Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC | Ligi kuu Bara| Manungu Morogoro

Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC | Ligi kuu Bara| Manungu Morogoro

1642860074907.png
 
Sijajua Kwanini @Moderators Wameondoa Uzi wa Mwanzo, muwe munaweka na sababu za kuondoa Uzi

NBC Premier League leo Jumamosi. Baada ya kupita miaka zaidi ya 20, leo Mnyama Simba SC anarudi katika dimba la Manungu kucheza na Mtibwa Sugar, huku Kila upande ukitamba kuondoka na alama tatu.

Je ni Mtilwa Sugar au Simba SC kuondoka na alama tatu? majibu utayapata JF.

HEAD TO HEAD

Tokea mwaka 2016 Mtibwa sugar na simba wameshakutana mara 10, simba akishinda michezo 7 na sare 3, mtibwa hajawahi kumfunga Simba Sc tokea Mwaka 2016

UPDATE.

Katika ligi kuu Simba yupo nafasi ya pili akiwa na jumla ya alama 24 baada ya kucheza michezo 11, nyuma ya vinara wa ligi Young africans ambao wana alama 32 baada ya kucheza michezo 12.

Simba amecheza michezo 11, amepoteza mchezo mmoja, ametoa sare michezo 3 na ameshinda michezo 7

Mtibwa sugar Yupo nafasi ya 14, nafasi ya 3 toka mwisho akiwa amecheza michezo 12

UPDATE

Hali ya uwanja ilivyo kwa sasa ambako mechi itapigwa

Hali ilivyo katika Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro hadi saa 6 mchana.

Uwanja huo unategemewa kutumika leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar FC dhidi ya Simba SC, saaa 10:00 jioni.
View attachment 2091644


UPDATE

Hadi sasa saa 9 na dakika 05 vikosi bado havijatoka

KIKOSI CHA SIMBA

View attachment 2091704

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR

View attachment 2091741

-Mpira umekwisha kuanza hapa Uwanja wa Manungu Morogoro.

- 3' Inonga anafanyiwa madhambi

-5' Mtibwa wamecha faulo 3 dhidi ya moja kwa simba

- 09' Kihimbwa anafanyiwa madhambi

-10' Ndemla anafanya shambulizi lakini Manula anaokoa vizuri

-12' Abraham anafanyiwa madhambi na Yuko chini akigangwa

-14' Kagere anacheza madhambi

-20' Mtibwa Sugar 0 Simba sc 0

-21' Mtibwa wanapata kona ya kwanza katika mchezo huu

-24' Mtibwa sugar wanapata kona

-27' Mtibwa Sugar offside

-30' Mtibwa Sugar 0 Simba Sc 0

-
31' Kado golokipa wa Mtibwa anakoa hapa na simba wanapata kona ya kwanza

-34' Mtibwa wanapata kona

-35' Mtibwa wanapiga kona ya 4

-40' Mtibwa Sugar 0 Simba Sc 0

- 41' Kadi ya njano anapewa George

-44' H. Dilunga anapiga shoot linaenda nje ya lango

- 45" Bila Bila

- Dakika 3 za Nyongeza kipindi cha kwanza

-Kipindi Cha kwanza kimemalizika Mtibwa Sugar 0 Simba sc 0
Pablo afungashiwe virago fasta kabla hajaifanya simba icheze kama gwambina au ihefu
 
Wanafanya hujuma za wazi wazi kabisa

Hii TFF kwasababu simba ilikataa mkataba wa mchongo aliosaini na GSM basi TFF imekuwa ikimuandama simba
Acheni uswahili, timu ngapi zimecheza hapo Manungu na hazijalalamika nyie ni nani muonekane mnaumuhimu sana kuliko timu zingine?
 
Acheni uswahili, timu ngapi zimecheza hapo Manungu na hazijalalamika nyie ni nani muonekane mnaumuhimu sana kuliko timu zingine?
Sio tu kucheza Manungu, hoja ni kwamba hizo timu ziliukuta uwanja katika hali gani
 
Simba inashinda hii mechi wala sina mashaka
 
Uzi umepoa sana huu, au mnyama haupigi mwingi huko majarubani??
 
Acheni uswahili, timu ngapi zimecheza hapo Manungu na hazijalalamika nyie ni nani muonekane mnaumuhimu sana kuliko timu zingine?
Swala la timu zingine kucheza kwenye kiwanja kibovu sio sababu ya simba wapenda soka kulizungumzia.Hii ni aibu yakujitakia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Dakika 50 simba imeongeza mashambulizi zaidi kwenye lango la mtibwa
 
Back
Top Bottom