Hamnaa!! Watu wa saint Kayumba wa Kibongo hawajui kingereza, mfano ni wewe hapa, humu kwenye JF huwa unaandika kituko cha kingereza, kila siku tunakusahihisha na kukuelimisha japo huwa kinakutesa sana na wenzako, ndio nyie mlioaminishwa kwamba kujua kingereza sio uzalendo, ilhali watoto wa vigogo wanakitumia freshi.
Hapo Bongo ni vigumu sana kumpata Mtanzania anayeongea kingereza vizuri na hana ajira, wote wameajiriwa maana kwa kweli kukijua kingereza ni raha sana, kwenye vikao utatiririka na kueleza issue mpaka inakaa, halafu napenda sana kukitumia nikiwa kwenye vikao vya wabongo maana wote hulala chali hamna maswali ya kijinga ya kuchelewesha muda, wanaokiongea na kuhoji hoji unakuta ni watu wenye akili mnaendana nao sawa na kazi zinafanyika.