Pre GE2025 Mtifuano wa Uchaguzi wa CHADEMA kwenye Kanda usipime. Hakuna mwenye uhakika wa kushinda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa ya sasa inayozunguka kila mahali.
===

Pazia la uchukuaji na urejeshaji fomu za kusaka uongozi katika kanda nne za kiuongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), linafunguliwa rasmi leo Ijumaa Aprili 12 hadi 22, saa 10 alasiri.

Nafasi zinazowaniwa ni mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kanda, mweka hazina na katibu wa kanda. Kanda hizo ni Victoria, Magharibi, Nyasa na Serengeti zinazounda mikoa ya Mwanza, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Njombe, Mara, Rukwa, Katavi, Tabora, Songwe na Kigoma.

Kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi lililotolewa leo Ijumaa Aprili 12, 2024 na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Benson Kigaila limeeleza kuwa fomu za kuwania nafasi hizo zitapatikana kwa makatibu wa mikoa na tovuti ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Miongoni wa vigogo wanaotajwa kuchukua fomu ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' atakayechuana na Mchungaji Peter Msigwa anayetetea uenyekiti wa kanda ya Nyasa. Wengine ni mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu atakayekabiliana na Ezekiah Wenje katika Kanda ya Victoria.
 
Endeleeni kujiimarisha wakati majirani wakigawana mbao za mtumbwi wakiwa katikati ya bahari.
 
Lakini hao wote mumejiridhisha kwamba ni wenye shibe, hawana njaaa??. Maaana hamchelewi kuwaatukana eti wananjaa kali pale wanapotaka kutumia uhuru wa utashi wa kuwa wanachama wa chama wakitakacho.
 
Back
Top Bottom