Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

MTIZAMO

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
image.jpeg
 
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha,(alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Hii dhana ilitakiwa uitoe wakati wa awamu iliyopita kwamba kuomba hakufai lakini mlikuwa wapiga zumari wakubwa.Leo mnajidai wazalendo wa kutupa.Siku zote ukitegemea cha ndugu utakufa maskini.SIZITAKI MBICHI HIZI!!!!!
 
Nilichogundua hapa hiki kizee kipo hapa kinatupia like kwa yeyote atakaye kuwa upande wake...yote hii ni U DC hana lolote na ninavyomjua gambe lazima akiteue maana tumekisema sanaa!
 
Huyu PolePole anajitoa ufahamu na kuwa msahaulifu.Eti "Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii" Bunge hili hili na watu waliopitisha katiba pendekezwa ambayo anaililia linaweza kitu kweli?
Lakini kwenye sheria ya mtandao kuna kesi ishafunguliwa, ngoja tuache mhimili mmoja wa dola ufanye kazi yake
 
Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

wewe Slowly-Slowly ungekuwa umeandika maneno yenye gravity hii hii hapa majuzi tu wakati demokrasia ya Zanzibar ilipokuwa inabakwa mchana kweupe, walahi mimi ningekuwa mtu wa kwanza (kama si wasifuri) kukuunga mkono kwenye haya unayoyaandika leo. walahi tena!!

lakini kwa unafiki wako huu, i tell you to go shut the f@347*!@ up!!
 
Hili bandiko ni maoni binafsi ya bwana Polepole ambayo kwa mtazamo wangu binafsi inabidi yapuuziwe kwasababu hayagusii japo chembe ya matatizo tuliyokuwa nayo sasa na hali ya hatari inayokuja mbele yetu.

Tusidanganyane hapa Zanzibar ni tatizo na Zanzibar ya sasa kamwe haitakuwa ile Zanzibar tuliyokuwa tumeizoea kabla ya October 25 mwakajana. Utatuzi wa tatizo la Zanzibar sio rahisi kama bwana Polepole alivyojaribu kuhainisha kwakuorodhesha pande zilizotakiwa kukaa na kujadiri. Tatizo la Zanzibar ni zao la mapungufu ya dhana ya democracy katika nchi iliyojitawala kwa mapinduzi na kisha kukubali democracy ya uso wa vyama vingi. Utatuzi wa tatizo la Zanzibar ni kwa wazanzibari wenyewe kuchagua moja kati ya mapinduzi na democracy.

Wakuu wa dunia ambao ndio wamiliki wa MCC na viranja wa democracy ya vyama vingi wanaungana na Watanzania wapenda democracy kuichagulia Zanzibar democracy badala ya mapinduzi yaliyoifanya Zanzibar ijitawale. Jecha na Watanzania wengine wakaamua kuichagulia Zanzibar Mapinduzi kwa kufuta uchaguzi ambao labda ungeleta ushindi kwa wapenzi wa democracy. Wakuu wa dunia na Watanzania wapenda democracy wamechukia kuona dhana ya mapinduzi ikipewa ushindi wa mezani na democracy ikidhalilishwa.

Tukubali kwamba tumekoroga uji na kwamba MCC imetoa adhabu stahiki kulingana na mandate yake katika ukuaji wa democracy. Binafsi ningeishangaa MCC kama isingetoa adhabu kwetu kwasababu ingekuwa aiamini kile inachohubiri. Na wala tusitafsiri adhabu hii kama namna ya ukoloni mamboleo na wala hailengi kutuingilia Tz kama nchi katika kufanya maamuzi yetu. Adhabu hii inalenga kudumisha na kuimairisha malengo na maono ya wamiliki wa MCC, malengo ambayo sisi wenyewe tulitia sahihi kuyatekeleza kabla Jecha na wenzake kufanya vinginevyo.

Inasikitisha kuona kwamba kwa mara ya kwanza Tz ambayo ilisifika vizuri kwenye nyanja za siasa za kimataifa leo inakuwa mfano wa kutoigwa. Democracy tuliyoipigania kwa miaka kadhaa na kupoteza mashujaa katika vita hivyo leo hii tunapiga U-turn kuelekea utawala usio wa kidemocrasia na tukipata adhabu kwa hilo tunajifanya jeuri kwa style ya bwana Polepole. Ajabu rais wetu anajitokeza hadharani kusema hawezi kuingilia maswala ya Democracy Zanzibar, maswala yanayogusa maslahi ya kipande cha pili cha eneo la utawala wake na pia maslahi ya wadau wa maendeleo yetu ambao leo wamekasirika.

Hitimisho ni kwamba bwana Polepole ameamua kwa makusudi kupaka rangi nyeusi kichwa chenye mvi akizani mvi ni rangi tu. Tumeadhibiwa kwa haki na ni wajibu wetu kutafuta suluhisho la tatizo sugu la Zanzibar! Tusijidanganye, marudio ya uchaguzi hayajatatua tatizo bado, tumepaka tu rangi nyeusi kwenye tatizo na waliotuadhibu wanatukumbusha kwamba mvi ni zaidi ya rangi ya nywele mana kama hivi sivyo wasingetuadhibu baada ya marudio ya uchaguzi.
 
Wanaovunja ni wachache tu na sio wengi.mambo kama haya yanahitaji kura ya maoni ya wananchi wwote. Toa pendekezo basi tuvenje uhusianavna marejani na EU
 
u DC utapata..... Haya sasa elezea kwa upande wa pili madhara ya kukosa hizo fedha
 
Polepole ni moja ya watu waliotumwa kuja kupotosha umma wa watanzania kuhusu hizi fedha za mcc ndani ya mitandao na huku yeye ndo alikuwa wa kwanza kuipigania democrasia hapa nchini kupitia katiba ya warioba ila kwa sasa hiyo democrasia kaipa kisogo ,,duuhh ccm ni hatari asee ikiamua kukuweka mfukoni ni dakika chache sana naona ukuu wa wilaya unamwendea muda si mrefu
Ndo maana tulisema ccm ni ileile na haitakuja kujirekebisha hata siku na moja
 
Hakuna lolote hapo, mdomo tu tumepewa wabongo. Ukitaka kuijua vizur ccm refer umeya wa dar, hakuna hata kiongoz mmoja aliibuka kusema jamani hapa hatuko fair, saiv wanatafuta umoja, me nasema tunyimwe misaada, tuwekewe na vikwazo vya kiuchumi tuone kama polisi wanaweza kupambana navyo.
 
Siungi mkono hoja ya akina Moyo kabisaa. Wapo watoa misaada wanaotoa kwa moyo mweupe kabisaa wa kusaidia nchi hizi fukara ila shida ni katika siasa na baadhi (kama sio wote) wanasiasa na viongozi wetu wa nchi hizi fukara. Wanapewa misaada, wengine wanaiba hiyohiyo misaada na kwenda kuficha kwa waliotoa misaada hiyo. Hapo ndipo shida inapoanzia. Maana hata wenyewe kwa wenyewe tunaibiana, tazama mashirika ya umma mengi utasikia habari za ufisadi na wizi tuu.
 
Hahahah PolePole bwana, Angejiuliza maswali yafuatayo
(1) Je Pesa za MCC tulikuwa tunazihitaji au hatuzihitaji?
(2) Je tulisaini masharti ya MCC hapo awali au la?
(3) Je Kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kulizingatia sheria ya uanzishwaji na ufanyaji kazi wa ZEC au la?
(4) Mbona tulipokuwa tunaqualify kupata pesa za MCC kwa vigezo vilevile vya Demokrasia, kupiga vita rushwa n.k mbona tulikuwa tunafurahia na kujipongeza lakini tulikuwa hatuwaambii hao wahisani kuwa Tuacheni na mambo yetu ya ndani?
(5) Je Uchaguzi wa Marudio ulikuwa wa Kiuwakilishi?, Je unaweza Kusema uliridhiwa na Wananchi wa Zanzibar wakati Kisiwani Pemba tuliona wananchi wengi wakijifungia ndani badala ya kwenda kupiga kura?

Polepole ajiulize
(1) Ni uongozi gani uliooneshwa na tume katika uchaguzi wa marudio lakini uongozi huo huo ushindwe kuonyeshwa baada ya mtu mmoja kufuta uchaguzi wa awali kinyume cha sheria?

Ninachokiona
(1) Waroho wa madaraka wakishindwa kukidhi haja za Kidemokrasia hukimbilia katika "Utaifa" na Uzalendo
(2) Iweje Usaini masharti ya MCC, halafu at one point in time ushindwe hayo masharti usingizie "eti uzalendo" na "heshima ya nchi?

Namwambia PolePole
(1) Uzalendo ni kuheshimu Demokrasia
(2) Uzalendo si kuweka mbele maslahi ya chama na badala yake kuweka mbele maslahi ya Taifa
(3) MCC ni chombo cha serikali ya Marekani, Kauli ya Bodi ni kauli ya Serikali ya Marekani, Ndugu Polepole hapa usizunguushe maneno

Nimkumbushe PolePole

(1) Si miezi mingi iliyopita alikuwa akipigania katiba ya Warioba, Lakini akumbuke Katiba ya Warioba ilisisitiza sana jambo la Demokrasia na utawala wa sheria, basi iweje PolePole ashindwe kuona kuwa kwa misingi yote ya ufutwaji wa Matokeo ya awali hayakuzingatia sheria ya Tume, na Uchaguzi wa Pili ambapo CCM wameshinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba siyo Realistic na hivyo kunajisiwa kwa wazi kabisa kwa demokrasia?

Nimshauri Polepole
(1) Chagua kuwa baridi au moto, usiwe vuguvugu, haki na batili havitengamani
(2) Chagua kuwa kama Martin Luther King Jr kwamba Injustice anywhere is an Injustice everywhere, Na kwamba Justice is Indivisible, Ama Chagua kuwa kama Machiavelli "By any means Necessary"
There is NO Universal definition of democracy and so does its application......

African democracy and its application is very different friom that of Americans and other European Nations......

Soma vizuri hiyo article ukiwa hujaielewa isome tena na tena ukishaelewa majibu utakua umeyapata.....
 
Misaada sio muhimu kwetu ila kwa hili la ubakaji wa demokrasia uliofanyika ZnZ ni uroho wa madaraka. JPM sio kama alkuwa hajui kuwa watapora demokrasia Znz HAPANA, alilijua fika na madhara yake pia aliyajua na hivyo alituandaa kisaikolojia kuwa hapendi msaada hapo tusiangalie msaada tu mwisho wa siku hata mahusiano na hizo nchi utakuwa sio mzuri. Hii yote ni kutokana na mijitu michache miroho ya madaraka.

Kuhusu azimio la Arusha dhima yake kubwa ni udikteta na sio kujitegemea kma inavyowekwa na kusemwa juu juu tu
 
Usitudharau kiasi hicho
Unatuambia tufunge mkanda wakati mkanda wenyewe umefika mwisho
Labda nyie mnaoishi kwa kuiba fedha za serikali mpo tundu la mwanzo
 
MY PRESIDENT HAS DISAPPONTED ME IN THIS, WE REAP WHAT WE SOW, AMERICANS ARE NOT CHINESE
 
Baada ya kutoka taarifa za Tanzania kukosa pesa za MCC na kuondolewa kabisaaaaa katika list ya kusaidika na MCC
Nimeona watu kibao wakibadilisha akili zao makusudi na kuanza kusema kuwa ndio muda wa Tanzania ya Viwanda kuchukua hatamu.
Tujiulize maswali yafuatayo:-
- Nini ni kiini cha kukosa pesa hizi ambazo zinge-boost miradi ya umeme, barabara na maji kwa wananchi hohehahe, wanaoishi vijijini?

- Je Maslahi ya Chama cha Mapinduzi ni maslahi mapana ya Tanzania na watanzania wote?

- Je misaada na mikopo kutoka Uchina ndio sababu ya kuwa na kiburi, kutesa, kunyanyasa raia na kutawala kwa mabavu?

-Je Hiyo Uchina na Urusi zimepata mafanikio ya kiuchumi pasipo makampuni ya Marekani na Nchi za Ulaya kuwekeza kwao?

- Hali itakuwaje kama Marekani anaamua kuiwekea Tanzania vikwazo vya ki-uchumi. Korosho na Katani tutauza Afrika hapa hapa?

-Tanzania ya Viwanda itapata wapi teknologia na mashine? Au kiwanda cha Nyumbu na textiles vitaokoa taifa hili linalo import mpaka toothpicks na viberiti?

- Je uchumi ukidorora, mfumuko wa bei na pesa kushuka thamani...wanasiasa wanaotupatia haya madhila watasemaje? Au ndio yale ya Mugabe Zimbabwe inadidimia, Mke na Mwanae wanafanya shopping Uchina?
-Je uko tayari kuumia kwa ajili ya maslahi mapana ya Chama cha Mapinduzi kwa mwamvuli wa utaifa na uzalendo bandia?

Uhuni wa CCM usiwe tiketi ya kuchafua taswira ya Tanzania. Kama muda wa kuondoka umefika, kabidhi madaraka kwa chama kingine. Tumeanza na pesa MCC, mwishowe itakuwa kuuwana kinyama. Jifunzeni Mashariki ya Kati....Syria yamebaki magofu, Iraq, Misri e.t.c
 
Duh hili shipa la MCC naona vijana wa Lumumba wanakazana kweli kweli lakini wanakwepa ukweli mchungu kwamba demokrasia imesiginwa Zanzibar.
 
Mimi siungi mkono ya akina Dambisa,ikulu itoe oficial statement,ni nini hasa kilichopelekea sisi kupokwa hii nafasi ya msaada wa MCC?
 
Limekuwa gumzo ambalo limesababisha mitazamo mbalimbali miongoni mwa Watanzania. Wengine wakienda mbali zaidi hata kuuweka uzalendo pembeni hata kuiombea nchi yetu mabaya kama vile mkwamo wa uchumi kana kwamba wao wanaishi sayari nyingine. Hizi ni zile fedha ambazo hutolewa na MCC takribani shilingi trioni moja.

Wafadhili hawa wamezikatalia fedha zao kwa hoja ya kukandamizwa demokrasia huko Zanzibar(wanavyodai wao) na ile sheria ya mitandao ikidaiwa kudidimiza haki za binadamu.

Mimi binafsi nimebaki na mshangao si wa kuwashangaa waliokatalia fedha zao bali ni mshangao wa kuwashangaa Watanzania wenzangu ambao wamesukumwa na hisia za kisiasa kuunga mkono ukoloni mambo leo. Wanaounga mkono ukoloni mambo leo sijui aidha wanafahamu agenda za haya mataifa ya Magharibi au hawajui kwa kuwa hisia za kisiasa zimetawala fikra. Ni nani kawaaminisha watu hawa kuwa Mataifa ya Magharibi yakiiongozwa na Marekani yanademokrasia ya kweli na yanapenda haki!

Je, haki na demokrasia ipo katika kusababisha vifo kwa watu wasiokuwa na hatia wala wasiojua nini maana ya uongozi raia wa Libya, Iraq na Syria? Bush alipoivamia Iraq kwa kisingizio cha kuwepo silaha za nyuklia, zilipokosekana na ilhali watu wamekwishapoteza maisha ni nani alimwajibisha au Marekani kama nchi iliwajibika vipi juu ya haki ya kuishi ya watu wa Iraq?

Mfaransa na washirika wake wameiharibu Libya nchi ambayo watu walikuwa wakipata haki katika huduma za kijamii ambazo ukizitaja hadi unalengwalengwa na machozi ukilinganisha na Libya ya leo, nani kamwekea vikwazo?

Wao wapenda haki mbona wamewaua hata ndugu zao kwa "black propaganda" ili waivamie Mashariki ya kati, waibe mafuta wanavyotaka? Martin Luther King Jr, John F. Kennedy na wengine wengi wamewapeleka wapi hawa watenda haki?

Kama Marekani ni kinara wa kuijua haki na demokrasia wametusaidiaje kuondokana na unyonyaji unaofanywa na makampuni ya kwao yanayochimba madini hapa nchini? Mbona wao ndiyo waliotega mirija yao kuendelea kuididimiza Tanzania kama kweli wanatuonea huruma? Wangekuwa ni waungwana kama wanavyojinasibu basi wangetufundisha kuvua samaki na si kutupa samaki ambaye tukila tukimaliza tunaenda kupiga magoti tena kwao watuongeze mwingine.

Ni mengi sana tunaweza kuyasema kwa uchungu Watanzania tulionauchungu wa nchi yetu, sasa ifike wakati tuseme kwa heri MCC, kwa heri Marekani na pesa zenu zenye ajenda ya siri. TANZANIA ilikuwepo kabla ya MCC na itaendelea kuwepo baada ya MCC.
 
Back
Top Bottom