Mtifuano mkali kati ya Wizara ya Afya na vyuo vya afya juu ya kubadili qualifications za kujiunga pharmacy ngazi ya cheti

Action and Reaction

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2021
Posts
1,438
Reaction score
1,496
Mshikeshike, mtifuano unaendelea kuhusu kubadili sifa za kujiunga na astashahada kutoka D mbili za Chemistry na Biology kwenda C mbili au zaidi za Chemistry na Biology!

Kiukweli, sifa zinazopendekezwa na serikali zitaathiri vyuo vya afya vinavyotoa hii kozi! C mbili za Chemistry na Biology ni kubwa mno kwa wanafunzi wetu, hivyo wizara haitendi haki kwa wanafunzi wetu waishio Tanzania.

Na mpaka sasa wizara haijatoa tamko lolote maana kikao kilikuwa na mtimtimti kikahairishwa kama si kuvunjika kabisa!

Serikali ya CCM, chama langu, muwasikilize Watanzania!
 
D2 kwa somo la fani maalum ni dharau kwa fani husika.

Haya mambo tuwaachie wanajeshi na polisi wao matokeo ya vyeti hayana maana ktk kozi zao,ni afya timamu na akili timanu.
Wewe hiyo D nne zinzotakiwa ila Mbili lazima ziwe za Kemia na Biology
 
Hata hivyo vyuo vimekuwa vikitapeli wanafunzi kwa kuwadanganya wanafunzi haiwezekani darasa la wanafunzi 200 wafuaulu 20 halafu waliofeli uwadanganye warudie mtihani mwakani wafeli tena huku wanazidi kulipia mtu anasoma certificate kwa miaka 4 na hamalizi mpaka anakimbia mwenyewe
Mshikeshike, mtifuano unaendelea kuhusu kubadili sifa za kujiunga na astashahada kutoka D mbili za Chemistry na Biology kwenda C mbili au zaidi za Chemistry na Biology!

Kiukweli, sifa zinazopendekezwa na serikali zitaathiri vyuo vya afya vinavyotoa hii kozi! C mbili za Chemistry na Biology ni kubwa mno kwa wanafunzi wetu, hivyo wizara haitendi haki kwa wanafunzi wetu waishio Tanzania.

Na mpaka sasa wizara haijatoa tamko lolote maana kikao kilikuwa na mtimtimti kikahairishwa kama si kuvunjika kabisa!

Serikali ya CCM, chama langu, muwasikilize Watanzania!
 
Kiukweli kwa kozi za Afya kupewa D2 kunashusha thamani na ubora wa wanafunzi. Angalau warudishe kama zamani hizo C2 ambazo ni lazima.
 
Hakuna tofauti kati ya D mbili na C mbili

Kwani akiwa na C mbili ndio itaongeza ufanisi kumzidi mwenye D mbili au?
 
Hata hivyo vyuo vimekuwa vikitapeli wanafunzi kwa kuwadanganya wanafunzi haiwezekani darasa la wanafunzi 200 wafuaulu 20 halafu waliofeli uwadanganye warudie mtihani mwakani wafeli tena huku wanazidi kulipia mtu anasoma certificate kwa miaka 4 na hamalizi mpaka anakimbia mwenyewe
Wanafaulu vizuri tyu labda wasiojituma kusoma!
 
Hata hivyo vyuo vimekuwa vikitapeli wanafunzi kwa kuwadanganya wanafunzi haiwezekani darasa la wanafunzi 200 wafuaulu 20 halafu waliofeli uwadanganye warudie mtihani mwakani wafeli tena huku wanazidi kulipia mtu anasoma certificate kwa miaka 4 na hamalizi mpaka anakimbia mwenyewe
Acha uongo mzee baba
 
Kwani hizo d ndizo zitampa cheti cha ufaulu huko chuo, ishu sio d wala c, ishu ni elimu yenyewe inayotolewa, kama kweli huyu mwenye d hana uwezo huo. Je anawezaje ku qualify na kupata hicho cheti cha chuo?
 
D mbili ni dharau kwa fani husika, hapo ni mwendo wa C tu, watu wajikaze wapambane, wasome, wapate c 2. Si kutuletea watu hawajui mambo vema.
Mtu anae pata c2 either anajuinga na advance au anapagiwa katika vyuo au sekondari za serikali.kwa maana hiyo vyuo private vitakufa rasmi kama shule za high school za binfsi zinavo kufa taratibu......
 
D2 kwa somo la fani maalum ni dharau kwa fani husika.

Haya mambo tuwaachie wanajeshi na polisi wao matokeo ya vyeti hayana maana ktk kozi zao,ni afya timamu na akili timanu.
unakuwaje na akili timamu katika D mbili??? Ndo maana Polisi wanafanya mambo ya hovyo hovyo maana huwezi kuwa na utimamu wa akili ktk D mbili.
 
Usikariri,aliyekwambia akili ni matokeo ya juu ya shule ndiye huyu kakuacha na cheti chako safi hujui hata unaamka na idea gani.

Upuuzi wa polisi hauhusiani na matokeo kabisa,kwani kuna maproff wangapi ndani ya serikali wanafanya mambo ya ajabu kabisa!!!,na hata hivyo wapo polisi na matokeo hayo hayo ya d 2 wana akili safi tu.

Kuamini matokeo ya darasani zaidi katika kila sekta nayo ni dalili ya kutokuwa na akili.
 
Mshikeshike, mtifuano unaendelea kuhusu kubadili sifa za kujiunga na astashahada kutoka D mbili za Chemistry na Biology kwenda C mbili au zaidi za Chemistry na Biology!

Kiukweli, sifa zinazopendekezwa na serikali zitaathiri vyuo vya afya vinavyotoa hii kozi! C mbili za Chemistry na Biology ni kubwa mno kwa wanafunzi wetu, hivyo wizara haitendi haki kwa wanafunzi wetu waishio Tanzania.

Na mpaka sasa wizara haijatoa tamko lolote maana kikao kilikuwa na mtimtimti kikahairishwa kama si kuvunjika kabisa!

Serikali ya CCM, chama langu, muwasikilize Watanzania!
Wamechelewa sana. Kuna utitiri wa wanafunzi kusomea afya kisa D mbili, shenzi.
Hata masomo mengine, wapandishe grades, ili elimu iwe na thamani.
 
Back
Top Bottom