MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Katika hali isiyo ya kawaida mgonjwa mmoja aliyekuwa akitaka kutoa hela kwa ajili ya matibabu alijikuta akizimia baada ya kukaa foleni kwa muda mrefu.
Katika benki ya NMB iliyopo Buzuruga plaza, yenye madirisha matano ya tellers, ni madirisha mawili tu yalikuwa yakifanya kazi, na katika madirisha hayo mawili dirisha moja lilimuhudumia mteja mmoja kwa zaidi ya masaa mawili huku dirisha moja lililobaki lilifungwa kuanzia majira ya saa 7 mpaka mishale ya kuelekea saa 9 na muhudumu huyo alisema ameenda kupata lunch nzito.
Kwa mbali niliwasikia mateller hao wakilalamika udogo wa mishahara ndio chanzo cha kufanya kazi kwa kusua sua.
Natoa ombi kwa mtu yoyote anayetaka kutumia NMB ajaribu matawi mengine, asije kusema hakuambiwa.
NMB Buzuruga ina watu wengi wa usafi na ulinzi kuliko wafanyakazi wa benki mpaka mmtu anijiuliza hivi hapa G4S au NMB?
Ili kupunguza matumizi inabidi NMB wapange jengo dogo kuendana na idadi ya mateller walionao, labda wafikirie kuchukua fremu hata Buzurga stendi- maana serikali nayo inasubiri gawio lake.