Mteja azimia NMB Buzuruga, ni baada ya kukaa kwenye foleni masaa manne

Mteja azimia NMB Buzuruga, ni baada ya kukaa kwenye foleni masaa manne

NMB Buzuruga panatisha. Nashauri watumishi wote pale wahamishwe na kuleta wapya. Kuna siku moja dada (teller) anayekaa dirisha la mwisho upande wa kulia. Alinitamkia neno ambalo ni aibu siwezi kuliandika humu.
 
Wakala, Online banking, Sim banking tusitumie tukaeni foleni masaa 4 tuzimie kukwepa tozo.
 
Huwa wanasemaga CRDB wana huduma mbovu ila mimi kuna siku walinihudumia vizuri tawi la UDSM hadi nikashangaa.
Yaani hadi muda wa kazi ukaisha wakafunga mlango na watu wa usafi wakaanza kudeki nikaambiwa tu ndugu mteja hamia huku! walihangaika hadi kuwasiliana na tawi lingine ili mradi tu tatizo langu liishe na likaisha baada ya nusu saa hivi baada ya benki kufungwa.

Muda mwingine ukitaka huduma nzuri na za haraka bank muwe mnafahamiana na staff wa bank, wewe hata foleni zitakuwa hazikuhusu ingawa sasa utakuwa unawaonea wateja wenzako.
Watu zaidi ya mil. 60 wote tufahamiane na staff wa benki patakuwa hapakaliki....
 
Tunasoma kwenye financial magazines kuwa NMB ndio bank inayotengeza faida kubwa baada ya kodi kuliko bank zote nchini. Ni bank bora na iliyo karibu na wateja nchi nzima.

changamoto ya huduma kwa foleni ipo kila mahali. Na kupunguza adha hiyo NMB wana App yao nzuri sana inaitwa NMB MKONONI. Kuna ATM kila mahali nchi nzima na wana NMB WAKALA kila sehemu. Hivyo foleni inaepukika.

Mleta mada soup hii umezidisha sana chumvi. Kuwa uliwasikia wakilalamika mishahara? Uongo!!! Lunch masaa mawili? Uongo!! Umesambaza uongo na sumu nyingi kwa sababu unazojua wewe. Lakini ujue tu NMB iko karibu yako kwa huduma bora kabisa.
 
Tumekustukia bank teller unataka uongeze mshahara hakikaa tutakujua na tutakufuta kazi
 
NMB wafanye maboresho hasa kwenye madirisha ya kutolea fedha. Mfano Benki inakuwa madirisha matano lakini yanayofanya kazi ni madirisha mawili tu?. Kwanini?.
 
Services za NMB zinazidi kuwa mbaya siku baada ya siku tangu wa Dutch waondoke. Kila siku wana sponsor activities. Give them another six months and they start being history
 
NMB wafanye maboresho hasa kwenye madirisha ya kutolea fedha. Mfano Benki inakuwa madirisha matano lakini yanayofanya kazi ni madirisha mawili tu?. Kwanini?.
sijui kwanini wanafanya hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom