Mtendaji wa Kijiji cha Hydom amshindilia makonde mwanakijiji. Asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Mtendaji wa Kijiji cha Hydom amshindilia makonde mwanakijiji. Asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Taarifa zinaonesha kwamba Mh Mtendaji anaitwa Adella na ni Mtendaji wa kijiji cha Hydom kilichopo Mbulu , mkoani Manyara.

Cha kushangaza ni kwamba Mwananchi aliyedundwa ndiye ameshtakiwa mahakamani kwa kumshambulia Mtendaji.

Nachukua nafasi hii kuwashukuru Wazalendo waliorekodi tukio hili la kishenzi na kulirusha mitandaoni.

View attachment 1681189

ASIMAMISHWA KAZI

DED wa Mbulu, Hudson Kamoga amesema kuwa amemsimamisha kazi mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi kubainisha kilichopelekea mpaka mtendaji huyo kumshambulia mwanakijiji huyo.

View attachment 1681405
Huyu ni mwananchi ni me au ni ke?
 
Hii Halmashauri ya Mbulu ina majanga, mara VEO kashusha kipondo huku nako tunasikia imekua ya mwisho kwa ukusanyaji wa mapato yani ni vurugu mechi
 
Huyo mwananchi hajadundwa vizuri.

Nashauri watendaji wapewe SMG ili kuwapiga risasi wataogoma kutoa michango ya ujenzi wa madarasa.

Hii nchi ni tajiri sana, tumelalliwa sana ndugu zangu.

MITANO TENA.
Kweli kabisa. Tumecheza sana haiwezekani hata vyumba tunavyolala na wake zetu vijengwe kwa hisani ya wamarekani. Mitano tenaaaaa.Alaaa!
 
Huyo mwananchi hajadundwa vizuri.

Nashauri watendaji wapewe SMG ili kuwapiga risasi wataogoma kutoa michango ya ujenzi wa madarasa.

Hii nchi ni tajiri sana, tumelalliwa sana ndugu zangu.

MITANO TENA.
Itabidi waanze kukupiga risasi wewe kwanza.
 
Mara paaaa,ili kumiliki simu ya smart phone na simu ya camera lazima uwe na leseni.
Hizi ndoto zinaanaga kama utani lakini mwisho inakuwa kweli.
Makofi kwa mtendaji tafadhali paaaa paaa paaaa paaaaaaaaaaaaa.
 
Back
Top Bottom