Mtihani kidato cha nne: OCD wilaya ya Kondoa ampiga vibaya mkuu wa shule wa Kikore

Mtihani kidato cha nne: OCD wilaya ya Kondoa ampiga vibaya mkuu wa shule wa Kikore

Katika hali isiyo ya kawaida, OCD wilaya ya Kondoa amempiga mateke, ngumi, vibao na kumchania shati mkuu wa shule wa shule ya sekori Kikore wilayani hapo.

Tukio hilo lilitokea jana 03/11/2013 ambapo kamati ya wilaya iilipopita shuleni hapo kusambaza mitihani ya kidato cha nne iliyoanza leo hii.OCD huyo alimuuliza mkuu wa shule "STRONG ROOM IKO WAPI?" mkuu wa shule akawaonesha chumba cha darasa ambacho hutumika kama ofisi ya mkuu wa shule na staff ya walimu,ndipo OCD alipoanza kutoa matusi ya nguoni akitaka kuoneshwa strong room nyingine, mkuu alipokosa majibu ndipo OCD alianza kumpatia kichapo kikali kilichosababisha majereha katika mwili wake.

Katika hali ya kushangaza wajumbe waliokua wameandamana na OCD huyo ambao ni AFISA ELIMU MSAIDIZI WA WILAYA, NA AFISA USALAMA WA WILAYA WALISHANGILIA TUKIO HILO JAMBO LILOMFANYA MKUU WA SHULE KUKOSA MSAADA.

Aidha shule ya sekondari ya Kikore ni moja ya shule za kata ambayo haina jengo la utawala na upungufu mkubwa wa miundombinu hivyo kumlazimu mkuu wa shule kuchukua chumba kimoja cha darasa na kukigawa upande mmoja kua ofisi yake na upande mwingine ofisi ya walimu wote.

POLE SANA MKUU WA SHULEPOLENI SANA WALIMU WA TANZANIA!

Hebu toa details zilivyokuwa bwana mbona umeanza juu juu tu kama kasuku? Yaani Mkuu wa shule kutokuwa na Strong Room ndo OCD akaanza kumpiga? Ninavyoona ni kama umekuja kushitaki hapa, hebu tupe chanzo na kama kweli Polisi alifanya hilo unalolisema as easy as that maana yake ni kama ana matatizo ya akili. Hebu nipe source nidadavue mwenyewe mtoa mada.
 
kaulii ya PINDA.....na wapigwe tu! hii cyo haki kabisa ni uonevu,,,pole mwalimu
 
Stori imepikwa, ikawekewa chumvi, rangi ya mboga, mdarasini, kachumbali, nyanya, nk.
 
Nichemba maalumu iliopo ndani ya ofisi kwa ajili ya kutunzia vitu vya siri kama mitihani, vyeti vya wanafunz waliomaliza, faili za siri za walimu au watumishi na hata fedha sometimes still cabinet zaweza tumika kama strong room.umenipata wangu?

asante nilikuwa sijui
 
imenisikitisha sana aisee,mi ningerusha mangumi liwalo na liwe aisee,tena ningemtoboatoboa na kalamu hadi wamsahau

Ha ha ha ha! Mkuu you've made my day! Yaani nimecheka sana! Ungemtoboa OCD na kalamu sio! Kumbuka yeye ana bastola kiunoni!
 
Strong room shuleni? imekuwa bank chumba cha kuhifadhia hela au polisi chumba cha kuifadhia silaha? Huyo ocd na baazazi tu, afisa elimu mwl wako anapigwa unaangalia tu wakati shule zako zoote hapo wilayani unajua zilivyo, shame on you
Kazi kweli kweli........jamani strong room ndo room gani
 
halafu walimu wengine wakawa wanafanya nini wakati mwalimu mkuu anapigwa na kudhalilishwa namna hii? huo umoja upo wapi wa walimu maeneo yao ya kazi?

ocd anapata wapi mamlaka haya ya kuwapiga watumishi wenzake wasio na hatia ya uvunjifu wa sheria?
ama kweli nchi yetu imefika wakati kila mtu anajiamulia kitu chake.
 
.
.
.
.
.
.
bado 2015 unawakuta walimu.......iyena iyenaa iyena iyenaaa che che me numbari one!.....m@anina,na bado mtapigwa sana mwaka huu.

Ukombozi wa nchi hii utakamilika tu walimu watakapokoma kukubali kutumika kama karatasi za chooni; yaani umuhimu wao kwa CCM huonekana chaguzi zinapojiri tu, hapo hugawiwa kofia, T-shirts za midebwedo, wengine tai na elfu kumi kumi za "posho" (takrima a.k.a rushwa) ambapo walimu hupagawa mithili ya mtu aliyepandisha mashetani kichwani na kuwa tayari kuwasaidia wahalifu hawa CCM kwa lolote ikiwa ni pamoja na kuwaibia kura!
Ila sasa kuna jambo linatia moyo, pole pole wameanza kujitambua kwamba wao si miongoni mwa "wenzetu" na kwa vitendo kama cha huyu PolisiCCM naona ujumbe watauelewa.
 
Mkuu wa shule naye boya tu, tatizo wakuu wengi wa shule wameupata kwa kujikomba hvyo wako tayari hata kuwa tigolized ili wasipoteze vyeo, na bado watapigwa sana!
 
Katika hali isiyo ya kawaida, OCD wilaya ya Kondoa amempiga mateke, ngumi, vibao na kumchania shati mkuu wa shule wa shule ya sekori Kikore wilayani hapo.

Tukio hilo lilitokea jana 03/11/2013 ambapo kamati ya wilaya iilipopita shuleni hapo kusambaza mitihani ya kidato cha nne iliyoanza leo hii.OCD huyo alimuuliza mkuu wa shule "STRONG ROOM IKO WAPI?" mkuu wa shule akawaonesha chumba cha darasa ambacho hutumika kama ofisi ya mkuu wa shule na staff ya walimu,ndipo OCD alipoanza kutoa matusi ya nguoni akitaka kuoneshwa strong room nyingine, mkuu alipokosa majibu ndipo OCD alianza kumpatia kichapo kikali kilichosababisha majereha katika mwili wake.

Katika hali ya kushangaza wajumbe waliokua wameandamana na OCD huyo ambao ni AFISA ELIMU MSAIDIZI WA WILAYA, NA AFISA USALAMA WA WILAYA WALISHANGILIA TUKIO HILO JAMBO LILOMFANYA MKUU WA SHULE KUKOSA MSAADA.

Aidha shule ya sekondari ya Kikore ni moja ya shule za kata ambayo haina jengo la utawala na upungufu mkubwa wa miundombinu hivyo kumlazimu mkuu wa shule kuchukua chumba kimoja cha darasa na kukigawa upande mmoja kua ofisi yake na upande mwingine ofisi ya walimu wote.

POLE SANA MKUU WA SHULEPOLENI SANA WALIMU WA TANZANIA!
Wapigwe tu... Tumechoka... Source Pinda
 
Nimesoma Thread Moja Huko Dodoma mwalimu Mkuu Amepigwa Na OCD Kisa Shule Haina Strong Room. Binafsi Nalaani Kitendo Kilichofanywa Na OCD dhidi ya mwalimu huyo kwani ni kitendo cha kinyama sana. pili ni nani anayepaswa kujenga miundo mbinu ya shule ikiwemo teachers' office? bila chembe ya shaka ni serikali. je iweje huyo OCD Achukue Sheria Mkononi Kwa Kumkandamiza Mkuu Wa Shule Kichapo?. Tatu OCD Hana Uelewa Kweli Wa Taaluma Yake? Amekosa Maadili Ya Uongozi. Ndugu Walimu Wakati Wa Kuonewa Sasa Umekwisha. Tuungane Kwa Maandamano Ambayo Kimsingi Ni Haki Ya Kila Raia Kulaani Kitendo Hicho.
 
Huyo mwalimu atakuwa legelege sana ma ocd wa kizazi hiki wote wazembe tu, angemkandika hata matofali ya uso.
 
Mimi si mwalimu lakini ninachukia sana watu wenye tabia ya kutukana na kuzarau walimu kama wewe, hujasomeshwa wewe? alafu mnatakiwa kujua wewe unavyomuogopa bosi wako akija na wageni ata walimu ndivyo walavyowaogopa maafisa elimu wanapokuja na wageni, ingawa kwa mtu mwingine hawezi kukubali
Mkuu wa shule naye boya tu, tatizo wakuu wengi wa shule wameupata kwa kujikomba hvyo wako tayari hata kuwa tigolized ili wasipoteze vyeo, na bado watapigwa sana!
 
Strong room shuleni? imekuwa bank chumba cha kuhifadhia hela au polisi chumba cha kuifadhia silaha? Huyo ocd na baazazi tu, afisa elimu mwl wako anapigwa unaangalia tu wakati shule zako zoote hapo wilayani unajua zilivyo, shame on you

Usishangae ram, ni kweli kiutaratibu lazima kila shule iwe na Strong Room (Chumba Madhubuti) kwani kama zinavyohifadhiwa pesa kwenye strong Room ya Bank basi Shuleni kuna nyaraka za muhimu kama Vyeti pamoja na Mitihani ambavyo havina budi kuhifadhiwa humo. Ndio maana wakati mwingine unamaliza shule na unaweza kukaa hata miaka kadha na uongozi wa shule ukabadilika lakini ukifuata cheti chako utakikuta salama, kipya as if ndo kimetoka NECTA...
aIONE Heaven on Earth.

BACK TO THE TOPIC,
Ndugu zetu askari nadhani wana tatizo kichwani kama mmoja alivyosema mabangi yanawasumbua. Wakuu wa Shule za Kata wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana sasa anampiga hiyo shule ni ya mama yake? Ajengee mshahara? Na je alimpelekea fungu la kufanya hivyo akakuta hajajenga? Yeye ni mamlaka yake ya ajira? Sheria zinaruhusu?
Mleta mada kama hii kitu ni ya kweli msaidie huyo mkuu apate publicity then haki ichukue mkondo wake.
 
polisi wamezidi uonevu usio na maana cc Charles Kenyela ona uonevuuuu... wanasheria hii ndi sehemu yakutoa msaada. polisi wamezidi kujiona miungu watu.
 
Last edited by a moderator:
Chama Cha Waalimu Tanzania hebu shughulikieni hilo ili asilimia mbili ya mshahara wa mwalimu huyo aone mnaikata kihalali
alaaniwe kikaragosi huyo aliyepiga mwalimu wetu
 
Back
Top Bottom