mara kadhaa kwa mikakati yao na kushindwa kwao nchini Ukraine. Wachambuzi wanasema Wizara ya Ulinzi ya Russia imejibu.

Kwa maoni ambayo si mazuri kuhusu kampeni ya uandikishaji inayofanywa na Wagner Group.

Ivan Eland, Kituo cha Amani na Ukombozi. anaeleza: “Wagner Group kwa hakika inashindana na vitengo vya jeshi la Russia, na wanaandikisha watu kutoka magerezani.

Unadhani wafungwa wanateswa na mambo kama hayo, lakini hilo halimaanishi kuwa wana mafunzo mazuri ya klijeshi.”

Inaonyesha jinsi jeshi la Russia lillivyodhaifu,”Brigadia Jenerali mstaafu wa Jeshi la Marekani, Peter Swach anakiri hilo.

Peter Zwack, Brigadia Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Marekani anasema:“Unapokuwa na majeshi mbadala kwa jeshi lako la kwanza kwasababu hawawezi kufanya mambo, hili halionekani vizuri kuhusu hali ya kitaifa kwa jeshi la Russia.”

Mamluki ya Russia wa kikundi cha Wagner wakionekana wanapanda helikopta huko kaskazini ya Mali.

Mamluki ya Russia wa kikundi cha Wagner Group wakipanda helicopter sehemu ya kaskazini nchini Mali Afrika ya Magharibi

Kwa wafungwa kujiunga na Wagner Group wanahisi kama njia ya kutoka gerezani. Romanova anasema hawana motisha ya kupigana, lakini badala yake wanachukulia kujiandikisha kama tiketi ya kuwa huru. Lakini wengi, baada ya kujiunga, wanajaribu kukimbia au kubadili pande na kujiunga na majeshi ya Ukraine – kitu ambacho Wagner Group haikichukulii kwa uzuri. Kwa mfano, katikati ya mwezi Novemba habari zilivuja…

Kanda ya video iliwaonyesha mamluki wa Wagner Group wakitumia nyundo kumuua mwanachama ambaye alikuwa anakwenda kujiunga na Ukraine.

Olga Romanova, Muanzilishi wa Russia Behind Bars: “Wengi walikubali kujiunga na Wagner Grouyp kwa matumaini ya kukimbia. Ndiyo maana wengi wao walijisalimisha, walijiunga - kwa idadi kubwa. Ndiyo maana utaona kuwa mauaji holela. Na hapa ndipo Prigozhin alifanya kosa kubwa. Alidhani mauaji haya yatawatia khofu wafungwa, na hivyo wataacha kukimbia, lakini walichofanya ni kuacha kujiunga na Wagner Group.”

Upelelezi wa Marekani unapendekeza kuwa Wagner Group pia inapata baadhi ya silaha zake kutoka Korea Kaskazini, anasema Kirby. Kwa mujibu wa data za Pentagopn, shehena ya kwanza kutoka Korea Kaskazini ilifika mwezi Novemba, na kwamba Kirby aliongezea, kuwa ni ukiukaji wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja Mataifa.


Source : Kirby: Hujuma mpya yagunduliwa na Marekani ya kundi la mamluki la Russia Wagner
 
Ndugu yangu kwa kuwapa kwa damu!
Unajikata kidole na mwenzio pia, alafu mna badilishana vidole mna kunywa kila mtu cha mwenzie [emoji22][emoji22][emoji22]
 
Ameonesha ujasiri ila alipaswa kupigania haki za watanzania wanaotozwa tozwaal
Habari inasema alienda kusoma, akafanya uhalifu akafungwa.

Kwahiyo yeye ni miongoni mwa wafungwa ambao Russia wamewatoa na kuwapeleka vitani.
 
Inaonesha miaka 2 inayokuja Russia haitakuwa na wafungwa
 
Kwani Nchi ilimtuma au alienda kuoigania Tanzania? Labda alikuwa anapigania Wazazi wake

Alikua masomoni, akafanya makosa, akafungwa urusi, akiwa gerezani Wagner group wakamchukua na kupata mafunzo ya muda mfupi ya kijeshi halafu akapelekwa uwanja wa vita ndio yamemkuta hayo ni ulaghai wa urusi maana iliwalaghai wafungwa kwa kuwaahidi watafutiwa adhabu zao,
 
mtu kajiamulia kwende akiwa na akili timamu, yamemkuta. Ulitaka Watanzani wafanyaje?
 
Alikua masomoni, akafanya makosa, akafungwa urusi, akiwa gerezani Wagner group wakamchukua na kupata mafunzo ya muda mfupi ya kijeshi halafu akapelekwa uwanja wa vita ndio yamemkuta hayo ni ulaghai wa urusi maana iliwalaghai wafungwa kwa kuwaahidi watafutiwa adhabu zao,
Kwani hawajafutiwa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapo unailamu Tanzania kwa lipi? Maana Nchi ilishawatoa Wananchi wake. Aliyebaki aliamua mwenyewe kwa hiari.
 
Bora huyo Amefia vitani ndugu zetu vijijini wanakufa na malaria mpaka leo
 
Back
Top Bottom