Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Kuna mtu alitahadharisha kwamba sifuni mchome asipewe cheo alichonacho .
 
Kiswahili = noun
Swahili = adjective
Swahili language is correct because SWAHILI as an adjective modifies the noun LANGUAGE.
KISWAHILI stands alone as a noun.

Hamna suffix "Ki" katika Kiingereza. Hicho ni Kibantu. Ndio maana kamusi za Kiingereza hukuti
"Kiswahili" bali "Swahili" . Ila kuna watumiaji wanalazimisha tu. Lugha yetu kwa Kiingereza ni Swahili, anayobisha atafute kamusi ya Kiingereza.
 
Hamna suffix "Ki" katika Kiingereza. Hicho ni Kibantu. Ndio maana kamusi za Kiingereza hukuti
"Kiswahili" bali "Swahili" . Ila kuna watumiaji wanalazimisha tu. Lugha yetu kwa Kiingereza ni Swahili, anayobisha atafute kamusi ya Kiingereza.

"Ki" ni prefix na sio "suffix"
"Kiswahili" ndio jina la lugha yetu na sio "Swahili"
Kwa mtazamo wako kama mtu anaitwa Maganga kwa Kiingereza aitwe "Ganga ?"
 
"Ki" ni prefix na sio "suffix"
"Kiswahili" ndio jina la lugha yetu na sio "Swahili"
Kwa mtazamo wako kama mtu anaitwa Maganga kwa Kiingereza aitwe "Ganga ?"

Sio kweli kuhusu jina la Mtu. Mtu ataitwa jina lolote analolitaka kuitwa.

Hata iwe prefix, niletee kamusi ya Kiingereza inayosema lugha yetu ni "Kiswahili" badala ya Swahili.
 
Sera mpya ya elimu iliyotolewa rasmi jana imekua gumzo kwenye vyombo vya babari na tovuti mbalimbali mitandaoni, kubwa zaidi ni elimu ya msingi kuongezeka mpaka kufikia miaka 10 badala ya 7, na sekondari kubakia miaka miwili tu katika mfumo ufuatao; 1+6+4+2+3. na hii ina maana

1=ELIMU YA AWALI
6=DARASA LA KWANZA MPAKA LA SITA
4=DARASA LA SABA MPAKA LA KUMI
na hio ndio itakua basic education kwa kila mwanafunzi,
2=ELIMU YA SEKONDARI
3=ELIMU YA JUU

Niki~nukuu sura mpya ya mitaala ya ufundishaji katika vyuo vya ualimu na elimu ya juu kwa education programme, walisema

"diploma ya kawaida elimu ya msingi itatolewa kwa miaka mitatu huku walimu kazini wakiombwa kuongeza taaluma zao kwa miaka miwili (diploma ya kawaida elimu kazini) na wahitimu watafundisha shule za msingi pia diploma ya elimu ya juu itatolewa miaka mitatu sawa na shahada na wahitimu watafundisha sekondari"

SASA JE?

Hii elimu ya msingi mpya itafundishwa na wailimu wenye sifa zipi?
 
Sio kweli kuhusu jina la Mtu. Mtu ataitwa jina lolote analolitaka kuitwa.

Hata iwe prefix, niletee kamusi ya Kiingereza inayosema lugha yetu ni "Kiswahili" badala ya Swahili.

Hao wazungu wanatakiwa wajue kuwa lugha yetu ni "Kiswahili " na sio "Swahili " hata kama walikosea kuchapisha kama walivyokosea kuandika majina ya maeneo mbalimbali ya nchi yetu, hatuwezi kukubali hali kama hii iendelee eti kwa sababu waliondika ni wazungu.

Who are they? Mpaka wakufanye uwaze na kuamini Kuwa kila walichokifanya / wanachokifanya ni dogma? Huhitaji kwenda BAKITA kujua kuwa lugha yetu haibadiliki kutoka KISWAHILI na kuwa Swahili hata ikiwa unaongea KIYUNANI!
 
Kwa hali hii tutazidi tengeneza Tanzania yenye vichwa vigumu kuelewa ili viongozi wetu wazidi kuiba na kuridhiana uongozi kwa watoto wao kwa sababu only few people will be compitate koz hao wanao

hivi sasa hawa somi hapa wala hawata soma hapa nchini so watakuwa na elimu bora kutuchaka chua sie tulio somea kataa kutokana na elimu duni inayo patikana kwenye shule zetu tutarudi kwenye ( Survival for the fittest) wenye nguvu wata peleka watoto wao shule nzr na nje ya nchni ss walala hoi tutabaki maids and servants wao.
 
Kikwete na kawambwa wameamua kumwachia rais anayekuja mtego, sijui kama atautegua!
 
Ninachojua building human capital needs strategic planning.

Hasa kutengeneneza proper infrastructures for implementation.

Sasa kwa hii sera tuliocopy (naweza sema) imepangwa yes, je ni mikakati ipi na lini walimu wa shule za msingi wamepewa workshops ili waweze kufundisha hadi kidato cha 4?

Kama pia issue ni kuwarudisha walimu wa diploma wafundishe primary, how willingly they are to cope the strategy?

Mara nyingi serikal yetu inafail kwenye mpango yake kwa sababu, mosi, imeshindindwa kuidentify the society needs(stakeholders), pili. Kuevaluate marketing system.

Tunaisubili utekelezaji wa hiyo project yao but it's useless.
 
Well, its a "lock in strategy". Tunajifungia ndani wakati hatuwezi kushindana kwenye "world Market", wakati huo huo hatuna fulsa za kututosha ndani ya nchi hii....!

Ni bahati mbaya/nzuri sana kwamba hao wanaoleta sera hii mpya ya Elimu, hakuna hata mmoja wao atakayempeleka mwanae katika shule za jumuiya.

Inapendeza sana kwani wengi wao either watoto wao na wajukuu wao tayari hawako mashuleni au wanasoma shule nje ya nchi, au wake zao tayari wamekwisha ingia kwenye kipindi cha "likizo" au "mapumziko" yaani "meno Pause" kiasi kwamba mfumo huu mpya hauwezi kuwaathiri moja kwa moja!!!

Naipenda sana nchi yangu ndo maana "navumilia kuwa Mtanzania"


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Kuna haja sasa ya kutafuta pesa ili kuwasomesha watoto kwa syllabus ya Cambridge. Hii ya kibongobongo imekosa mwelekeo sasa.
 
Hao wazungu wanatakiwa wajue kuwa lugha yetu ni "Kiswahili " na sio "Swahili " hata kama walikosea kuchapisha kama walivyokosea kuandika majina ya maeneo mbalimbali ya nchi yetu, hatuwezi kukubali hali kama hii iendelee eti kwa sababu waliondika ni wazungu. Who are they? Mpaka wakufanye uwaze na kuamini Kuwa kila walichokifanya / wanachokifanya ni dogma?
Huhitaji kwenda BAKITA kujua kuwa lugha yetu haibadiliki kutoka KISWAHILI na kuwa Swahili hata ikiwa unaongea KIYUNANI!


Ni lugha yao na Kiswahili kwa lugha yao ni "Swahili". Wewe amua upendavyo, Piga makelele, laani wazungu milele lakini haitabadilika. Itakuwa ile ile
"Swahili".

Na kwa nini sisi tunaita " Kiingereza" sio KiEnglish? Huwezi kuwapangia watu lugha unavyopenda wewe itamkwe vipi. Huu ni upuuzi.

Kubadili Majina ya miji ni uhuru wako. Wao wataita utakavyo wewe. Mbona Bombay sasa inaitwa mumbai, Burma inaitwa Mayanmar. Lakini hio "ki" haimo katika lugha ya Kiingereza na hata bakwata au Ikulu ikiamua vipi, kwa Kiingereza ni Swahili tu.

Pia, ukienda Japan, pengine utawaua kwa hasira . David inakuwa "dabito". Sasa wakikuita Dabito utalia pia? Ukibadilisha uraia na kuchukua wa kijapani, jina lako litakuwa Dabito kwa sababu lazima itamkwe kwa Katakana kwanza halafu ndio waandike kwa Kiingereza kwenye pasi yako. Sahau David.
 
David= unaitwa/ inaandikwa Debito, dabito au Deibiddo ukiwa Japan. Inategemea mwandishi anasikia vipi "David" katika sikio lake.
 
Mkuu labda uhoji content ya sera yenyewe kama blueprint ya Taifa katika elimu inakotaka kuelekea. Kwa maana kwamba sera huelezea nini serikali itafanya kwa muda flani.

Sera ikisha tungwa kwa namna moja au nyingine huathiri mfumo na sheria pia kanuni zilizopo. Hivyo kabla ya sera kutekelezwa kwa ukamilifu wake sheria fulani hufutwa, hurekebishwa au hutungwa mpya ili kukidhi matakwa ya sera mpya.

Tusubiri sheria zitakazo tungwa na bunge ambazo zitaonesha ni mwalim wa sifa zipi atatakiwa kufundisha elimu hii ya msingi iliyopanuliwa toka miaka saba hadi kumi.

Nadhani la muhim sana kwetu kwa sasa ni kuisoma sera hii ili ruwe na uhakika kwa kile tutakacho jadili. Sera yenyewe ndo ina page 68 tu!
 
MKWANO

Mkuu nikupe taarifa kidogo tu yawezekana hili hukulijua!

Mwalimu mwenye diploma ya ualimu anatakiwa kufundisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na pili tu, na wale wa shahada ya kwanza katika ualimu wanapaswa kwa sheria ya sasa wafundishe kidato cha tatu mpaka sita!

Kutokana na scarce ya walimu, walim wa diploma wanafundisha mpaka kidato cha nne!

Sera inapobadilika automatically baadhi ya sheria huathirika moja kwa moja. Naamini sheria zitaonesha ni nani afundishe katika ngazi ipi ya elimu!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nikupe taarifa kidogo tu yawezekana hili hukulijua!

Mwalimu mwenye diploma ya ualimu anatakiwa kufundisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na pili tu, na wale wa shahada ya kwanza katika ualimu wanapaswa kwa sheria ya sasa wafundishe kidato cha tatu mpaka sita!

Kutokana na scarce ya walimu, walim wa diploma wanafundisha mpaka kidato cha nne!

Sera inapobadilika automatically baadhi ya sheria huathirika moja kwa moja. Naamini sheria zitaonesha ni nani afundishe katika ngazi ipi ya elimu!

Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu, hofu yangu ni hizi shule za kata, kama primary ni hadi darasa la 10 (Ngumu kuitaja) ko hizi za kata zitakuwa Advance zote?

Nini intention ya serikal hasa? Wanataka niamini kwamba Elimu tuliyo nayo ni bora sana kiasi kwamba Wanataka tuwe bora zaidi? Je jamii imehusishwa? Au ni Order from the Top? Are we after skills or certificates?
 
Jamani nisaidieni kujibu yafuatayo maana haya mambo ya elimu si mjuzi sana:

1. Kwa mfumo huu mpya ina maana habari za form 5 na 6 - high school ya sasa haitakiwepo tena?

2. Je kwa mfumo huu mpya - ina maana hakutakuwa na kufail/ kushindwa shule tangu shule ya awali hadi sekondari?

3. Je hizi shule za sasa za sekondari kama Azania,Kantalamba,Kilakala, Umbwe, etc zitakuwa zinafundisha wanafunzi wa ngazi ipi?

5. Je universities, zitadahili wanafunzi wa ngazi ipi Katika shahada ya kwanza?maana tulizoea wenye elimu ya kidato cha sita au diploma ndio hujiunga huko.

Ni hayo tu.
 
MALALIKA

Hakuna kituvkinachoitwa shahada katika ualimu bali ni shahada ya elimu.

Then tunaomba muongozo wako wenyekuonesha kwamba mwalimu wa diploma anatakiwa kufundisha form one na two.
Then shahada afundishe three hadi six.

Tupatie ushahidi wa kudhibitisha kauli hiyo
 
Back
Top Bottom