Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Masheta. Wa kupinga watapinga tu ngoja uoneee
 
Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu.

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje.

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo.

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka.

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo.

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu.

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana?

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake.

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar.

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii.

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa.

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).
*************

Imeandikwa na: Humphrey Polepole.
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
 
Hata mimi naona hao mcc wana jambo nyuma ya pazia. Ni kweli Zanzibar mambo yalipinduliwa pinduliwa lakini kwa wakati huu hakukuwa na njia rahisi hasa ukizingatia kuwa seif aliweka msimamo mmoja tu kwamba mshindi atangazwe. Nadhani ingekuwa na itakuwa ajabu mno leo tume iseme inatangaza matokeo ya October 2015. Kwenye mazungumzo yoyote hamuwezi kuafikiana ikiwa kila mtu anakuja akiwa na msimamo anaotaka yeye. misimamo kama hii ndio iliharibu bunge la katiba, wameingia kwenye bunge kila chama kina katiba yake kichwani hakuna anayemsikiliza mwenzie hatimaye ukawa wakasusa. Najua ccm ndio chanzo cha shida hii lakini viongozi wa upinzani wapunguze kususa! Hivi Nyerere (rip) angemsusia mkoloni tungepata uhuru 1961?
 
Nguo ya kuazima
 
Magufuli usimsahau huyu mbaba katika ufalme wako hakika ni Tunu kwa taifa tusimpoteze huyu kijana.
 
Nchi huru zote duniani kuna taratibu na kanuni zake ,haiwezi kuwa nchi huru iamue inavyotaka jumuia za kimataifa zipo kuna taratibu zake ,kanuni zake ,sharia zake ndivyo ulimwengu unavyoenda ,tunaona Syria ni nchi huru ,Iraq ni nchi huru ,Libya ni nchi huru ,jumuia za kimataifa hazikukaa kimya ,tujiulize tulikotoka na tunakoenda wapo washauri wasomi ila ushauri wao si wa kisomi
 
Makala ya Ndg Pole Pole ni ya kinafiki na imejaa uzandiki.

1.Masharti ya MCC yapo wazi.Ni utawala bora na haki za wananchi kiuchumi,kisiasa na kijamii.Haya ni masharti ya kistaarabu na yanalenga kumlinda mwananchi.Na ni wananchi ndio walionza kumlalamikia Jecha na sheria ya makosa ya mitandao kabla ya marekani kufuta MCC 2.Ni kilio cha wananchi kimefanya MCC 2 iote mbawa.

2.Ni kweli huko nyuma tumewahi kuvunja mahusiano na Ujerumani Magharibi na Uingereza.Tofauti ni kwamba wakati huo tulikuwa na sababu za msingi na tuliungwa mkono na nchi zingine nyingi tu.Hili la sasa eti tuvunje uhusiano na Marekani kwa sababu ya ujinga wa Jecha sioni kama lina mashiko yoyote.

3.Anasema MCC 2 isingetusaidia lolote kwa sababu walengwa ni sekta binafsi marekeani.Mi nachojua MCC 2 lengo lake ni kusambaza umeme vijijini.Nchi hii ina sera ya kuvutia wawekezaji.Sasa kama wawekezaji wa kimarekani wakija na watu wanaoishi vijijini wakapata umeme tatizo ni nini?It is a win win situation.Kama MCC 2 ilikuwa ni mbaya hivyo basi tungeukataa tangu mwanzo.

4.Anasema Marekani ndio inahitaji zaidi MCC 2 kuliko Tanzania.Anasahau kuwa Tanzania tuna madeni lukuki.Deni la taifa ni trilioni 42.Deni la wakandarasi ni trilioni moja.Deni la PSPF ni trilioni moja 1.Hiyo trilioni moja na ushee tunayokusanya kwa sasa inatumika kulipa mishahara na kulipa madeni.Hatuna hela ya kutosha ya kufanya maendeleo.Ndio sera ya kujitegemea ni nzuri ila mpaka tuje tuweze kusimama wenyewe bado tunahitaji misaada.

Kwa kifupi Ndg.Polepole amejitoa ufahamu kukataa kukiri kuwa yalifanyika Zanzibar hayana ata punje ya demokrasia na hata hiyo sheria ya makosa ya mitandao haina tija yoyote kwa mwananchi wa kawaida zaidi ya kumminya uhuru wake.
 
Amejenga Hoja vizuri sana lakini alivyozungumzia swala la Zanzibar hapo kaweka mambo ya kichama zaidi na siungi mkono hoja hapo lakini kwa mengine naunga mkono hoja yake.
Kwa Zanzibar ilitakiwa CCM wasilazimishe mambo badala take waache Democrasia iamue
 
Hyu sijui pole pole au mbole mbole si muelewagi mada zake zote,anajifanya anajua kuchambua, kumbe anachambua pumba tu kila wakati yeye ni kuitetea CCM hata kile kilicho wazi kabisa machoni mwa watu yeye yupo against nacho,ni nani hajui uupuzi wa CCM wa waliofanya kule Zanzibar?hata mtoto mdogo anajua wewe mbole mbole unakuja kudanganya watu hapa, mambo ya uzalendo, uzalendo,kwanza wewe siyo mzalendo wewe ni kibaraka wa CCM na shangaa na juhudi zote hizo za kujipendekeza hawakupi hata cheo,naona hata wao hawakuamini pia,Kwani ni lazima Tanzania bara au visiwani iongozwe CCM kila siku?ni lazima tufike mahali tukubali demokrasia ifanye kazi yake, wewe unaejifanya mwanasheria sijui wapi?ile tume ilikuwa na haki ya kufuta uchaguzi bila kufuata kufuata utaratibu wake iliyojiwekea,au Jecha ndiyo tume?Hatukubali tumie kwasababu ya maslahi ya watu wachache,ambao kila siku wao wanataka kuongoza wao tu,wengine hawafai..Mbole mbole ujiangalie wakati mwingine sio kila kitu wewe uchangie kuwa unajua,wakati hujui,unakubali makosa halafu unasema hukupenda,pia ukisema habari ya mahakama wakati unajua mahakama zetu ni za chama,Jaji mkuu anachagulia na huyo huyo unaeshindana nae halafu unategemea haki upate wewe kweli inawezekana?
 
CCM wameamua kumchinja polepole mazima? hata vipindi vya TV simuoni tena, wafadhili wake wamemtupa??
Ni ajabu na ujinga kuihifadhi c0nd0m ukishaitumia kwa ajili ya badae, dawa ni kuitupa tu
 
Maneno ya kweli na mifano halisi likini katika matumizi mabaya.

Hatulazimishwi demokrasia tunatakiwa kuiheshimu demokrasia.

Kwa kushindwa kufuata na kuenda haki tutalia na kusaga meno.

Amerika ina haki ya kufanya hivyo. Tunawajibu wa kuilaumu CCM. Fikiria walivyokomalia umeya wa Dar, walivyokanyaga haki nyingi za binadamu. JPM analofanya hakuna bila haki, ni ubatili mtupu
WEWE FUMBUA MACHO UONE,,,,,mimi ninacho fahamu kuhusu upinzani ni kuisababisha serikali iliyoko madarakani ifanye kazi kwa juhudi,,,hivyo lazima ikosolowe,,,sasa ikifikia hatua upinzani unakosoa hadi mambo mazuri,,,hatua nzuri za kupata uhuru wetu,,, TUTAANZA KUWA NA MASHAKA NA NINYI,,,sioni haya kusema kuwa inawezekana NINYI NI MIZIMU ya marekani ndo maana mnasisitiza Tanzania IWE TEGEMEZI HADI LEO MIAKA 55,,YA UHURU,,,,,HADI LINI?????SOMA VIZURI MTUMA POSTI HAPO JUU,,,,
 
Kwenye sakata la MCC, hakuna nchi ya nje iliyotufanyia au inayotaka kutufanyia maamuzi. Aidha hatukua na mpango wa kuzikosa pesa hizo. Tumestukizwa. Wala hazihusiani na misimamo mikuu ya kisera ya taifa tunayosimamia kama ilivyokuwa tulipovunja uhusiano na FRG, Israel na Uingereza kipindi cha vita baridi.

Zaidi, pesa za MCC si chambo zaidi ya misaada mingine toka USA na nchi nyingine tunayopania kuipokea na kuingiza kwenye bajeti ya taifa. Kisha tunatumia ovyo baadhi yake. Tukitaka kuepuka "vyambo" vya aina hii basi tuwe makini na mikakati yetu ya kiuchumi na hasa kutumia rasilimali zetu na pesa toka nje kwa umakini mkubwa unatuongezea uwezo zaidi wa kujitegemea. Halafu kuhusisha mjadala wa kujitegemea na suala la MCC is nothing short of mipasho. Hilo ni jambo kubwa sana linalohitaji nafasi ya kipekee.

Ni rahisi sana kwa mtu mwenye "elimu" kujenga hoja ku-justify chochote. Kuna wakati niliongea na balozi mmoja wa Ujerumani akaniambia watu wasiojua wanafikiri Hitler alikuwa mwehu. Kiukweli alikuwa na timu kabambe ya wataalamu waliojenga hoja nzito kuhusu falsafa zake na kuwashawishi wengi kukubaliana nazo. Hadi leo wapo wanazuoni na watetezi wa falsafa hizo za kifashisti. Kama hukujiandaa kwa mjadala, wanakupiga knock out.

Ndio maana kuna usemi wa kiingereza kuwa "talk is cheap".
 
wana macho lakini hawaoni,wanaujua ukweli lakini wanataka kutimiza tija zao za kisiasa.

Marekani ina miradi ya afya zaidi
50 kwa nchi hii inayogharamiwa
kwa "mabilioni ya fedha".
Mashirika ya Marekani yanayo-
operate hapa nchini kusaidia
huduma za afya ni zaidi ya 20
yakijikita zaidi maeneo ya vijijini.
Ukweli ni kuwa Marekani ni uti wa
mgongo wa afya ya watanzania.
Miradi mikubwa ya mabilioni ya
dola kusaidia afya ya watanzania
inafadhiliwa nao. Miradi ya
UKIMWI, Malaria, Kansa ya Shingo
ya Kizazi, Kansa ya matiti, TB na
magonjwa mengine hatarishi.
Wanatoa huduma hizi bure kabisa.
Kuna watu wangekuwa
wamepoteza maisha kama sio
huduma hizi zinazofadhiliwa na
Marekani, lakini leo wana
matumaini ya kuishi.
Wamesaidiwa na hao mnaosema
"waondoke na misaada yao".
Nakumbuka kisa kimoja wilayani
Makete nilipoenda mwaka 2014.
Mzee mmoja alituhadithia kuhusu
maisha yake na changamoto
alizopitia kutokana janga la
UKIMWI kuvamia familia yake
miaka kadhaa iliyopita. Anasema
alipoteza familia yake yote kwa
UKIMWI akabaki yeye na mjukuu
wake mmoja.
Akakata tamaa na kupoteza
matumaini ya kuishi. Akajiandaa
kufa. Akawa anaomba afe yeye
kwanza kabla ya mjukuu wake
maana hataweza kuishi ikiwa
mjukuu wake atatangulia maana
ndiye aliyekua anamhudumia,
kumuogesha, kumpikia etc.
Kajukuu ka miaka 8 kamebeba
majukumu ya baba wa familia..
kanamtunza babu yake. Kana
vidonda mdomoni na miguuni,
afya yake haikua nzuri sana. Babu
yake ndio alikonda hadi akatisha.
Nywele zikanyonyoka..
Mwaka 2002 zikaja dawa za
kupunguza makali ya virusi vya
UKIMWI (ARVs) lakini zikawa
zinauzwa bei ghali sana.. Babu
akauza shamba lake la miti ili
kupata matibabu yeye na mjukuu
wake.. akaanza kutumia dawa na
afya yake ikaanza kuboreka..
lakini fedha zilipoisha akarudi
kwenye mateso ya awali..
Miaka kadhaa baadae huduma za
ARVs zikaanza kutolewa bila
malipo kipaumbele kikiwa kwa
waathirika wenye CD4 chini ya
250. Akawa enrolled kwenye
huduma ya CTC ya kupokea ARVs
bure yeye na mjukuu wake kupitia
mradi mmoja wa "Care &
Treatment" wa shirika fulani la hao
Wamarekani ambalo sitalitaja jina.
Leo miaka zaidi 10 babu yuko
"well & good" na ukikutana nae
wala huwezi kugundua kama ana
maambukizi. Utaona amedhoofu
kdg lakini utajua ni uzee tu wa
kawaida.
Tulipoenda kwake kwa ajili ya
kuandika "success story" ilikua
ngumu kuamini kama ana
maambukizi maana alikua na afya
nzuri sana. Mjukuu wake by then
alikua chuo cha Ualimu.. bila
shaka saivi ni mwalimu
somewhere na atakua anamtunza
babu yake.
Hivi familia kama hii unaielezaje
kuhusu kufutwa kwa misaada ya
Wamarekani?. Walikiona kifo lakini
wameponea kwenye tundu la
sindano kwa msaada wa watu wa
Marekani.
Leo unawaambia eti hawatapata
tena huduma ya ARVs kwa sababu
Kuna mtu Zanzibar anang'ang'ania
madaraka. Seriously? Kwamba
Urais wa Zanzibar ni muhimu
kuliko uhai wao?
Yani turuhusu watu wafe kwa
kukosa dawa kwa sababu ya Urais
wa Zanzibar? Huyo Rais
atamuongoza nani kama
ataruhusu watu wake wafe kwa
UKIMWI?
Tunaposema Marekani wachukue
misaada yao tunaweza
kujitegemea je tumetengeneza
"alternative" ipi ili wagonjwa
waliokuwa wakipata huduma kwa
msaada wa Marekani wasiathirike?
Nje ya miradi ya UKIMWI kuna
miradi mingine mingi ya afya
inayofadhiliwa na serikali ya
Marekani nchini. (Sitaki
kuzungumzia miradi ya maendeleo
kama umeme, maji na kilimo). Leo
niongelee miradi ya afya tu.
Akina mama maskini wa Peramiho,
Newala, Maswa, Biharamulo,
Kaliua, Nkasi etc wanapewa
huduma ya uchunguzi bure wa
kansa ya shingo ya kizazi na
kansa ya matiti na wakikutwa na
dalili wanagharamiwa matibabu
bure.
Wengine unakuta wameugua hadi
wamepoteza matumaini ya kuishi
lakini kupitia miradi hii wamepata
tena nuru ya uhai.
Lakini kwa kukosa busara
tuwanaropoka tu kuwa eti
"Marekani waondoe misaada
yao..".. Hivi wakati unasema hivyo
umefikiria ni watanzania wangapi
wenye virusi vya UKIMWI
wataathirika? Umejiuliza ni
watanzania wangapi wenye TB
watathirika? Leo inatangazwa
vipimo vya TB ni bure tunafurahia
bila kujua ni mkono wa Marekani.
Umejiuliza ni akina mama wangapi
watakaokufa kwa kansa ya shingo
ya kizazi au kansa ya matiti wakati
wangepata msaada wa matibabu
bure kupitia miradi hii
inayofadhiliwa na Marekani?
Hivi unafikiria yote hayo au
unajifikiria wewe tu?? Kwamba
hata misaada ikikatishwa wewe
hutaathirika utaendelea na maisha
yako kama kawaida kwa hiyo
hujali kitu. Huu ni ubinafsi mbaya
sana..
Siungi mkono kuwa ombaomba na
kutegemea wahisani kwenye kila
kitu lakini nasisitiza ni vizuri
tukajipanga kwanza. Mnaposema
waondoe misaada yao jiulize je
tumejipanga.
Wamarekani wakiondka leo ndugu
zetu wa Makete wataendelea
kupata huduma za ARVs kama
zamani? Ndugu zetu wa
Shinyanga watapata msaada wa
matibabu ya TB bure kama ilivyo
sasa? Mama zetu wa Nkasi
watapata huduma ya uchunguzi
wa saratani ya shingo ya kizazi na
kupewa matibabu bure?
Serikali yetu imejipanga
kucompasate hilo gap? Yani
wamarekani wakiondoka sasa hivi
tunaweza "kutake lead" kwenye
hizo huduma za kusaidia
watanzania wenzetu kama hata
"panadol" serikali inashindwa
kununua?
Bado nasisitiza tunahitaji muda
wa kujipanga.. kufanya maamuzi
bila kujipanga ni kujitafutia
madhara makubwa zaidi.
Tuache kujadili suala hili kwa
ubinafsi na itikadi za vyama..
tujadili kwa maslahi mapana ya
kitaifa.. je tuko tayari kusimama
peke yetu kwa sasa?
Na kama tuko tayari kwanini
hatukuomba kusimama peke yetu
hadi tumenyimwa msaada ndio
tunajitapa kuwa tupo tayari?
Kuna tofauti kubwa kati ya ndoa
ya kulazimishwa na ndoa ya
kuridhia mwenyewe japo zote ni
ndoa. Ukimpa binti mimba
ukalazimishwa umuoe ni NDOA.
Ukimpenda binti ukamtolea mahari
ukamuoa ni NDOA.
Lakini kati ya hizi ndoa mbili kuna
moja haina "sustainability".. Muda
wowote inavunjika..maana
hawakupendana ila wamejikuta
wamelazimika kuishi pamoja.
Hawakujiandaa.
Na sisi ndivyo tunavyotaka
kufanya. Tunataka kujilazimisha
kuwa tunaweza kusimama
wenyewe wakati si kweli.
Tujipe muda tujipange vizuri,
tuweke mikakati madhubuti ya
kujitegemea kisha sisi ndio
tukatae hiyo misaada yao sio
tusubiri watunyime.
Inawezekana. Tunaweza kuwa na
"strategic plan" ya miaka mitano
au kumi, tukahakikisha kila njia
kuu ya uzalishaji inakua "utilized
to the maximum" na kuleta
manufaa kwa nchi.
Kama ni bandari tunahakikisha
nchi zote za Afrika ya kati
zinatumia bandari yetu.. huduma
zinakuwa bora na za ufanisi
tunapata mapato makubwa.
Kama ni utalii tunaweka mikakati
mizuri ya kufanya "marketing" ya
vivutio vyetu na kuhakikisha
tunapata watalii wengi na mapato
mengi yatokanayo na sekta ya
utalii kuliko nchi zote za Afrika
Mashariki na kati.
Kama ni viwanda tunaanzisha
viwanda vya uzalishaji kwa
malighafi zinazopatikana nchini
kisha tunauza "finished goods" au
"semi processed goods" na sio
kuuza "raw materials" kama ilivyo
sasa. Hii itasaidia nchi kupata
mapato makubwa.
Kama ni kilimo tunahakikisha
tunafanya kilimo chenye tija
tunapata chakula cha kutosha na
tunawauzia nchi jirani.. Tunapata
pesa nyingi.
Hatimaye unakuta kila sekta ya
uchumi nchini inazalisha "to the
maximum".
Yani kama bajeti yetu kwa mwaka
ni Trilioni 30 sisi tuwe tunazalisha
Trilioni 100 (reserve ya trilioni 70)
. Hapa sasa tunaweza kuwa na
kiburi cha kukataa misaada ya
wahisani.
Na hatutasubiri watunyime.. Sisi
wenyewe tutawaambia "asanteni
kwa kuja".. tunawashukuru kwa
msaada wao kisha tunawaomba
wakasaidie watu wengine maana
sisi tumeshajiweza kiuchumi.
Haya ni mambo ambayo
yanawezekana ndani ya miaka
michache kana tukijipanga vzr na
tukawa serious. Tunazo rasilimali
za kutosha kufanya hivyo;
Muhimu ni kujipanga na kuweka
mikakati mizuri.
Lakini kukurupuka sasa hivi na
kudai tunaweza kujitegemea
wakati hatujajipanga ni ujinga
mkubwa mno. Unawezaje
kujitegemea wakati hata
"paracetamol" unapewa msaada?
Tuache mihemko ya kisiasa na
tujadili suala hili kwa maslahi
mapana ya kitaifa.. je kweli
tunaweza kusimama wenyewe?
Tunawezaje kusimama wenyewe
wakati tupata asilimia 04% kwenye
madini na wawekezaji wanachukua
asilimia 96%?? Tunawezaje
kusimama wenyewe wakati
uchumi wetu ni "import &Export
oriented"? Yani tunanunua zaidi
nje kuliko tunavyouza hali
inayosababisha shilingi yetu
kuporomoka kila siku!
Tunawezaje kusimama wenyewe
wakati Kenya wanafaidi mlima
Kilimanjaro mara mbili kuliko sisi
wakati mlima uko kwetu?
Tnawezaje kusimama wenyewe
wakati bado mkulima anategmea
jembe la mkono na hata akilima
hana uhakika wa soko?
Nadhani tuweke mihemko ya
kisiasa pembeni. Tujadili suala hili
la ufadhili wa Wahisani kwa
maslahi mapana ya kitaifa.
Tukifanya hivyo tutakubaliana
wote kwamba BADO TUNAHITAJI
MUDA ili kuweza kusimama
wenyewe.
Kama ni mimba hii ya kwetu ina
miezi mitano tu.. kwa hiyo
tukilazimisha kuzaa tutaua mama
na mtoto.. bora tusubiri angalau
ifikishe miezi 7 tunaweza kupata
walau mtoto ambaye ni
"premature"
Naipenda Tanzania. Napenda
kuona ikijitegemea na kuondoka
kwenye misaada ya wahisani
lakini nasisitiza BADO TUNAHITAJI
MUDA WA KUJIPANGA. MUNGU
ibariki Tanzania yangu na watu
wake.!
 
Pole pole katika ubora wake ccm ina wapambe kinoma kama huyu jamaa simpendi ni mnafki sana huyu pole pole
 
Back
Top Bottom