Mtazamo wa watu zamani kwa mwanaume na mwanamke hata kiroho

Mtazamo wa watu zamani kwa mwanaume na mwanamke hata kiroho

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
16
Wakati wa sasa ni watu wengi sana wanafahamu habari ya maandiko kutoka kwenye vitabu vya dini. Jamii ya kiswahili inafahamu uwepo wa dini nyingi na hasa dini mbili uislamu na ukristo.

Watu wa zamani pamoja na mambo yote walielewa uwepo wa nguvu za aina mbili katika uwepo, yaani uwepo wa nguvu changa au nguvu za juu na uwepo wa nguvu hasi au nguvu za chini.

Zaidi watu wa zamani walielewa kuwa nguvu zote hizi zipo chini ya chanzo kimoja kikuu.
Pia walielewa kuwa nguvu hasi au nguvu zote sio nguvu ambazo moja kwa moja ni ovu bali asili yake ni nguvu hasi ivyo ivyo.

Wakiangalia katika uwili uhusiano wa sehemu mbili ndio hutengeneza ukamilifu na uthabiti wa kitu.
Hata katika maisha bayana nishati ya umeme inahitaji uwili yaani chanya na hasi ndio iwe nishati ya umeme.
Basi nguvu hasi za kiroho ni muhimu katika uwepo, japo kuwa watu wengi huchanganya habari ya uovu wa nishati za kiroho na nishati hasi, ni bayana kuna utofauti mkubwa sana kati ya nishati za kiroho ovu na nishati za kiroho hasi.

Nishati ovu ni nishati zinaweza kuwa chanya au hasi. Nishati ya kiroho hasi ikiwa ovu inakuwa nishati ovu na vile vile nishati chanya ikiwa ovu inakuwa nishati ovu.

Nishati chanya ikiwa ovu haiwezi kuwa nishati chanya tena inakuwa nishati ovu.
Nishati hasi ikiwa ovu haiwezi kuwa nishati hasi tena inakuwa nishati ovu.

Watu wengi huchanganya nishati ovu na nishati hasi za chini, bila kufahamu kuwa sio kila nishati hasi ni ovu wala haina maana kuwa nishati chanya hazi asi, nishati chanya pia zina asi japo kwa mujibu wa watu wa zamani ni mara chache sana nishati hizi ku asi, ila nishati hasi nyingi zina asi na kuwa ovu.

Hata katika maandiko ya vitabu vya dini utakuna na habari ya viumbe wa kiroho ambapo utasoma na kuelewa hata kiumbe maarufu muovu wa kiroho shetani inadaiwa kwenye kumbukumbu za vitabu vya dini alikuwa malaika.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kuna mitazamo mingi kuhusu dini mbili maarufu katika jamii ya kiswahili.
Mtazamo maarufu ukisema dini ya uislamu ni sehemu ya dini ya ukristo.
Mtazamo mwingine ukisema ni dini tofauti ambazo msimamizi wake hapa duniani ni mmoja.

Lakini hoja ya wazi dini zote mbili zinataja chanzo kimoja kikuu cha uwepo.

Wasomi wa dini wengine wakidai kuwa mafundisho ya dini ya ukristo yana jumuisha habari ya nguvu chanya na nguvu hasi za kiroho, na mafundisho yale ya kiislamu yamezama zaidi kwenye nguvu hasi peke yake chini ya mamlaka kuu ya uwepo.

Na pia imekuwepo sintofahamu kati ya wafuasi wa dini hizi mbili, wafuasi wa dini ya ukristo baadhi wasio fahamu wanadai kuwa wafuasi wa dini ya uislamu ni kusoma habari ya roho waovu, mtazamo huu unakuwa tofauti na uhalisia wa imani ya wafuasi wa dini ya uislamu kwa kiwango kikubwa.

Huku wafuasi wa dini ya kiislamu wakiendelea kukiri kwamba katika nguvu hasi kuna nguvu za kiroho zile ovu laikini zipo nguvu hasi ambazo ni njema.

Vilevile wafuasi wa dini ya kiislamu wale wasio fahamu wamekuwa na mtazamo mgando juu ya sheria za uwepo zilizo shuhudiwa na wasomi wa maarifa ya kiroho wa kale, wale wasomi wa kabla ya mikusanyiko na maandiko ya jumuishi ya vitabu vya dini.

Mtazamo mgando huo kwa baadhi ya wafuasi wa dini ya kiislamu wanaamini viumbe wote wa kiroho ni roho hasi, na hawa hawataki wala hawana muda wa kuelewa habari ya uwepo wa nishati za viumbe wengine wa kiroho mtazamo ambao sio sahihi kwa kiwango flani.

Pamoja na habari zote zilizo andikwa ndani ya maandiko ya kiroho ya vitabu vya dini, kuna habari ambayo imekuwa ikichanganya fahamu za baadhi ya wasomi wa vitabu vya dini na hata wasomi wa mambo ya kijamii.


Habari yenyewe ni kipaumbele cha mwanaume na mwanamke.
Maandiko ya dini ya Kiislamu imetaja habari ya wanaume peke yake.
Hata maandiko ya dini ya kikristo imeweka bayana zaidi habari ya mwanaume zaidi kuliko mwanamke.

Lakini bila kusahau habari ya jamii za zamani za kale jinsi na namna walivyo weka vipaumbele vya mwanaume na mwanamke.

Ni mifumo ya kidunia pekee ndio inafanya kampeni kinyume au tofauti na habari ya uislamu, ukristo na jamii ya watu wa kale.

Hata hivyo ufahamu wa kiroho umeweka bayana habari hii bila kupindisha kuwa mwanamke ni sehemu ya mwanaume.

Ni sehemu ya mwanaume kwa maana ya mfano wa mguu ni sehemu ya mwili.

Basi unaweza kutafakari mambo mengi kutokana na ufahamu wa kiroho kuwa mwanamke ni sehemu ya mwanaume.

ni maumivu makali sana anapata mtu yule anaye jaribu kuumiza sehemu yake yeye mwenyewe. Mfano kinatokea nini pale mtu anapo umiza kidole cha mguu wake.

Hiyo ndio maana ya kusema kitu ni sehemu ya kitu.

Lakini kitatokea nini pale mtu ataamua kukata mguu wake mwenyewe, bila shaka mtu huyo anayekata mguu wake atapata maumivu makali yatakayo koma baada ya muda, ila sasa mtu huyo atabaki akiwa hana mguu.

Na itakuwaje kwa mguu unao tolewa kwenye sehemu yake, mguu huo baada ya kutolewa sehemu yake , wenyewe haujui chochote kuwa mtu huyo atabaki bila mguu au mtu huyo anapata maumivu, na wala mguu huo hauna uzima tena na badala yake unaweza hata kuoza.

Kama ilivyo kwa kiungo kingine cha mtu kinaweza kutolewa kwa mtu huyu kikapandikizwa kwa mtu yule na pindi kinapo jishikiza kikamilifu kiungo hicho huendelea na maisha yake kama kawaida na inakuwa kama ndio asili yake mahali hapo kilipo pandikizwa.

Kwa kuangalia habari ya kiungo ambacho ni sehemu ya mwili, ndilo hilo ufahamu wa kiroho wa watu wa kale unajaribu kutueleza kuhusu mwanamke.

Mwanamke anaweza kuishi na mwanaume anaye mfanya ajiskie vizuri akawa na furaha na akaweka kiapo cha kuto kuachana naye daima.

Ila ikitokea ametenganishwa na mwanaume huyo na kwenda mahali pengine kwa mwanaume mwingine huko nako akifanyiwa wema wa aina nyingine, wema huo umfanye ajiskie vizuri ataanza kufurahi na kujiachia kama awali.

Mwanamke huyo anaweza kuulizwa kati ya hapa na kule unapenda wapi akakosa majibu sahihi ya haraka.

Watu wanaweza kulaumu kusema hivi ama vile juu ya huyo mwanamke lakini ufahamu wa kiroho wa watu wa zamani unatueleza kuwa hiyo ndio asili ya mwanamke yeye ni sehemu ya mwanaume.

Kama ilivyo mguu ukipigiza unaumia wewe.
Huo mguu ukiupendezesha una kuwa unavutia.

Mguu huo ambao ni sehemu yako ukiuboresha una kuwa bora zaidi na mguu ukiwa bora una kuwa bora zaidi na mguu ukiwa bora una kupa safari njema ya kutembea.

Mguu mbovu kwa uzembe wako utakufanya ushindwe kutembea.
Sehemu ya mwili ya kidole cha mkono ikiwa na dosari basi mtu atashindwa kufanya jambo kwa mkono ule kwa ukamilifu inakuwaje mtu asipo kuwa na sehemu yake moja, ndio hivyo mtu anakuwa asipo kuwa na sehemu yake.

Ufahamu wa kiroho unatueleza kuwa katika uwili uhusiano mzuri na imara wa sehemu mbili ndio unaleta ukamilifu.

Uhusiano huo unakuwa na nguvu ikiwa kila sehemu inafanya majukumu yake, kama vile sehemu ya matawi ya mti haiwezi kuwa na uzima bila mizizi na mizizi itakuwa kwa ajili ya nini kama sio matawi.

Ufahamu wa kiroho wa watu wa zamani unatufundisha kwamba kuna nguvu ya kiume na nguvu ya kike, mafundisho ya watu wa kale yanaleta ushahidi wa uwepo wa kiumbe mtu wa kiume na wakike, elimu hii inaenda mbali na kusema nguvu ya kike ni sehemu ya nguvu ya kiume.

Elimu na maarifa ya kale yana aandika sifa za nguvu ya kiume na sifa ya nguvu ya kike, lakini pamoja na sifa zote sifa moja ni nguvu ya kike asili yake ni kuzunguka nguvu ya kiume daima daima.

Pia inaeleza kuwa nguvu ya kiume ni nguvu ya nje na nguvu ya ndani ni nguvu ya kike, vilevile nguvu ya kiume ni nguvu ya utendaji.

Hivyo basi unapo zungumzia mwanaume na mwanamke unakuwa unazungumzia nguvu ya kiume na nguvu ya kike katika maumbo ya kimwili ambazo ni uwili, na ukamilifu ni matokeo ya mahusiano mazuri ya sehemu mbili za uwili huo.

Mtu wa sasa ni muhimu kuelewa habari ya uwili na kusimama katika majukumu yake kila mmoja.

Mwanaume anapaswa kutambua kuwa mwanamke ni sehemu yake ambayo hawezi kuinyanyasa wala kuiumiza na wakati huo mwanamke anatakiwa kuelewa yakuwa yeye ni sehemu ya mwanaume.

Mwanaume aishi akijali sehemu zake na majukumu yake kwa sehemu zake.
Mwanamke aishi akijua yeye ni sehemu ya mwanaume.

Mdomo unaweza kusema nini kama mwenye mdomo haja aamua kusema.

Mdomo unaweza kusema nini ikiwa hauwezi kusema, hata mwenye mdomo akitaka kusema.

Uwili ni kanuni na sheria ya kiroho ambayo inafanya umilele wa ukamilifu.
Sheria hii inavunjwa ama kwa kujua, ama kwa kuto kujua ni lazima mambo yasiyo ya kawaida yataendelea kwa kuwa namna na jinsi ya kawaida imetoweka.

Matatizo mengi ni matokeo ya kutokuwepo kwa mpangilio wa kawaida kwa namna nyingi hata kwa mitazamo.

Katika suala la mwanaume na mwanamke ni bayana kwamba mwanamke anapenda kujiskia vizuri bila kujali kujiskia vizuri kuna tokana na nini, kitu ambacho kwa mwanaume sio cha moja kwa moja, mwanaume mara nyingi hutaka kuelewa kila jambo.

Mwanaume asijaribu kuinyanyasa sehemu yake mwenyewe maana ataumia na atashindwa kutenda, mwanaume atambue majukumu asije kutolewa na kutolewa anaweza kuoza asipo pata sehemu nyingine kama mguu kiungo au sehemu ya mwili inavyo kufa ikiko
sa mwili mwingine inapoweza kukaa.

Vilevile sehemu ya mwili inaweza kupata ajali bila mwenye mwili kutegemea.
 
Back
Top Bottom