Mtendaji wa Kijiji cha Hydom amshindilia makonde mwanakijiji. Asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Mtendaji wa Kijiji cha Hydom amshindilia makonde mwanakijiji. Asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa zinaonesha kwamba Mh Mtendaji anaitwa Adella na ni Mtendaji wa kijiji cha Hydom kilichopo Mbulu , mkoani Manyara.

Cha kushangaza ni kwamba Mwananchi aliyedundwa ndiye ameshtakiwa mahakamani kwa kumshambulia Mtendaji.

Nachukua nafasi hii kuwashukuru Wazalendo waliorekodi tukio hili la kishenzi na kulirusha mitandaoni.

ASIMAMISHWA KAZI

DED wa Mbulu, Hudson Kamoga amesema kuwa amemsimamisha kazi mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi kubainisha kilichopelekea mpaka mtendaji huyo kumshambulia mwanakijiji huyo.

Huu ni unyanyasaji na udhalilishaji mkubwa kwa wananchi.

Huyu mtendaji anatakiwa kushikiliwa na vyombo husika, achukulie hatua stahiki na muajiri wake kadri ya mkataba wa ajira,
Na achukuliwe hatua za kisheria kadri ya taratibu za vyombo vya afya, usalama wa raia na mahakama

Pamoja na yote hayo wasisahau kumpima akili huyu anaweza kuwa na tatizo
 
Huu ni unyanyasaji na udhalilishaji mkubwa kwa wananchi.
Huyu mtendaji anatakiwa kushikiliwa na vyombo husika, achukulie hatua stahiki na muajiri wake kadri ya mkataba wa ajira, na achukuliwe hatua ZA kisheria kadri ya taratibu za vyombo vya afya usalama na mahakama
Unaambiwa aliyeshitakiwa ni huyo mwanakijiji
 
Kushtakiwa inawezekana na inategemea nani aliwahi kwenye vyombo husika. Je, baada ya kushtakiwa amesikilizwa? Na hukumu imetoka?
Wapinga maendeleo lazima washughulikiwe
 
Tatizo linaanzia kwa viongozi wa juu. Busara ikikosekana ndio mambo kama haya yanatokea.

Mwezi huu au wa 12 mwaka jana. Kuna Mkuu wa Wilaya alimweka ndani mtendaji kata kwa sababu hakuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa.

Hivyo mwisho wa siku kila mmoja ana deal na anayemmudu.

Hiyo kesi mtashangaa inaisha kimya kimya.
 
Tatizo linaanzia kwa viongozi wa juu. Busara ikikosekana ndio mambo kama haya yanatokea. Mwezi huu au wa 12 mwaka jana. Kuna Mkuu wa Wilaya alimweka ndani mtendaji kata kwa sababu hakuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa.
Hivyo mwisho wa siku kila mmoja ana deal na anayemmudu.
Hiyo kesi mtashangaa inaisha kimya kimya.
Aiseeee !!
 
Huu ni unyanyasaji na udhalilishaji mkubwa kwa wananchi.

Huyu mtendaji anatakiwa kushikiliwa na vyombo husika, achukulie hatua stahiki na muajiri wake kadri ya mkataba wa ajira,
Na achukuliwe hatua za kisheria kadri ya taratibu za vyombo vya afya, usalama wa raia na mahakama

Pamoja na yote hayo wasisahau kumpima akili huyu anaweza kuwa na tatizo
Like father like a daughter.....mitano Tena!
 
Back
Top Bottom