All the Best Mkuu,
kila kitu kinawezekana ni juhudi tu na kumwomba Mungu!
Ila Kama hapa Bongo unaweza ukapata income zaidi ya 1.5 m kwa mwezi fikilia mara mbilimbili kabla haujaenda nje.
Nchi ambazo sikushauri Kwenda labda kama una mkataba rasmi wa ajira!
1. Nchi zenye majina yanayoishia na neno"STAN" - zina ubaguzi uliopitiliza kiasi cha kuhatarisha maisha ya mtu mweusi. pia fursa kupatikana ni adimu. Fursa pekee ambayo utaipata tena kirahisi tena kwa minajiri ya kupata thawabu ni kusafisha nyumba za ibada (Wanapenda kutoa fursa hii kwa weusi).
2. East European countries (Poland, Moldova, Serbia, Hungary, Romania, Slovenia n.k). huku kuna ubaguzi na wana shida za ajira kama sisi. Na wenyewe huwa wanazamia kwenda Magharibi.
3. South European countries ( Ureno, Spain, Ugiriki, Saprus, Italy, Ufaransa, Malta n.k) zina hali ngumu ya maisha na Waafrika wengi waliopo huko wanaataabika (wanakufa na tai shingoni) ambapo wengine wanauza pipi na kulala chini ya madaraja. Ila kama una mkataba wa kazi maalumu nenda.
4. Latino Countries; unaweza geuzwa mtumwa au utakuwa zungu la unga au ganstar
Nchi ambazo Nashauri uende!
a. Nordic Countries; Norway, sweden, Denmark, Finland. standard ya maisha ipo juu, watu ni wema na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa.
b. Germany speaking countries; Germany, Austria and Switzerland. standard ya maisha ipo juu na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa.
c. English speaking countries; UK, Ireland, Icelanda, USA, Canada na Australia, Newzealand. standard ya maisha ipo juu, watu ni wema na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa. changamoto ni kuwa living cost zipo juu sana na accommodation ni adimu. watu wana stress sana kutokana na kutingwa na gharama kubwa za maisha. ukilemaa au ukipenda kitonga unaweza ukaolewa na mtu wa jinsia yako, siyo utani.
d. Nchi za watu warefu; Netherlands, Luxmburg. standard ya maisha ipo juu, na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa.
f. Tiger countries; Japan, South Korea, Vietnam. Fursa kubwa huku ni English Teacher. Lakini pia kazi za box zinapatikana.
Note: fursa kubwa ni kuchamba vibibi/vibabu, catering and industrial box.
Njia za kwenda:
1. Omba course za hotel management hasa upishi.
2. Omba kushiriki mikutano ya Kimataifa hasa ya sirikali
3. nenda kashiriki maonyesha ya kimataifa
4. anza kusoma masomo ya lugha Dar then baadaye omba kwenda kuongeza ujuzi katika nchi hizo. Mfano anza masomo ya kijerumani au kifaransa nchini ukihihitimu omba omba kwenda Uswiss au Ujerumani au Austria kujiendeleza zaidi.
5. Kwa ambao wanatoka familia bora ni rahisi kwenda nchi yeyote, nenda kafanye master degree au shahada watakupa visa.
Note: jitahidi kabla ya kwenda West passport yako iwe angalau na visa za South Africa, South Korea, Japan au Israel