Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Nonda #87

Ubutu wa kufikiri ni tatizo kubwa nchini. Muungano upo naturally, ni kuweka misingi ya kuimarisha uwepo usiwepo tutakuwa pamoja iwe iwavyo.

Muungano haulindwi na maderaya.USSR isingesambaratika, Shah wa Iran asingefia ughaibuni. Itafika mahali haitawezekana

Mfano, kauli ya Sitta katika video imelenga kudhoofisha muungano badala ya kuujenga

Wanaondoa suala la siasa katika majukwaa wanalipeleka katika imani.

Hawajifunzi, ktk mambo yote duniani, imani inaonekana inaunganisha watu kwa nguvu

Siku nguvu hiyo itakapotimia, dereya, mizinga vifaru havitakuwa na kazi.

Shah wa Iran anajua, Mfalame wa Hungary anaju, Gorbachev anajua hilo

Niachie hapo

Bilioni 5 kwa maagizo wakijua SMZ haitolewi kwa karatasi.
Ilihitaji nini basi kufanya uchaguzi na kutumia migharama yote hiyo? Jipu
Gharama za kuweka majeshi kule hazielezeki na sijui kama si jipu

Rais alisafiri na kuacha shughuli za umma achilia mbali gharama kwenda kuomba MCC.
Wakati huo walijua ili kupata lazima demokrasia ya watoaji itimie.

Walirudi na kutamba, tumepewa kwasababu ya utawala bora na demokrasia!

Leo wanarudi na hadithi za kipuuzi wakituma wapambe eti MCC isiingilie Demokrasia yetu.

Huko nyuma walisifia demokrasia yetu kama kigezo cha kupata MCC.

Unaweza kuona kwanini wazungu wanatuendesha!Hatujitambui. Tulienda kuomba! jipu

Wakatueleza miradi ni matokeo ya safari za Rais na Demokrasia nchini.
Leo wanaponda eti ''tunaweza bila misaada''!
Kwanini hatukuweza wakati ndege zinaruka kwenda NY kila subuhi?

Wanaona hasira za wananchi, wanatuma wapambe watushawishi uzalendo!
Huu ni utoto! Uzalendo leo! Uzalendo gani mapesa yametumika katika ze comedy ZNZ

Hakuna cha uzalendo, ukweli unabaki pale pale MCC wapo sahihi.
Tuliende kuomba wenyewe. Tumeshindwa kujisimamia sasa wakitusimamia tuna ng'aka

Tutaanza kulipia nguzo za umeme kwasababu hawana pesa, zilikuwa za MCC
Gharama hiyo wanatupambaza eti uzalendo

Hili tusimame pamoja, hatuwezi kuwa Taifa la watu 100 au 200 ni watu milioni 45 .

Hatuwezi kudanganywa na uzalendo wakati uzalendo umewashinda wao.

Hawawezi kufuja mapesa kwa ze comedy wakitushawishi ni uzalendo
 
- Gharama na utu wetu kama Taifa hauwezi kupimwa kwa Shillingi Trilioni Moja kwanza ni matusi makubwa sana, Wamarekani walupomuua Chief Abiola Nigeria kusudi waibe mafuta yao hatukusema kitu sio kwamba hatukujua, Walipoivamia Iraq walisema kuna Chemical Weapons mpaka leo hawajaziona, Walipomuibia kura Al-Gore hatukusema kitu, Walipomuua rafiki yao wa zamani Saddam Hussein hatukusema kitu,

- Zanzibar ni Taifa huru lenye Sheria na Katiba yake ambayo inasema kama kuna aliyedhulumiwa uchaguzi anatakiwa aende Mahakamani, Muungano wetu hauna uhusiano na Uchaguzi isipokuwa Ulinzi kwa waliochaguliwa na Serikali iliyochaguliwa, so

- Wabaki na misaada yao, Tulikuwa watumwa once sio wakati wote!!

le Mutuz
 
Kuna nini basi hata hao wasimamizi wa kimataifa wakashindwa kuyaona hayo mapungufu unayoyasema wewe?

Nakwanini hawaku complain chochote juu ya uchaguzi wa Tanzania Bara?

Kikwete alipokwenda MCC hakujua vigezo vya democrasia iliyozungumziwa?
 
tufike sehemu tujikubali,,ipo siku watatuonea wivu,,ndipo misaada yao haitakuwa na mashart makali,,mcc safar njema natambua ipo siku mtarud kwa jina lingine namsipe nafas kirahis kama mlivyo ingia.
Hivi unajua kuna misaada ya aina ngapi kutoka marekani? MCC ni misaada ilionza kutolewa baada ya kuanzishwa taasisi ya MCC mwaka 2004 na serikali ya marekani. sifa ya kupewa msaada huu ni utawala bora na demokrasia. Kwahiyo kuna misaada mingi tuu huo mmoja ndio umefutwa.
 
Na ili nchi yetu ipige hatua katika nyanza zote tunahitaji misaada ya utaalamu zaidi kuliko fedha ili tuweze kujitegemea
Na km mataifa haya wanayojiita wahisani wangekuwa na nia njema wangekuwa wamewekeza ktk elimu ambayo pekee ingelikwamua bara la Afrika badala yake wamekuwa mstari wa mbele kuinyang'anya afrika wataalamu wote na kuwaweka katika taasisi zao za kinyonyaji zinazoitwa za kumataifa
Sera ya deindustrialization pekee ni pigo kubwa ambalo AFrika tungekuwa na uhuru wa kulazimisha bidhaa zinazozalishwa kutokana na malighafi inayopatikana afrika viwanda vyake vijengwe afrika . Afrika ndo lingekuwa bara lenye viwanda vingi kukiko yote
(OMBA OMBA HAJAWAHI KUTAJIRIKA)
(HAKUNA UTUMWA MBAYA KM UTUMWA WA AKILI)
 
Hizi story mnazileta Leo baada ya kunyimwa msaada.
Kwanini maneno haya hamkua mkiyasema wakati tukipokea misaada?
Ni katiba ipi inayotoa nafasi ya kwenda kupinga matokeo ya urais mahakamani?

Wehu wa CCM leo mtaharisha viwavi jeshi vyote ila kwenye hili la MCC hampindui.
 
Stupid Kama sio marekani ku_subsidise dawa za ukimwi tungelikuwaje afrika hasa tanzania
 
Polepole hina tofauti ns dada poa wanaouza utu wao kwa pesa. Njaa na ussliti vinakusumbua. Ulale mahali pema peponi na usaliti wako
 
"Rai yangu kwa Vyama vya upinzani nchini jaribuni kuweka utaifa kwanza na siasa baadae" kwa yaliyofanywa zanzibar tutakuwaje wazalendo? never ever!
 
Humphrey Polepole, ishukuru sheria ya makosa ya mtandao! Natetea sana nchi kujenga uwezo wa kujitegemea na kuthamini uhuru wake bila kuingiliwa na taifa lingine kwa kisingizio cha misaada. Lakini yule anayejaribu kuupotosha ukweli kwa maslahi yake au ya kikundi flani kwa makusudi ni mmbaya zaidi.
 
"Rai yangu kwa Vyama vya upinzani nchini jaribuni kuweka utaifa kwanza na siasa baadae" kwa yaliyofanywa zanzibar tutakuwaje wazalendo? never ever!

Inavyoonekana magufuli hautaki upinzani ila kwa sasa ni bora akajiandaa na uasi
 
Mkuu Polepole nani asekufahamu?me sijaelewa wanunuliwa bei gani.Lijapo suala la utaifa tuache unafik na kuganga njaa.
 
hivi Karibuni utapewa U-DC , ukifika huko waambie wananchi kuwa hawatapata umeme walioahidiwa kwa sababu pesa ya MCC uliikataa. Usisahau kufagilia Sheria ya Makosa ya Mtandao na Ukiukwaji wa Demokrasia.
mpaka sasa sijui kilichokusibu ppole. Haiwezi kuwa njaa!!!
 
Kada mweleze huyo mjinga hajielewi pambaf
 
Ahahahaha umeongea ya moyoni sna umenipa raha unajua sana ila magu ajue zile barabara alizokua anatamba amejenga na serikali yake sasa cjui alikua ajui ni mcc matambo ya musa yalimkosti kwa mungu sasa musa magu kumbuka tena na mabango ujayatoa kule ya msaada wa watu wa marekani au ndo anahisi ashavuka mto na wachina wake njaa tutapata wote lkn chama kitalaumiwa akumbuke hilo ndugu ndugu tuendelee kuwakumbusha sana wasilale
 
MCC walichokifanya si kizur sana lakini ni kizuri coz wametuonesha madhara yakuwategememezi . Watanzania tunapaswa kujitahidi sana tufanyekazi sana ili tuongeze kipato kwetu na taifa kwa ujumla. America inatufundisha somo na hayo ndio madhara yakutegemea. Watz tupigeni kazi tuuze bidhaa na mazao nje.
 
Wewe Mawazo yako yanaona Leo tu wala si hata kesho? Nani kakwambia kuwa msaada uliositishwa utakuwa wa MCC tuu?

Hebu usiwe Na Mawazo mgando huu ni mwanzo tuu misaada mingine itasitishwa Kwa awamu Kama ilivokua inatolewa.

Na cha kushangaza zaid wewe si lolote si chochote Kwa Tanzania, Waziri analialia ambaye anajua athari Kwa wazungu hapo ujue hakuna kitakachotoka.
 
Tatizo nilionalo hapa ni tafsiri ya kile Marekani inachomaanisha.
Kama Marekani yupo kimaslahi zaidi je,huu hautakuwa mwanzo wa mvutano mkubwa zaidi kati yetu na hawa mabwana wakubwa na wenzao?
Kama ndivyo,je,tumejiandaa kwa vita hii ya kimaslahi na Marekani?
Je,wale wanaotupa kiburi(naona watu wanajivunia mchina humu jf)wanao uwezo na dhamira ya kutusaidia pale wakubwa hawa watakapoamua kutushughulikia?
Je,ni lazima sana kutofautiana na mmarekani kwa wakati huu na kwa sababu zilizopo za masuala ya Zanzibar na cybercrime?
Hatuna njia nyingine ya kidiplomasia ya kuishi na hawa wakubwa huku maslahi yao na yetu yakienda sambamba bila ugomvi?
Ni lazima sana kukingiana kifua na mmarekani kwa sasa?Itatusaidia au itatuumiza?
Hekima inahitajika kuliko nguvu hapa.
Magufuli my friend,be very very veeery careful na hili suala..nakutahadharisha sana,now you need your head.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…