Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mmmh. . . .
Na baada ya kupokea?Unaona kuna uhitaji wa kurudisha (na wewe kutoa zawadi)?
...khaa, SALE hapa mpaka boxing day bana...halafu mtu kajitutumua zawadi ya gharama halafu unanishauri nikamtafutie PRIMARK kizawadi cha sale? Lizzy usinifanye nionekane cheap bana, krismasi comes but once a year bana...ila mnh, bajeti na recession hii!...
Nitaipokea kwa mikono yote miwili na kwa moyo mkunjufu kabisa kwani kukataa zawadi si uungwana.
Mwenzio kukufikiria na kutumia muda wake kwenda kutafuta na hatimaye kuinunua hiyo zawadi si jambo dogo la kuletea masikhara.
Wewe unaonaje?
Sasa hapo itategemea. Itategemea na kama na mimi nami nimeshampa ya kwake. Kama nitakuwa nimeshampa kutakuwa hakuna haja tena ya mimi kurudisha maana nikifanya hivyo na yeye akifanya hivyo baada tena ya kupokea ya kwangu hatutamaliza kupeana hizo zawadi na itakuwa si kupeana zawadi tena bali utageuka kuwa ni mchezo na kupoteza kabisa maana.
Ila mimi kwa jinsi nilivyo, nikishampa mtu zawadi huwa sitegemei wala kutarajia kuwa na yeye atanipa zawadi. Huwa napata faraja ya kuridhisha kabisa pale nisikiapo 'akhsante Ngabu'.
....hayo maneno kuntu kabisa, nime ya bold, nimeyapaka rangi na kuyapigia msitari watu wayasome na kuyaelewa hapa, mtihani huu.
Fair enough.
Ila hiyo ya kupeana na kurudishiana mbona poa tu, kama ile ya kusindikizana mpaka jogoo anawika.We hutaki?
Sasa Mbu unataka nikwambie ujikwamua ufikie bei?
Hamna ulazima, zawadi sio lazima ilingane bei na uliyopewa wewe.We jikune mpaka pale mkono unapofika tu basi, muhimu tafuta kitu kizuri kitakachofurahisha nafsi bila kusahau ulimi/pua/masikio n.k
Sasa Mbu si na wewe unatumia muda wako kwenda dukani kumtafutia kitu kizuri?Hapo ulipopigia mstari bei haijawekwa kama kigezo hivyo sio muhimu sana, muhimu ni zawadi yenyewe.....hayo maneno kuntu kabisa, nime ya bold, nimeyapaka rangi na kuyapigia msitari watu wayasome na kuyaelewa hapa, mtihani huu.
...so Lizzy kwa ushauri wako unaniambia nitafute zawadi itayonifurahisha mimi nafsi yangu, sio yeye?
dahhh, nitakuwa kama sijamtendea haki aisee...au?
...hizi zawadi nyingine mtihani kutunukiwa...aarrgghhh!
Kwa nini nsitake? Lol
Sasa Mbu si na wewe unatumia muda wako kwenda dukani kumtafutia kitu kizuri?Hapo ulipopigia mstari bei haijawekwa kama kigezo hivyo sio muhimu sana, muhimu ni zawadi yenyewe.
Lolzzz. . .siumesema itapoteza maana?
Unaweza kuta ndo mnajenga maana!!
...Mkuu Mbu mtafutie kitu kama hiki wala si bei mbaya kabisa ππ
Hahahaha,kama yeye alivyochungulia?Lizzy sikiliza, watu tunafana lakini pia hatufanani. Kuna watu ukiwanunulia zawadi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuangalia kimetoka wapi halafu wanaenda kuchuguza bei.
Kwa hiyo mimi nauelewa kabisa mtihani alionao Mbu. Wewe unaweza usielewa kwa sababu ni mdada.
Una akili wewe!
....khaaaa....counterfeit ya mchina ee kaka....hahahah...!
Unajua kaka, huku ukubwani nimejifunza zawadi inakuwa kama deni vile,
yaani unapewa kitu lakini ujue utakilipia kwa namna moja au nyingine...
...huu mwiba kaka, nataka niuchomoe kabla ya wikiendi!
Lizzy sikiliza, watu tunafana lakini pia hatufanani. Kuna watu ukiwanunulia zawadi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuangalia kimetoka wapi halafu wanaenda kuchuguza bei.
Kwa hiyo mimi nauelewa kabisa mtihani alionao Mbu. Wewe unaweza usielewa kwa sababu ni mdada.
Basi tuanze kusindikizana bila kukoma, au tuzawadiane?Lolz
...aaahhh? siku hizi hakuna cha wa'wake wala wa'ume bana, ukipewa zawadi jua umetwishwa deni...!
yaani Lizzy utakubali upewe zawadi bure bure tu? hahaha....
...halafu kuna wengine akikupa zawadi siku ya valentine, unakumbushiwa kuilipa siku ya pasaka, siku ya iddi, na krismasi....! never ending aisee...