Mtazamo wangu kuelekea Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika

Mtazamo wangu kuelekea Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika

Kwanza niseme wazi kuwa mimi ni mshabiki wa Simba sports club lakini uchambuzi wangu utazungumzia uzoefu mdogo nilionao kuhusu soka la Africa.

1.Kwa asilimia 100% nina uhakika Simba Sports Club ataenda Robo fainali hata kama wakibaki na hizo point 10 hio inamaanisha viongozi ni heli wakafikiria kuongoza kundi ili Kuipandisha hadhi team yetu.

2.Tukifika robo fainali nina uhakika mashabiki wa Simba hatutafurahishwa na kama ikitokea tukatolewa lakini nina uhakika pia tutajivunia team yetu kwa hatua ambayo tutakua tumefikia.

3.Team za Africa viwango vyao karibia vyote vinafanana na ndio maana ni mara chache sana kupata matokeo ya team kupigwa goli kuanzia mbili na kuendelea watu tunaobeti nafikiri hapa mnanielewa.

3.Kuna Wydad, Esperance na Mamelod ambao watu wengi wanaona kama ni tishio kitu ambacho niukweli ila ukiwa upande wa hizo team nina uhakika kwao team tishio na hawataki kukutana nayo ni Al Ahly na Simba Sport club kiasi ambacho hawaoni nani ana nafuu kati ya simba na Al Ahly ili waombee nan angoze au awe wa pili kwenye kundi lake.

4.Uwanja wa mkapa zamani nilikua naona kama ni rahisi kuondoka na matokeo ila saiz nmeanza kuelewa ni ngumu kuondoka na alama pale kwa team za nje hata kama zitakutana na Yanga achilia mbali Simba.

5.Simba wako vizuri kwenye defense haswa, Akiwapo onyango, wawa, mzamiru, Lwanga, Manula hua nawaza forward line ya team pinzan inapataje goli yaan wapite wote hao defensive men na ukamfunge Air manula ni kazi ya nguvu na mbinu inatakiwa kuganywa na team pinzani ili hilo litokee

6. Simba na Al Ahly ndio team pekee kati ya 16 zilizopo group stage ambazo zinaweza kua na uhakika wa ku posses mpira kama wakiamua,,,na hata wakiamua kua na approach tofauti hizi team zinamudu...imagine kwenye uwanja wa As Vita...Simba hakutaka kufunguka na alienda na approach ya kudefense na kuacha mpinzan akushambulie lakini As Vita alikua na shots on Target mbili pekee.

7.Simba tatizo ni Finishing na kama tukitaka kutibu tumuombe Gomes Da Rosa amuamini Kagere kwan uwezo wake upo juu sana ukimfananisha na mugalu ambae hawezi kulingana hata na John Boko.

8.Kama Tshabalala , Wawa, Onyango, Lwanga, Mkude, Morrison, Kapombe, Manula, Chama, Luis, kahata, Bwalya, Kagere, Mkude wakiwa fiti, Au wasiwe na corona hakuna team Africa ambayo itakua tishio moja kwa moja kwa Simba au hakuna team ambayo haitaheshimu uwezo wa Simba pale zitapokutana.

9. Team ya Simba ni miongoni mwa team yenye depth kubwa kwa maana ya kwamba wachezaji wanaoanza, waliopo bench na hata wanaobaki reserves wana ubora mkubwa

10. Hii imekaa kiushabiki na sio kiuchambuzi, Simba kama ukitaka kuingalia usiiione kama kanyau ni kudude gukubwa gunakotisha sana, ni kama zile ndoto za kuweweseka kwa team pinzani ila za heri kwa wanasimba
Nimebahatika kuangalia timu nyingine zinazo cheza nimetambua simba ni tishio washabiki wengi wa first runners kweli wanaziogopa timu za group a hawapendi wakutane nazo ila hamna jinsi lazima kiumane
 
Sorry hiyo comment nili edit.

Bandiko lako limejaa mahaba,hisia na dhahania kuliko uhalisia.

Football haiko hivyo ndugu...Al ahly huwa hapati matokeo Congo...lakini msimu Vita kapigwa 3-0 wakati Egypt alipata sare....record zipo ili kuvunjwa ndugu...na huwezi jua ni lini zinavunjwa kuweka asilimia mia kwenye michezo ambayo haijakamilika thats not football..mpira mchezo wa suprise...Manchester alishindwa kupata point moja tu kwa Leipzig leo hii anacheza Europa,Simba ni nani?

Halafu tena una claim kuwa Simba na Al ahly pekee ndo wanaweza possess mpira kwenye timu 16. Kitu kinachoonyesha mpira wenyewe labda unaangalia mechi za Simba tu...ushawahi take your time kuwaangalia hata Mamelody?
Haha hao jamaa ni balaa...

Kuna game moja waliwafunga Ile timu wapo nayo kundi moja ya waarabu inaitwa CR beloughzidad sijui huko😄 ...jamaa walipigiwa pasi 43 ndo wakafungwa goli ....
Nasio kwamba hao waarabu ni wakisport sport ila ndo Ivo...

Hao mamelody ni balaa 🙌
 
Group A lina team ngumu mno saiz ni bora Al Ahly watoke tu robo fainali
Nimebahatika kuangalia timu nyingine zinazo cheza nimetambua simba ni tishio washabiki wengi wa first runners kweli wanaziogopa timu za group a hawapendi wakutane nazo ila hamna jinsi lazima kiumane
 
Ile game ilichezwa kwa mkapa saa 10 sio game uwanja mzuri kwa waarabu sijui hata belouizdad waliwaza nin kuomba kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani
Haha hao jamaa ni balaa...

Kuna game moja waliwafunga Ile timu wapo nayo kundi moja ya waarabu inaitwa CR beloughzidad sijui huko[emoji1] ...jamaa walipigiwa pasi 43 ndo wakafungwa goli ....
Nasio kwamba hao waarabu ni wakisport sport ila ndo Ivo...

Hao mamelody ni balaa [emoji119]
 
Siyo tu huna uzoefu na mpira wa Africa bali huna uzoefu na mpira wenyewe kabisa,nilipoona tu umeandika una asilimia 100 Simba kufika robo fainali nikajua kweli huna uzoefu,100%? kweli? kwenye mpira?

Simba na Al ahly ndo pekee wenye uwezo wa ku possess mpira kwenye timu zilizo kwenye 16 kweli? huijui hata Mamelody? I guess unaisikia tu.

Kifupi bandiko lako limejaa Mahaba hisia na dhahania kuliko uhalisia.
Yeye na wewe ni nani ambae hana uzoefu au hajui Moira wa Africa ? Manake kujua mpira wa Africa ni pamoja na kujua Simba hafungwi nyumbani
 
Ni vyema ukaishauri timu yako kuendelea kucheza kwa bidii ili waongoze kundi lao A na hivyo kuepukana kukutana na waongozaji MAKATILI wa makundi mengine kama Mamelod Sundowns, Esperance na Wydad Casablanca!
Hao wapuuzi wanakupiga kokote! Iwe nyumbani au ugenini!

Na kuhusu Mugalu vs Kagere, huenda kocha wenu ana sababu za msingi. Kagere ni finisher mzuri, lakini siyo mpambanaji uwanjani kama huyo Cris Mugalu! Mugalu anakaba sana timu ikishambuliwa kuliko Kagere!

Hivyo kwa kiasi fulani, mwalimu wenu yuko sahihi. Ingawa huyo Mugalu mwenyewe ni Sarpong wa timu yako. Anapata nafasi tano, anaitumia moja tu!
Hata wakaunda timu ya pamoja , huo uwezo wa kumfunga simba ndani nje hawana , na kama wangekua nao wangefanya vizuri kwenye makundi yao kuzidi Simba alivyofanya kwenye kundi lake , hakuna hata mmoja aliemfunika uwezo Simba
 
Haha hao jamaa ni balaa...

Kuna game moja waliwafunga Ile timu wapo nayo kundi moja ya waarabu inaitwa CR beloughzidad sijui huko[emoji1] ...jamaa walipigiwa pasi 43 ndo wakafungwa goli ....
Nasio kwamba hao waarabu ni wakisport sport ila ndo Ivo...

Hao mamelody ni balaa [emoji119]
Simba vs El Merrick iligonga pasi 49 , anyway, Mamelodi yuko kwenye kundi la viwete , sio wa kusifiwa
 
Siyo tu huna uzoefu na mpira wa Africa bali huna uzoefu na mpira wenyewe kabisa,nilipoona tu umeandika una asilimia 100 Simba kufika robo fainali nikajua kweli huna uzoefu,100%? kweli? kwenye mpira?

Simba na Al ahly ndo pekee wenye uwezo wa ku possess mpira kwenye timu zilizo kwenye 16 kweli? huijui hata Mamelody? I guess unaisikia tu.

Kifupi bandiko lako limejaa Mahaba hisia na dhahania kuliko uhalisia.
Mkuu povu la nini?
Jamaa kaweka disclaimer chini.
 
Siyo tu huna uzoefu na mpira wa Africa bali huna uzoefu na mpira wenyewe kabisa,nilipoona tu umeandika una asilimia 100 Simba kufika robo fainali nikajua kweli huna uzoefu,100%? kweli? kwenye mpira?

Simba na Al ahly ndo pekee wenye uwezo wa ku possess mpira kwenye timu zilizo kwenye 16 kweli? huijui hata Mamelody? I guess unaisikia tu.

Kifupi bandiko lako limejaa Mahaba hisia na dhahania kuliko uhalisia.
Simba kaishafuzu robo fainal

Ni kiasi gani unajiona ndezi muda huu kwa utabiri wako?
 
Simba vs El Merrick iligonga pasi 49 , anyway, Mamelodi yuko kwenye kundi la viwete , sio wa kusifiwa
mkuu mimi si mnazi .....ni mpenda soka tu.
Unazi ukizidi huwezi kuongelea mpira Kwa upana na uhalisia.

Simba msimu huu tupo vizuri ila ukiongelea mamelody hao jamaa wapo vizuri sana c msimu huu tu na c Tu Kwa mchezaji mmoja mmoja hata kucheza kitimu wana nidhamu haswa.
 
mkuu mimi si mnazi .....ni mpenda soka tu.
Unazi ukizidi huwezi kuongelea mpira Kwa upana na uhalisia.

Simba msimu huu tupo vizuri ila ukiongelea mamelody hao jamaa wapo vizuri sana c msimu huu tu.
Nakataa , wako kundi la viwete , zaid ya yeye hakuna timu nyingine iliyokua imeshinda mpaka juz Belouzdad anamfunga mazembe , timu zimecheza mechi 4 zote kutoa memelod zilikua na point 3 kushuka chini , Al Hilal tulicheza nao sisi , pale South katoka 2-1 kule Sudan wakatoka 0-0 , yuko kundi la viwete angekua kundi letu au la Esperance de Tunis asingepata point alizo nazo
 
Sawa mkuu ....

Case closed.
 
Al Hilal na Mazembe sio wazuri sana hao belouizdad wamepoteza game na mamelod kwa mkapa kwa ujinga wao wenyewe

Huweze cheza pale dhidi ya mamelod kama we mwarabu wangezingatia sana hili

Back
Top Bottom