KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za muda huu waungwana.
Mapenzi ni maisha na mapenzi ni sehemu kubwa ya maisha. Ni vigumu kuyaweka kando mapenzi kwani hata ukifanya hivyo moyo utakuamulia, hivyo basi hatuwezi kuyacha kuyajadili kwa mazuri na mabaya yake.
Nyakati za hivi karibuni kumeshamiri wimbi la hali ya uongo, usaliti, wizi, na ukatili kwenye ndoa. Wingi wa visa hivyo kumepelekea taasisi ya ndoa kupoteza maana mpaka mtu ukiamua kuoa watu wanakushangaa na kukuonea huruma kana kwamba unafanya jambo la kishetani.
Hasa nikiangazia upande wa wanawake walio kwenye ndoa unakutana na matukio ya usaliti wa kupindukia, unakutana na matukio ya wanawake kuwaibia waume zao au kufanya mambo yao kwa siri pasi na mume kujua kuamua kuachana na mumewe pindi tu anapopata uwezo wa kiuchumi na kuweza kujitegemea.
Vipo vilio vya wanaume wengi waliojaribu kwa namna moja au nyingine kuwainua wanawake zao kiuchumi kwa nia njema kabisa lakini matokeo yake yamekuwa machungu.
Wingi wa mtiririko wa matukio haya ya wanawake kukithiri kwa vilio hivi kwa wanaume kuongezeka kwa taraka na kukimbiana baada ya mke kujiona kuwa anaweza kujimudu yote inadhihirisha ukweli kuwa wanawake walio wengi wapo kwenye ndoa au mahusiano kwa sababu za kiuchumi zaidi kuliko mapenzi.
Kuna uwezekano mkubwa huyo unayemuita mkeo au mpenzi wako yupo na wewe kwa kuwa kwa muda huu ni wewe pekee unayeweza kusimamia vyema matatizo yake ya kiuchumi. Nguzo ya upendo haipo moyoni mwake.
Hatukatai kwamba mwanaume lazima utoe huduma kwa mkeo lakini kwanza yatangulie mapenzi kwani kwenye maisha kuna nyakati nyingi hasa si uungwana kuwa na mtu ndoani kwa sababu fulani kwani inawezekana sababu hiyo siku moja ikaondoka.
Ingawa hali ni ngumu na ni vigumu kutambua maana waigizaji ni wengi sana wanapoona kuwa kuna uwezekano wa kupata chochote kitu kwenye muunganiko huo tusijisahau wanaume wenzangu. Lazima ufanye jitihada za kumjua mwenzako ni mtu wa namna gani ili ujiandae kisaikolojia kukabiliana na unalolijua.
Word is enough for the wise.