Mshikeshike, mtifuano unaendelea kuhusu kubadili sifa za kujiunga na astashahada kutoka D mbili za Chemistry na Biology kwenda C mbili au zaidi za Chemistry na Biology!
Kiukweli, sifa zinazopendekezwa na serikali zitaathiri vyuo vya afya vinavyotoa hii kozi! C mbili za Chemistry na Biology ni kubwa mno kwa wanafunzi wetu, hivyo wizara haitendi haki kwa wanafunzi wetu waishio Tanzania.
Na mpaka sasa wizara haijatoa tamko lolote maana kikao kilikuwa na mtimtimti kikahairishwa kama si kuvunjika kabisa!
Serikali ya CCM, chama langu, muwasikilize Watanzania!