fidelity
Member
- Apr 22, 2012
- 91
- 11
Katika hali isiyo ya kawaida, OCD wilaya ya Kondoa amempiga mateke, ngumi, vibao na kumchania shati mkuu wa shule wa shule ya sekori Kikore wilayani hapo.
Tukio hilo lilitokea jana 03/11/2013 ambapo kamati ya wilaya iilipopita shuleni hapo kusambaza mitihani ya kidato cha nne iliyoanza leo hii.OCD huyo alimuuliza mkuu wa shule "STRONG ROOM IKO WAPI?" mkuu wa shule akawaonesha chumba cha darasa ambacho hutumika kama ofisi ya mkuu wa shule na staff ya walimu,ndipo OCD alipoanza kutoa matusi ya nguoni akitaka kuoneshwa strong room nyingine, mkuu alipokosa majibu ndipo OCD alianza kumpatia kichapo kikali kilichosababisha majereha katika mwili wake.
Katika hali ya kushangaza wajumbe waliokua wameandamana na OCD huyo ambao ni AFISA ELIMU MSAIDIZI WA WILAYA, NA AFISA USALAMA WA WILAYA WALISHANGILIA TUKIO HILO JAMBO LILOMFANYA MKUU WA SHULE KUKOSA MSAADA.
Aidha shule ya sekondari ya Kikore ni moja ya shule za kata ambayo haina jengo la utawala na upungufu mkubwa wa miundombinu hivyo kumlazimu mkuu wa shule kuchukua chumba kimoja cha darasa na kukigawa upande mmoja kua ofisi yake na upande mwingine ofisi ya walimu wote.
POLE SANA MKUU WA SHULEPOLENI SANA WALIMU WA TANZANIA!