Mtazamo Wangu: Tatizo la Simba SC kuwa na matokeo mabovu linaanzia hapa...

Salaam..

Nimekaa nikajiuliza, hasa baada ya timu pendwa ya Simba Sc kuwa matokeo yasiyoridhisha kwa mechi za hivi karibuni baada, hii ni baada ya kuchapwa 0-3 na mwarabu, na jana usiku, kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam.

Tukiondoa sababu nyingine kama wachezaji kukosa nafasi za wazi, ambalo limeonekana kuwa tatizo kwa sasa pale Simba Sc, umri wa wachezaji na uchovu kwa kucheza mfululizo miaka mingi, lakini pia naona bado kuna tatizo jingine kubwa ambalo nalo hatujalitazama kwa umakini.

Nimekaa nikajiuliza, hivi ni ipi mantiki kwa Simba Sc, hasa viongozi wake, kuamua kuwa na makocha wawili, wote wenye sifa za kuifundisha timu, wenye umri mkubwa, kwa wakati mmoja?

Kama walishaamua kufuata maoni ya mashabiki kwamba Mgunda alikuwa hatoshi, wakaamua kumleta Mzungu, sasa ni sababu ipi inayowafanya waendelee kuwa na Mgunda pale kwenye benchi la ufundi?

Huu mkanganyiko unaojitokeza sasa matokeo yake ni kama vile Simba Sc imegawanyika makundi mawili, ina kocha wa viongozi, Mgunda, na kocha wa mashabiki waliotaka Mgunda aondoke kwa kura, mzungu.

Sijui ni kitu gani kinachowashinda viongozi wa Simba Sc kumwambia Mgunda asante kwa kazi yako, wamlipe chake, kisha aondoke, wamwambie ukweli sasa tumeamua kwenda na uelekeo tofauti, uwepo wake kwneye benchi naamini unawavuruga wachezaji kwa namna fulani.

Tumeona nyakati kadhaa Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati mechi ikiendelea, huyu mtu anaweza kuwa anatoa malekezo tofauti na kocha mkuu anachotaka, matokeo yake ni kuwachanganya wachezaji, kwanini kocha mkuu asiachwe huru kufanya majukumu yake kwa nafasi?

Kwangu, viongozi wa Simba Sc ndio chanzo cha hili tatizo, kwani sijawahi kuona timu zinazojielewa hapa duniani zinakuwa na makocha wakuu wawili, hapa wanaajiri kocha mpya, na pale bado wanaendelea kubaki na yule wa mwanzo!, halafu tunajitapa tunakwenda kimataifa, mataifa yapi hayo?!

Viongozi wa Simba Sc pamoja na Mo wabadilike, waachane na mambo ya kimazoea na uswahili mwingi kwenye uendeshaji wa timu, tusipoamka mapema itakuwa too late.
Unamjua kaze wa yanga na huyu nabi,kaze aliwahi kuwa head coach wa yanga akanda akarudi.
Mwambusi pia yaliwahi kumkuta.
Na still timu ilishinda
 
Nani alokwambia simba sc ina makocha wakuu wawili? Muache mgunda nae apate rikizi mkuu punguza roho mbaya.Mgunda yupo kama daktari jadi(mfano mzuri reverse ya juzi) ndiyo kazi ya mgunda,angalia chuma ile alovaa mkononi ndiyo utajua inaitwa vyuma chakavu
Hii ndo akili mlitegemea kwenda nayo kucheza na waarabu?
 
Yalikua ni mawazo ya kipuuzi tu kumwacha Mgunda na kuleta kocha mwingine. Huyu kocha wa sasa hana mbinu. Mgunda mnamsingizia tu,angalia historia ya huyo kocha. Toka mwaka 2009 mpaka anakuja Simba,ni mwaka 2014-2016 pekee ndio alikaa na timu miaka miwili. Minginw yote alikua anakaa na timu mwaka mmoja mmoja pekee
Kwanini unasema kocha hana mbinu? Kama waahambuliaji wanapoteza nafasi za wazi kwanini kumlaumu kocha?
 
Pamoja na yote hayo ya benchi la ufundi na mambo yao kwangu tatizo mama la Simba ni kufeli kwenye sajili zake toka msimu uliopita.

Msimu ulipoita kati ya wachezaji wote tuliosajili ni Inonga na kanoute ndio ambao wanaoneoana kua sawa kiasi japo nao wana mapungufu yao weingine wote hamna lolote,Inonga ana makosa kadhaa ikiwemo na kucheza sana na majukwaa, overconfidence inayofanya kumsababishia hatari nyingi golini japo baadhi hua anazifanyia recovery.

Kanoute ana tank kubwa energy ya kutosha but not skilful hana maarifa mengi uwanjani yeye ni kukaba tu na rafu.

Sacko utoto mwingi hawezi kuku guarantee chochote anaweza cheza vibaya mna mwingi akafanya jambo moja likakufanya utabasamu inamana sio mchezaji wa kumtumainia.

Msimu huu yale yale katika wachezaji wote tuliosajili ni Phiri tu ndie tumeona kua tumepata wengine wote magalasa na anagalau Saidoo kaja kutupush kidogo January hapa lasivyo hali ingekua mbaya zaidi.

Leo hii kama tungefanya usajili vizuri Onyango asingeanza pale nyuma,Mzamiru asingeanza pale kati Bocco asingeanza pale mbele,Nakama nna mido mwingine wa maana hata kanoute haanzi,Sacko haanzi vilevile.

Tukajipange msimu ujao huu ushaisha
Usikate tamaa, tusubiri Uganda kesho jumamosi ndio tutajua hatma yetu ..
 
Unamjua kaze wa yanga na huyu nabi,kaze aliwahi kuwa head coach wa yanga akanda akarudi.
Mwambusi pia yaliwahi kumkuta.
Na still timu ilishinda
Kaze na Nabi nimeandika juu wanawlewana kwa sababu lugha wanayoitumia ni kifaransa, na Kaze anafanya kazi ya kutafsiri kwa kiswahili kwa wachezaji wao, ndio maana mambo yao yanaenda..
 
cha ajabu msimu ukiisha wazee wote watabaki alafu watauzwa wenye nafuu.
mfano aliachwa Gyan,Kahata,Chikwenda,Dunkan Nyoni,Ibrahim Ame wakabaki mizigo kisha wakaongeza mizigo mingine kina Oatara.dah,,,!
 
Tulia, kesho tunaanza moja Ug.
 
Salaam..

Nimekaa nikajiuliza, hasa baada ya timu pendwa ya Simba Sc kuwa matokeo yasiyoridhisha kwa mechi za hivi karibuni baada, hii ni baada ya kuchapwa 0-3 na mwarabu, na jana usiku, kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam.

Tukiondoa sababu nyingine kama wachezaji kukosa nafasi za wazi, ambalo limeonekana kuwa tatizo kwa sasa pale Simba Sc, umri wa wachezaji na uchovu kwa kucheza mfululizo miaka mingi, lakini pia naona bado kuna tatizo jingine kubwa ambalo nalo hatujalitazama kwa umakini.

Nimekaa nikajiuliza, hivi ni ipi mantiki kwa Simba Sc, hasa viongozi wake, kuamua kuwa na makocha wawili, wote wenye sifa za kuifundisha timu, wenye umri mkubwa, kwa wakati mmoja?

Kama walishaamua kufuata maoni ya mashabiki kwamba Mgunda alikuwa hatoshi, wakaamua kumleta Mzungu, sasa ni sababu ipi inayowafanya waendelee kuwa na Mgunda pale kwenye benchi la ufundi?

Huu mkanganyiko unaojitokeza sasa matokeo yake ni kama vile Simba Sc imegawanyika makundi mawili, ina kocha wa viongozi, Mgunda, na kocha wa mashabiki waliotaka Mgunda aondoke kwa kura, mzungu.

Sijui ni kitu gani kinachowashinda viongozi wa Simba Sc kumwambia Mgunda asante kwa kazi yako, wamlipe chake, kisha aondoke, wamwambie ukweli sasa tumeamua kwenda na uelekeo tofauti, uwepo wake kwneye benchi naamini unawavuruga wachezaji kwa namna fulani.

Tumeona nyakati kadhaa Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati mechi ikiendelea, huyu mtu anaweza kuwa anatoa malekezo tofauti na kocha mkuu anachotaka, matokeo yake ni kuwachanganya wachezaji, kwanini kocha mkuu asiachwe huru kufanya majukumu yake kwa nafasi?

Kwangu, viongozi wa Simba Sc ndio chanzo cha hili tatizo, kwani sijawahi kuona timu zinazojielewa hapa duniani zinakuwa na makocha wakuu wawili, hapa wanaajiri kocha mpya, na pale bado wanaendelea kubaki na yule wa mwanzo!, halafu tunajitapa tunakwenda kimataifa, mataifa yapi hayo?!

Viongozi wa Simba Sc pamoja na Mo wabadilike, waachane na mambo ya kimazoea na uswahili mwingi kwenye uendeshaji wa timu, tusipoamka mapema itakuwa too late.
Kwa mtazamo wangu kocha huyu mzungu na wao viongozi wameshamwona hafai kabisa Sasa mgunda atakuwa Kama backup Yao endapo huyu akishindwa Sasa ña mgunda hili ameligundua Kwa hyo ndo maana unaona na yeye anamwingiza Chaka mzungu kuanzia kwenye upangaji wa kikosi Hadi kwenye substitution huwezi kuwa kumuacha bocco acheze dakika 78_80 halafu Phil yupo benchi??
 
Nani alokwambia simba sc ina makocha wakuu wawili? Muache mgunda nae apate rikizi mkuu punguza roho mbaya.Mgunda yupo kama daktari jadi(mfano mzuri reverse ya juzi) ndiyo kazi ya mgunda,angalia chuma ile alovaa mkononi ndiyo utajua inaitwa vyuma chakavu
Mbona mnamuangalia sana mgosi?
 
Back
Top Bottom