Mtazamo binafsi: Wanafunzi wanufaika wa mikopo wafungue mashtaka juu ya ucheleweshwaji wa stahiki zao

Mtazamo binafsi: Wanafunzi wanufaika wa mikopo wafungue mashtaka juu ya ucheleweshwaji wa stahiki zao

Ozone_

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
277
Reaction score
352
Habari za mda wanajukwaa.
Moja kwa moja niende kwemye mada husika.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchi kuwa wamecheleweshewa stahiki zao( fedha za kujikimu) kutoka bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Ifahamike ya kuwa hizo pesa ni mikopo na sio misaada kwa wanafunzi hao, ambayo baadae watatakiwa kuilipa tena kwa riba.

Hoja yangu ni kuwa ikiwa watatakiwa kuilipa tena kwa riba, kwa ufaham wangu mdogo ni kuwa ikiwa utachelewa kulipa mkopo ukubwa wa deni hiongezeka, sasa ikiwa ni hivyo je, ni kipi kinatakiwa kufanywa na bodi ya mikopo pale wanapochelewesha malipo ya mikopo kwa wanafunzi.


Nadhani wanafunzi wanatakiwa kutumia futsa hii kuishtali bodi ili na wao wapate riba kwakuwa wamecheleweshewa stahiki zao, kitu kilichopelelea usumbufu kwao..

N.b
Hili linatakiwa kuwa kama sehemu ya practical kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sheria
 
Tathmini zipi na alishatoa notes kwamba hela inaingia tarehe 20 na leo ni tarehe 26 watu hawana kitu
acheni udwanzi mnakaa kulalamika tuu. ingieni barabarani vunjeni hata hilo daraja la ubungo hela itaingizwa
hilo jengo lao si la vyoo tupu na nikaribu tu hapo vunjeni jengo
 
Tathmini zipi na alishatoa notes kwamba hela inaingia tarehe 20 na leo ni tarehe 26 watu hawana kitu
Tulia wewe tulambe asali sisi
Andamaneni

Vitoto vya siku hiz mmekua legelege sana enzi zetu kishanuka mapema 2007-2012

Hela tumeweka fixed account kwanza mtapewa tarehe 01/6

Wapuuzi nyie

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mnajifanya mbogo kwenye kutaka mikopo tuu ila kwenye kulipa mikopo mnaingia mitini
 
Back
Top Bottom