Mleta mada umeandika mengi, ila binafsi hebu nitulie hapo kwa Magufuli na Tundu Lissu.
Umesema binafsi hauna chama, good; umeanza kuzungumzia tukio la Tundu Lissu kwa kulaumu uovu ule aliofanyiwa.
Baadae umesogea zaidi ukazumgumzia uhasama uliopo kati ya Lissu na Magufuli ( kwa mtazamo wako).
Halafu ukaja hapo chini kumlaumu Lissu kwa kuichafua Tanzania, hapa sasa ndio nataka unisome vizuri unijibu;
Tanzania kwa mtazamo wako ni nini?
a) Rais Magufuli
b) Eneo la ardhi linalounda nchi yetu.
Kama jibu lako ni (a) iko hivi;
Rais Magufuli akiwa kama kiongozi wa taifa la Tanzania, tukubaliane kwa nafasi yake alikuwa na uwezo wa angalau kuagiza uchunguzi ufanyike juu ya tukio lile la kushambuliwa Tundu Lissu. Lakini hakuwahi kufanya hivyo, huku sio kuichafua Tanzania, ni kusema ukweli juu ya maovu yanayotokea Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Sasa unapomshambulia Tundu Lissu anaichafua Tanzania kwenye hili ningependa kujua umetumia vigezo gani, na ningependa pia kujua wewe kwa upande wako ulitaka Lissu afanyaje kama wale wenye mamlaka ya kufanya kitu waliamua kukaa kimya?
Kama jibu lako ni (b) kwamba Tanzania ni eneo la ardhi, binafsi sijaona popote Lissu akilaumu kitu hicho, bali hulaumu yale yafanywayo ndani ya eneo hilo huku viongozi wake wenye mamlaka ya kuzuia hali hiyo wakiwa kimya, na hapa ndipo Lissu hu-base malalamiko yake.
Mara nyingi Lissu hutumia maneno; "Tanzania chini ya Rais Magufuli" akiwa anamaanisha Tanzania kama nchi, chini ya uongozi wa Rais Magufuli, kwamba huyu kiongozi ndie mwenye mamlaka ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia wake, bila kujali itikadi, rangi, dini, wala kabila.
Sent using
Jamii Forums mobile app