Mtanzania usijiroge kwenda kutafuta maisha nje ya nchi. Tanzania kuna maisha yote

Mtanzania usijiroge kwenda kutafuta maisha nje ya nchi. Tanzania kuna maisha yote

Mkuu, ndio utakuwa na fedha za kutosha ila kumbuka jamii nyingi za waafrika wamejaa chuki, ujinga na wivu kutokana na umaskini wao.

Wata anza kukuonea wivu pengine hata kuku ua.

Kuna familia moja ni wakazi wa kisii nchini kenya, walitoka Kuishi Marekani na kuhamia Kenya kuishi na kufanya uwekezaji.

Ila walikuja vamiwa na majambazi,waka uwawa.

Hii ni kutokana na mentality za waafrika wengi kudhani ukitoka Ughaibuni umejaa Mahela sana.

Ndio maana mkuu nakwambia hivi,

Kuishi na waafrika hata kama una Hela lazima ujifiche fiche sana, Maana wana mentality za kipumbavu sana.

Kwa nchi za ughaibuni mfano USA, Hata ukinunua ndege hakuna wa kukuonea wivu ni kawaida sana.

Waafrika wana upumbavu wa milele.

Na mentality za wivu, chuki,husda na tamaa.

Kuishi nao inahitaji Akili sana.

Wana laana, uafrika hasa utanzania ni laana

sasa kama unahela kwanini uishi nao hao wenye mentality hizo.
 
Maisha ya nje ni utumwa labda uende kama mtalii, uwe umepata ajira huko au uwe na hela nyingi kama wanasiasa... Vinginevyo ule msemo wa laiti ningejua utakuwa wako
Acha Fikra za kimaskini.

Perception zako hazi apply kwa wote.

Jisemee wewe binafsi kwamba umeona, maisha ya nje ni utumwa.
 
Hii mada inawahusu ma expert na wale wrnzangu na Mimi, Yaani wale ambao hawana elimu au elimu yako sio dili katika soko la ajira ulimwenguni.

Tanzania ukilipwa mshahara hata millioni Moja na nusu unainjoi kuliko anayelipwa mamilioni huko nje.

South Africa vijana wa kitanzania wanakufa kama nzi.

Huko nje utabaguliwa sana, na maisha ya upweke yana faida gani huku bongo fursa nyingi?

Naona kazi kuendelea kuandika.

Nendeni mkale bata huko ulaya .
Ushatembelea nchi ngapi mpaka ukafikia conclusion hii?
 
huko huko Germany Kuna waliotoboa, wanaishi vizuri na home wame invest. Mbona huwataji hao? Kama mifano ya kuigwa? Kuna wengine nawajua hapo hapo Germany especially wakenya….wengine wameenda kama house girls..leo wamejiendeleza wana taaluma nzuri tuu. Some of them ni madaktari. I know them.
Watanzania tuache negativity. Kuishi nje siyo lelemama. Lazima ukomae kweli kweli. Kama ni kilimo..ni kile cha Nyerere cha kufa na kupona!

Na fursa ya kuishi Ulaya, better was expected from you. But wapi!
Shida sio kuwa na fani shida ni una investment gani ? Ndio sikatai kuna madaktari na kuna watu wanafanya kazi makampuni makubwa lakini kama mtu hana nyumba huku na pia hana nyumba au kiwanja nyumbani huyo tunasema anafanya nini. System ya huku imetengenezwa uwe na hela ya kula na kuenjoy kidogo. Ila ukijibana ukarudi nayo bongo unaweza kufanya mambo makubwa sana. Huku sio sehemu ya kuzeekea tembea ulaya na marekani yote angalia maisha ya wazee. Ndo maana ninawaasa watanzania wenzangu huku ni sehemu ya kujiimarisha na kurudi nyumbani na kupiga hela. Kuna watu wamechukua uraia wa nchi zilizoendelea bado wanakuwa treated kama second class citizens. Wanatamani warudi nyumbani lakini inakuwa too late. Kama tulivyoshuhudia yule Mtanzania Raia wa Uingereza alivyozuiwa pale uwanja wa ndege. Hakuna mtu aliyerudi Tanzania baada ya kujiimarisha kiuchumi na kitaaluma katika nchi hizi anaishi maisha mabovu. Tofauti ni kuna wale watoto wa mama wanalipiwa ada ya chuo na kupewa pocket money hao ndio wakirudi bongo wanaishia kuvuta bangi maana hakuna walichojifunza huku. Namalizia kuwa ili uchukue maarifa muhimu katika nchi hizi zilizoendelea inabidi uwe certified na ufanye kazi usikae kizembe gonga mzigo. Kwenye kazi utajifunza mengi ambayo ukirudi nyumbani uta apply.
 
Hizi ni akili za kimaskini mtu anayeyaogopa maisha.Woga wako ndio umaskini wako.Maisha ni popote itategemea na akili zako.Ukiwa mtoto wa mama lazima uwe na mawazo kama yako.
 
Watu wamegoma kubaki...
Exposure muhimu sana
 
Mimi nipo Ujerumani ninakubaliana na wewe lakini kwa asilimia 50. Ni vizuri kuja nje na ni vizuri zaidi kama umekuja kusoma na kufanya kazi. Lakini ushauri wangu ni kuwa usibweteke ukafocus kwenye kuhamia nje moja kwa moja. Fanya kazi, save hela then rudi nyumbani. Exposure ulioipata huku itakusaidia sana nyumbani, kuna watu wana miaka ishirini Ujerumani lakini hawana nyumba wala investement yoyote. Yaani mtu anaona aibu kurudi nyumbani. Lakini waliorudi nyumbani wamepiga hatua kubwa sana. Nje ukikaa sana ufanye kazi miaka mitano maximum excluding miaka ya kusoma.
Miaka 5 kidogo sana

Entry level ya mshahra hapa ni $50,000/year kwa Canada kama upo single sawa, kama una familia $24,000/year kwa nyumba pekee

Maybe unasave $8000/year

Nunua nymba NHC kwa morgage kisha unalipia na Uber hapo (hii nitaipiga)
 
All the Best Mkuu,
kila kitu kinawezekana ni juhudi tu na kumwomba Mungu!
Ila Kama hapa Bongo unaweza ukapata income zaidi ya 1.5 m kwa mwezi fikilia mara mbilimbili kabla haujaenda nje.

Nchi ambazo sikushauri Kwenda labda kama una mkataba rasmi wa ajira!
1. Nchi zenye majina yanayoishia na neno"STAN" - zina ubaguzi uliopitiliza kiasi cha kuhatarisha maisha ya mtu mweusi. pia fursa kupatikana ni adimu. Fursa pekee ambayo utaipata tena kirahisi tena kwa minajiri ya kupata thawabu ni kusafisha nyumba za ibada (Wanapenda kutoa fursa hii kwa weusi).
2. East European countries (Poland, Moldova, Serbia, Hungary, Romania, Slovenia n.k). huku kuna ubaguzi na wana shida za ajira kama sisi. Na wenyewe huwa wanazamia kwenda Magharibi.
3. South European countries ( Ureno, Spain, Ugiriki, Saprus, Italy, Ufaransa, Malta n.k) zina hali ngumu ya maisha na Waafrika wengi waliopo huko wanaataabika (wanakufa na tai shingoni) ambapo wengine wanauza pipi na kulala chini ya madaraja. Ila kama una mkataba wa kazi maalumu nenda.
4. Latino Countries; unaweza geuzwa mtumwa au utakuwa zungu la unga au ganstar

Nchi ambazo Nashauri uende!
a. Nordic Countries; Norway, sweden, Denmark, Finland. standard ya maisha ipo juu, watu ni wema na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa.
b. Germany speaking countries; Germany, Austria and Switzerland. standard ya maisha ipo juu na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa.
c. English speaking countries; UK, Ireland, Icelanda, USA, Canada na Australia, Newzealand. standard ya maisha ipo juu, watu ni wema na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa. changamoto ni kuwa living cost zipo juu sana na accommodation ni adimu. watu wana stress sana kutokana na kutingwa na gharama kubwa za maisha. ukilemaa au ukipenda kitonga unaweza ukaolewa na mtu wa jinsia yako, siyo utani.
d. Nchi za watu warefu; Netherlands, Luxmburg. standard ya maisha ipo juu, na fursa zipo. hata kama kichwani haupo vema utapata fursa.
f. Tiger countries; Japan, South Korea, Vietnam. Fursa kubwa huku ni English Teacher. Lakini pia kazi za box zinapatikana.

Note: fursa kubwa ni kuchamba vibibi/vibabu, catering and industrial box.

Njia za kwenda:
1. Omba course za hotel management hasa upishi.
2. Omba kushiriki mikutano ya Kimataifa hasa ya sirikali
3. nenda kashiriki maonyesha ya kimataifa
4. anza kusoma masomo ya lugha Dar then baadaye omba kwenda kuongeza ujuzi katika nchi hizo. Mfano anza masomo ya kijerumani au kifaransa nchini ukihihitimu omba omba kwenda Uswiss au Ujerumani au Austria kujiendeleza zaidi.
5. Kwa ambao wanatoka familia bora ni rahisi kwenda nchi yeyote, nenda kafanye master degree au shahada watakupa visa.
Note: jitahidi kabla ya kwenda West passport yako iwe angalau na visa za South Africa, South Korea, Japan au Israel
 
Hii mada inawahusu ma expert na wale wrnzangu na Mimi, Yaani wale ambao hawana elimu au elimu yako sio dili katika soko la ajira ulimwenguni.

Tanzania ukilipwa mshahara hata millioni Moja na nusu unainjoi kuliko anayelipwa mamilioni huko nje.

South Africa vijana wa kitanzania wanakufa kama nzi.

Huko nje utabaguliwa sana, na maisha ya upweke yana faida gani huku bongo fursa nyingi?

Naona kazi kuendelea kuandika.

Nendeni mkale bata huko ulaya .
CCM ni janga.
 
Back
Top Bottom