Mtazamo wangu kuhusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli

Nambie kaka

Ila ile kesi ya babu seya nimesikia sikia kuwa ilikuwa ya kutengeneza tu na haikuwa na ukweli ndani yake ndio maana raisi kawatoa. Ila wabakaji na walawiti huwa wanapata msamaha wa raisi?

..kesi ya kutengeza ndiyo ushindwe mpaka mahakama ya rufaa na ya afrika mashariki?

..wale ni mashoga na walawiti na Jpm alishikana nao mkuu ikulu.

..sasa tuambie alichosema Lissu unaweza kufananisha na alichotenda Jpm?
 
Naomba nirudi tena hapo kwenye Siasa za Upinzani:

Unadai siku hizi wapinzani hawasemi watajenga madarasa, hospitali n.k. hivyo kazi yao imebaki kulaumu tu.

Nikwambie jambo, kazi ya upinzani sio kujenga shule, hospitali, na vinginevyo. Kazi ya upinzani ni kuisukuma serikali iwapelekee wananchi maendeleo. Wapinzani hawakusanyi kodi.

Hivyo, ulivyosema Magufuli anajenga reli, barabara, hospitali, kwanza umekosea, Magufuli hatoi fedha zake mfukoni kujenga hivyo vitu, ni fedha zinazotokana na kodi za wananchi, na kama huwa unamsikiliza Magufuli vizuri huwa anasema fedha za watanzania.

Hivyo kwa hapa sikubaliani na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKAWA ni Nzi wa kijani iliyozubaa ukitaka kujua hilo leo hii Jiwe akisema anahamia upinzani watamshangilia na kumpa kila Aina ya sifa unafiki wa Watanganyika hauna kifani dunia hii.
Wenyewe wanafikiri usafi wa mwanasiasa ni kuwa chama flani.
Akivaa khaki tu anakuwa msafi na akivaa kijani tu anakuwa mchafu.
Akivaa kijani tu anakuwa mzalendo kwa taifa na akivaa khaki au bluu (blue) ni msaliti anatumiwa na mabeberu.

Akikosekana kwenye mavazi ya khaki na kijani basi kwao huyo mtu ni mnafiki hafai sababu hajachagua upande wa kuutetea mabaya na mazuri yake.
Huyu ndiye adui wao mkubwa sababu hatatetea mapungufu(uchafu) wa aina yeyote unaotendwa na kundi lao au viongozi wao.
Huyu ni hatari zaidi kwao sababu sio mtumwa wa fikra na hatumikii njaa ya tumbo lake. Huyu siyo dogmatic disciple wa kikundi chochote cha ulaji kilichojivika jina la chama cha siasa.
Huyu ni hatari sababu atadai hoja ya mgombea binafsi na kuzuwia fursa ya kupitisha uovu kutumia nguvu ya kikundi.
Huyu analeta uwezekano wa kuzuwia ulaji ruzuku wa wachache kwa mgongo wa jina la kikundi(chama).
Huyu huchukiwa na wote magamba ya kijani na magwanda ya khaki kama sio maganda ya bluu au zambarau.

Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi dogmatic maana yake ni kuwa mtiifu kwa bwana(master) wako kama mbwa(dog), unatii bila kuuliza maswali.
Dogmatic means to be loyal like a dog.
Kwani mbwa akiamrishwa kitu anamhoji mwenye mbwa kwanini nimng'ate yule, au kwanini nikae chini?
Yeye hutekeleza tu amri ya kung'ata au kumlinda bwana wake. Akiambiwa kaa chini au simama anatii bila maswali.
 

Kwa mtazamo wangu sio (a) wala (b), kwangu Tanzania ni watu, eneo la ardhi likiwepo bila sisi kuwepo hapa pasingekuwa Tanzania. Kwa mtazamo wangu ukifanya jambo kuhusu Tanzania umelifanya kwa watu wa Tanzania na si kwa ardhi ya Tanzania kama unavyoona wewe. .

Binafsinaomba mnielewe siwezi kushangilia Tundu Lisu kupigwa risasi hata kama sina undugu nae tuna damu ya UTANZANIA kewa hiyo naelewa kushindwa hata mabeberu huko ulaya. .

Ila hapa inavyoonekana hili jambi linapelekwa kisiasa sana kana kwamba Magufuli anajua aliyempiga risasi Tundu Lisu. Hapo ndio naposhindwa ku argue na yeyote yule alafu mtu kufanyiwa uhalifu anaweza kuwa kafanyiwa na yeyote na tukiweka list ya nadharia ya watu wanaoweza kufanya vile ni wengi mno. .

Ila nchi hii ni mamlaka, na mamlaka katika mapana yake kunamamlaka chini yake. Hii nchi ina polisi na hata huko ughaibuni kuna polisi kama interpols si ndiyo? Unaweza kupeleka kesi yako popote pale kama umeona polisi wa Tanzania hawawezi kukusaidia. Tundu Lisu kagoma kutoa ushirikiano wowote kwa polisi wa Tanzania, Hapo Magufuli anafanyaje? Kwamba aamru polisi wafanye kazi yake? Au watu wanachotaka ni kuwaMagufuli acheze wimbo wa Lisu ili mseme kuwa si mnaona anacheza ule wimbo wake? Hana Imani na raisi alafu leo tushangae kuwa kwa nini Magu anaendelea na yake?

Mie sitaki kubishana kuhusu Lisu ila chukiyake ilikuwa kabla ya kupigwa risasi, kinachotokea hapa ni public sympathy. Nakumbuka siku Lisu anapigwa risasi nilisali sana kwa Yesu amtie nguvu na nimalaani sana kitendo hicho. Lakini haimpi sababu ya kufanya anayoyafanya na kuyaeleza huko ughaibuni huku akilenga kuharibu Tanzania (nikimanisha sisi ndio tunaoumia sio Magufuli) kwa chuki binafsi dhidi ya Magufuli. .
 
Hapo kwa Magufuli na Wananchi wake, umezungumzia chuki iliyopo baina ya makundi mawili, ningependa kwa mtazamo wako utuambie nini chanzo cha hiyo chuki?

Hapo ndio utajua hao unaowaona wana chuki, je, wanasababu ya msingi kuwa na hiyo chuki ama hawana, but usilazimishe watu kuwa na furaha bila kuwa na sababu ya kuwa nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKAWA ni Nzi wa kijani iliyozubaa ukitaka kujua hilo leo hii Jiwe akisema anahamia upinzani watamshangilia na kumpa kila Aina ya sifa unafiki wa Watanganyika hauna kifani dunia hii.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Kitendo cha Chadema kumkubali kwa mikono miwili Lowassa waliokuwa wakimsema kuwa ni fisadi kwa miaka mingi lilinichekesha mpaka leo.
Aisee siasa za Tanzania ni za kuchekesha sana.
Halafu Lowassa aliporudi CCM wakaanza tena kumshushia mvua ya matusi. 😂😂😂😂😂😂
Nahisi Magufuli akihamia UPINZANI watamshangilia BALAA na WATAMSAFISHA KWELIKWELI 😂😂😂
 

Hujasoma nilichokiandika vizuri naomba ukasome tena

Nimeandika Upinzani kwa juhudi za kukusanya michango au kuwaleta wananchi pamoja wangeweza kuleta maendeleo mengi sana. Mfano wangeweza wakakusanya hela halafu wakanunua madawati, serikali ingekataa tu wananchi wangejua Upinzani unafanya kazi nyingi za kuleta maendeleo huku utawala unapinga huoni ingeleta tija kwa upinzani bila kutumia nguvu nyingi kushidana kwa kelele ambazo hazina msingi


Navyozungumza hivi naomba msininukuu vibaya mie napinga CCM kwa kuwa ni mbovu mno, hata viongozi wengi wanaochaguliwa ndani ya CCM na Magufuli wameonyesha udhaifu wa hali ya juu mbali na usomi wao .Ila vile vile napinga upinzani Pia kwa kunionyesha kuwa bado wanashindwa kuleta mabadiliko, hoja zao hata humu ndani ni matusi na kelele tu. .
 
Kama unasema Tanzania ni eneo jumlisha na watu waliopo, halafu unasema Lissu anaichafua Tanzania; binafsi sijawahi kumuona Lissu akiwalalamikia watanzania kwa kupigwa kwake risasi, siku zote Lissu analalamikia vyombo vya dola vilivyokuwa na jukumu la kuhakikisha ulinzi wake bali vikashindwa kutekeleza wajibu wao, na pia, Lissu anamlalamikia Magufuli, kwasababu kwa mamlaka yake alikuwa na uwezo wa angalau kuagiza uchunguzi ufanyike lakini hakufanya hivyo.

Sijui unafahamu tukio la siku Lissu anapigwa risasi ulinzi uliondolewa nyumbani kwake?

Na kamera za CCTV nazo ziliondolewa?

Kwa matendo hayo wewe binafsi unaweza vipi kuwa na imani na vyombo vya ulinzi?

Hata suala la Lissu kuwa na chuki hata kabla ya kupigwa risasi ni hisia zako tu, mtu kukemea uovu sio chuki, huwezi lazimisha kusifiwa hata pasipostahili.

Hivyo, argument yako kwamba Lissu anaichafua Tanzania (ukimaanisha watu na ardhi kama ulivyojibu mwenyewe) umekosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Siasa sio Matusi au Chuki, Hoja Hupingwa Kwa Hoja”
Huna hoja dogo zaidi ya kujikomba . Uzi umewafungulia wapinzani kuwananga as if wamemkwamisha mh Rais kutekeleza majukumu yake. Ukiomba kazi ya u Rais , wananchi wote ni wako. Wakupendao na wasiokupenda. Si kulipa visasi kwa wale wasiokukubali.

After all siasa za ki democracy zipo kikatiba na hazitgemei hisani ya mtu, kuvunja au kutokuvunja katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hii chuki imepandikwa na siasa CHAFU kwa sasa Tanzania tumekuwa na siasa za watu wachache wanao influence asilimia kubwa ya watu kwa kuwapandikiza CHUKI ikiwa kama mbinu ambayo inakuwa inafatwa kuingia madarakani

Mimi nnaamini kabisa kama huna jambo la kusema juu ya kitu basi ni vyema mtu akakaa kimya ila watu kwa kutaka kuleta matabaka huwa wanapandikiza CHUKI. Kitu ambacho ni kibaya sana tena kwa vizazi vinavyokuja. .

WaTanzania tunatakiwa tubadlike twende na mabadiliko Ya kidunia. Watu wengi ni wavivu mpaka wa kufikiri na wengi wamesoma lakini elimu yao haijawakomboa. Nadhani watu wamekosa ubunifu na kutengeneza fursa za maisha, ili wajifurahishe lazima watafute wa kumlaumu wakati wa kujilaumu ni wao wenyewe. Siku zote ukiona yako hayaendi uatatafuta uyapeleke wapi kulaumu ila lawama hazikusogezi mbele je unachukua maamuzi gani kusonga mbele?

Unaona maisha magumu hapa Tanzania? Kweli hujatembea nchi za watu. Tanzania inabidi tutoe maoni yetu yapelekw bungeni na kwa serikali ili tujue tunatatua changamoto zetu vipi, ila tukianza kuweka lawama hakuna kitakachofanyika kikamfurahisha mwenye lawama. Wale waliotua lawama wanasonga mbele tu. .
 

Wewe umekubali kabisa Tundu Lisu alivyojibu wakati anahojiwa kuwa Tanzania ikubali ushoga?
Mimi nazungumzia siasa zake za Tundu Lisu kuichafua Tanzania, wewe unazungumzia Tundu Lisu kupigwa risasi vitu viwili tofauti ila ngoja nikuwekee uzi ambao kuna walichangia mada yako:

JE Tundu Anti Pasi LISU analichafua TAIFA au anaichafua SELIKARI?JE serikali ni Taifa?
 

Samahani, ila propaganda zako zimeshindwa hata kabla hazijaanza. Kuna clip mataga mwenzako ameiweka hapa akidai kuwa Watanzania "tumebarikiwa" kwa kupata Rais "mnyenyekevu" wakati kwenye hiyo clip "Rais mnyenyekevu" anawatukana na kuwadhalilisha wasaidizi ALIOWATEUA yeye mwenyewe huku akikiri kuwa UCHUMI UMEDORORA.
Pole sana jomba.
 
Wewe umechukua ambacho kimekugusa ila nimeelezea mtazamo wangu tu sifanyi siasa
Wapinzani hawajamkwamisha Magufuli kufanya kazi zake mbona naona zinasonga mbele kama alivyopanga au kuna iliyokwama unieleze?

Nani kalipa kisasi kwa nani? hapo sijakuelew naomba unifafanulie

Kweli kabisa siasa za ki democracy zipo kikatika na hazitegemei hisani ya mtu, kuvunja katiba
 
Samahani Mfiaukweli mataga ni nini?
Mimi sijasema Magu hana mapungufu yake mbona mnanipiga mawe, Magu sio Mungu
Tubishane kwa Hoja tu ila sio kelele

Nifundishe na mie nielewe ambacho unadhani sikielewi
 

Are you stupid or something? Otherwise utasemaje kuwa "watu wachache wana influence watu wengi"? Does it mean unakiri kuwa majority ya Watanzania ni mbumbumbu wasioweza kufikiri wenyewe hadi wawe influenced?
 
Nambie kaka

Ila ile kesi ya babu seya nimesikia sikia kuwa ilikuwa ya kutengeneza tu na haikuwa na ukweli ndani yake ndio maana raisi kawatoa. Ila wabakaji na walawiti huwa wanapata msamaha wa raisi?
Lakini ndivyo mahakama zetu zilivyowahukumu. Na hakuna hukumu nyingine iliyoiua hukumu ya jaji Mihayo !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina wasiwasi kama wapinzani walivyokuwa wanasema watajenga mashule, barabara, n.k ulikuwa unawaelewa.

Hata hivyo wapinzani, na wananchi, bila ushirikiano na serikali iliyopo madarakani peke yao ni vigumu sana kujenga hivyo vitu.

Hujawahi kusikia kauli " serikali haipeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani?"

Au hivi karibuni mbunge viti maalum CDM alipeleka sare kwenye shule fulani Singida akanyimwa kuzigawa kwa wanafunzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…