Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Huyu tangu awe nduwila kuwili na kupiga domo kwiiingi amepuuzika like a used toilet paper.
 
Unapaswa kujua Misri haipo chini ya MCC ndiyo maana inapokea misaada tofauti na nchi zilizopo chini ya mpango wa MCC.

Kuna eligibility ya kupata misaada chini ya MCC ambayo ni utawala bora, demokrasia na haki za binadamu. MCC wamesema sisi tumekosa sifa kwa sababu ya uchaguzi wa Zanzibar na Sheria ya makosa ya mtandao. Sasa wewe unalinganisha Tz na nchi isiyo chini ya mpango wa MCC. unatoka nje ya mada na eligibility requirements za MCC Hivyo huwezi judge kwanini Misri apate wakati sisi hatupati.

Misri wanapewa fedha kama Fidia ambayo waliahidiwa Kumaaliza Vita Na Israel, Misri wanapewa Fidia Kwa sababu Israel Iliwanyemelea kivita bila kuwatangazia Vita na Wakaharibu Vifaa vyao vya Kivita na Mali nyingi. Hayo yalikuwa ni Makubaliano ya Kupatikana amani kati ya Misri na Israel. Sio Msaada per ce
 
mlipokuwa mnachezea demokrasia hamkujua kuna MCC? kuna mtu humu namuunga mkono anaposema kwenye hili la mcc hawezi kuvaa uzalendo wa kinafiki. mleta uzi unaandika upuuzi wa karne eti sijui madini, mapori tele, haya yote sio mageni hapa nchini, kilitushinda nini kuendelea mpaka rais wetu aliyepita akawa anasafiri kaila siku kwenda kutuombea kibaba? propaganda kwwnye huu upuuzi wa ccm huku mkijifanya nchi kwanza kumbe pembeni ni ccm kw
Anahalalisha walichokifanya Zanzibar.
 
Tumbo linatuponza wengi,unaweza kujitoa ufahamu bila aibu,mleta mada kwann wamesahau kukupa ukuu wa wilaya .mmelikoroga mlinnywe full stop mengine ni blah blah unaleta
 
Huwezi kukataa misaada yote, mingine ni yakistaarabu!

Sijaona ubaya wa MCC.
Wamefadhaika na uchaguzi Zanzibar.Sidhani kama kuna watanzania wengi waliofurahia uchaguzi ule.
Wamepigia kelele sheria ya utandawazi.Watanzania pia kwa ujumla wao walipinga sana hii sheria.
Ni ustaarabu gani unaozungumzia?
 
CCM ya sasa wanasema wataendelea na Katiba Pendekezwa,Polepole anasema waliokwamisha katiba ya Warioba wamehamia UKAWA,huyu mpumbavu aseme nini nimwamini
 
Sijaona ubaya wa MCC.
Wamefadhaika na uchaguzi Zanzibar.Sidhani kama kuna watanzania wengi waliofurahia uchaguzi ule.
Wamepigia kelele sheria ya utandawazi.Watanzania pia kwa ujumla wao walipinga sana hii sheria.
Ni ustaarabu gani unaozungumzia?
Haya ni mawazo yako usiwasemee watanzania wote! Kama ni watanzania wote mbona wengine wamepiga kura za marudio?
 
Tukifanikiwa kufanya exportation zaidi kwa bidhaa zetu Na tukazuia importation za bidhaa kama sticks Na bidhaa nyingine ambazo tu naweza tengeneza hapa basi haya yote yasingetokea umaskini mmbaya sana ila siungi mkono hoja ya Polepole kuwa MCC kutotoa Pesa ni hasara kwa mashirika binafsi lazima itakula kwetu tu uwe ccm cuf au chadema hili ni pigo heavy tu.
sawa je wakikuambia huruhusiwi kuruka 20,000ft kutoka usawa wa bahari na kusafiri zaidi ya 5km ndani ya bahari tutafanyaje maana hawashindwi ata kuleta yale mandege yao yapo kama popo yakawa yanakatiza kwenye anga letu je tunauwezo wa kupambana nao!!??
 
Pole pole sababu walizotaja MCC (dubious election in Zanzibar na Cybercrime) zina chembe ya ukweli au hakuna? Kama ukweli upo hakuna namna ya kukwepa lawama hapa. Kama wao ndo wametunyima kabla sisi hatujakataa basi hoja zako zinakosa nguvu.
Tatizo la msingi lipo ila tunarukiarukia vijisababu na historia tofauti. Tuna tatizo tulitafutie ufumbuzi siyo kujishauwashauwa. Yawezekana wana malengo yao mengine lakini tatizo tunalo tukubali hilo kwanza kabla ya kujitetea uwongo.

Tusikiuke misingi ya haki halafu tuseme tuna demokrasia yetu inayokua taratibu. Kama ndiyo hivyo tuachane na mambo ya kuwa na katiba haina haja. Maana tutasema katiba na sheria zetu zina historia ya ulaya au Asiatuachane nazo na tuifanye ndo demokrasia yetu. Viongozi wa Afrika wakibanwa kuhusu kukiuka misingi wanakimbilia this is African democracy.
 
MCC walichokifanya si kizur sana lakini ni kizuri coz wametuonesha madhara yakuwategememezi . Watanzania tunapaswa kujitahidi sana tufanyekazi sana ili tuongeze kipato kwetu na taifa kwa ujumla. America inatufundisha somo na hayo ndio madhara yakutegemea. Watz tupigeni kazi tuuze bidhaa na mazao nje.
Upo sawa ila hapo kwenye nyeusi ondoa kabisa hatupaswi kuuza mazao ghafi tuuze bidhaa zilizotokana na hayo mazao kwani hata sasa hatuuzi mazao nje si tunauza.
 
Huwezi kukataa misaada yote, mingine ni yakistaarabu!
Nchi za dunia ya tatu zinategemea wahisani na wafadhli kujikwamua kimaendeleo. Nchi zote zinazotoa misaada kuja kwa nchi masikini ni nchi za kibepari.

Sasa nitajie misaada yote na inapotoka kuwa huu ni wakistaarabu na huu si wakistaarabu kwa data rasmi na sababu ya kusema kwanini huu ni wakistaarabu au sio wakistaarabu.
 
Polepole nae msanii tu!Yaliyotokea zanzibar kuhusu mzozo wa kisiasa zijafurahishwa nayo kipi hujafurahishwa nacho si hamna tatizo asa mbona unaweweseka mara misri mara palestina hayo yanakujaje?Mhe. Kikwete alishawahi kusema wajinga ndo waliwao.........!
 
Msikilize mtu anasema hataki msaada wakati hata matangazo ya siku ya choo yanafadhiliwa na watu wa Marekani
Je makusanyo ya Magu yatanunua dawa za ARV wanazopewa waathirika nchi nzima bure kwa msaada wa wahisani,wakati malaria inaua watu wengi kuliko ukimwi na hakuna dawa ya bure
Aah!...yako mengi mengine
Tusubiri tuone hili picha la kihindi linaisha vipi..........Watanzania ni mabingwa wa kuandika riwaya
 
Upo sawa ila hapo kwenye nyeusi ondoa kabisa hatupaswi kuuza mazao ghafi tuuze bidhaa zilizotokana na hayo mazao kwani hata sasa hatuuzi mazao nje si tunauza.
sawa ataondoa je wakikuambia bidhaa yako haijakizi viwango ata kama we unajua imekidhi viwango wakakuambia inabidi waichome moto na petrol ambayo haijachakachuliwa kutoka kwa gadafi ambaya alikuwa na sauti ambayo ata baada ya miaka 200 tutakuwa hatujaifikia !! tutafanyaje?
tafakari chukuwa hatua!!
 
Haya ni mawazo yako usiwasemee watanzania wote! Kama ni watanzania wote mbona wengine wamepiga kura za marudio?
Hapo nimekuelewa.Naona kwa mtizamo wako Uchaguzi Vsiwani ulikuwa wa huru na haki na MCC walipaswa kutupa pesa yete kwa vile Dr Shein alipata ushindi wa kishindo wa asilimia 92%.Tupo pamoja!
 
Polepole amekuwa kichaa siku hizi coz anataka ukuu wa wilaya
 
KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Ovyo kabisa kama mliyaona hayo mapema kwanini msingezikata, kwanini leo wamegoma kutoa ndio mnaanza kutoa sababu za ovyo kuficha ukweli,suala la zanzibar na sheria ya makosa ya kimtandao wamesema uongo?au mnatafuta sababu ya kuwaambia wadanganyika,tuache kujifariji au mnataka mpaka mama ntilie alipe kodi,? Makusanyo ya 1.3 tr kwa mwezi hayatoshi kukidhi bajeti ya 25tr tungekuwa tunakusanya 3tr au 4tr kwa mwezi apo tungeringa lakini sasa ni porojo tu kila mtu anajidai mchumi
 
Nchi za dunia ya tatu zinategemea wahisani na wafadhli kujikwamua kimaendeleo. Nchi zote zinazotoa misaada kuja kwa nchi masikini ni nchi za kibepari.

Sasa nitajie misaada yote na inapotoka kuwa huu ni wakistaarabu na huu si wakistaarabu kwa data rasmi na sababu ya kusema kwanini huu ni wakistaarabu au sio wakistaarabu.
Misaada ya kistaarabu ni ile ambayo haiambatani na masharti. Unafahamu kwanini Baba wa Taifa alielekea China kuomba msaada wa kujenga reli ya TAZARA? Ni kwasababu nchi za magharibi wakati ule zilitoa masharti mengi ikiwemo kutounga mkono jitihada za nchi za Kusini kujipatia uhuru wao!
 
Hapo nimekuelewa.Naona kwa mtizamo wako Uchaguzi Vsiwani ulikuwa wa huru na haki na MCC walipaswa kutupa pesa yete kwa vile Dr Shein alipata ushindi wa kishindo wa asilimia 92%.Tupo pamoja!
Nimekuambia usiseme "watanzania"! Mimi na wengine kama milioni 30 hatuna mawazo kama ya kwako! Semea NAFSI yako na siyo kujumuisha watanzania wengine!
 
Back
Top Bottom