Mtazamo wangu: Huenda Yanga SC ikajihakikishia rasmi Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa Matokeo ya Mnyama na Coastal Union Leo au Police Tanzania Jumapili

Mtazamo wangu: Huenda Yanga SC ikajihakikishia rasmi Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa Matokeo ya Mnyama na Coastal Union Leo au Police Tanzania Jumapili

Kwa timu iliyokosa furaha kwa misimu minne sioni ajabu mwaka huu wakichukua wao..as long mnyama malengo yake kimataifa yako vizuri! Na kwa akili tu ya kawaida usimba na uyanga unanoga ikiwa timu zote zinafanya vizuri! Sasa fikiria timu moja hiyohiyo kila mwaka inachukua yenyewe tu kombe..
Na ndio maana hata hizi kelele za kuipamba yanga za waandishi wa habari sio za bahati mbaya..ni kuhakikisha wanairudisha yanga kwenye ramani..hata simba wanalijua hili,na huwezi amini hata Manara kwenda yanga ni katika kukamilisha huo mkakati ngalau yanga nao wawe na furaha..Simba haikufika pale bahati mbaya iliwachukua miaka mingi sana ya machozi na damu.
Umebarikiwa kipaji cha uongo, propaganda na upotoshaji.
 
Mechi 11 bado.Dalili kwa yanga kuwa bingwa zinaonekana kwa jinsi mazingira yalivyo tengenezwa nje na ndani ya uwanja
 
Wanazidi kurahisisha kazi, wamejitahidi kukimbiza mwenge lakini naona wanaanza kusanda wao wenyewe, uwezi kukimbia mwendo mrefu wakati umejaza wazee wa pensheni kwenye timu na ndio unaowategemea wakupe matokeo mwisho wa siku pumzi inakata kama ivyo
 
Kwa Matokeo ya Chamazi Complex Jana Usiku, kwa Presha Kubwa iliyoko sasa, kwa Ratiba ngumu ya Ligi Kuu na ile ya ASFC, kwa Rotation ya Wachezaji ili Kukwepa injuries na kwa Mawazo pamoja na Maandalizi ya Mechi na Waafrika Kusini katika Robo Fainali ya CAF Kiufundi GENTAMYCINE naona kuna Uwezekano mkubwa wa Kuangusha Alama Muhimu ama na Coastal Union FC leo au na Police Tanzania Jumapili hali ambayo itawahakikishia rasmi Ubingwa Wapinzani kwani tayari watakuwa wameshajikusanyia Alama ( Points ) nyingi za kuwapa Jeuri hiyo.

Nasisitiza huu ni Mtizamo wangu wa Kiufundi Mimi GENTAMYCINE na sijakulazimisha Uuamini au Uuchukue bali naomba / nakuomba tu Uuheshimu na kama hiki nilichokiandika Kitakukwaza ( Kitakukera ) nakusihi Vumilia tu kwani wengine tumebarikiwa kuwa Wakweli, Waona Mbali na hatujawahi ama Kuhisi Kitu au Kutabiri Jambo halafu kwa 75% hadi 99.999% kisiwe / lisiwe Kweli.

Na kama labda utakuwa na Hasira ( Jazba ) mno na GENTAMYCINE kwa huu Mtazamo wangu wa Kiufundi kutokana na Mapenzi ( Mahaba ) niue yako kwa Klabu yako pendwa nakuomba Kwanza anza Kuwakasirikia Viongozi wako ( hasa Mwekezaji wako ) ambaye alisitisha ( aligoma ) kutoa Posho kwa Wachezaji na CEO wenu nae akawacheleweshea Mishahara Wachezaji wenu hali iliyopelekea Wachezaji kushuka Morali na hatimaye Kuharibu Mechi ya Mbeya na Mbeya City FC na ile ya Kagera na Kagera Sugar FC.

Niwatakieni tu Karume Day njema Leo.
kumbe ulijua kutabiri kabisaa kolo genta
 
Back
Top Bottom