Mtihani, zawadi ya krismasi..!

Mtihani, zawadi ya krismasi..!

Mmmh. . . .
Na baada ya kupokea?Unaona kuna uhitaji wa kurudisha (na wewe kutoa zawadi)?

Sasa hapo itategemea. Itategemea na kama na mimi nami nimeshampa ya kwake. Kama nitakuwa nimeshampa kutakuwa hakuna haja tena ya mimi kurudisha maana nikifanya hivyo na yeye akifanya hivyo baada tena ya kupokea ya kwangu hatutamaliza kupeana hizo zawadi na itakuwa si kupeana zawadi tena bali utageuka kuwa ni mchezo na kupoteza kabisa maana.

Ila mimi kwa jinsi nilivyo, nikishampa mtu zawadi huwa sitegemei wala kutarajia kuwa na yeye atanipa zawadi. Huwa napata faraja ya kuridhisha kabisa pale nisikiapo 'akhsante Ngabu'.
 
...khaa, SALE hapa mpaka boxing day bana...halafu mtu kajitutumua zawadi ya gharama halafu unanishauri nikamtafutie PRIMARK kizawadi cha sale? Lizzy usinifanye nionekane cheap bana, krismasi comes but once a year bana...ila mnh, bajeti na recession hii!...

Sasa Mbu unataka nikwambie ujikwamua ufikie bei?
Hamna ulazima, zawadi sio lazima ilingane bei na uliyopewa wewe.We jikune mpaka pale mkono unapofika tu basi, muhimu tafuta kitu kizuri kitakachofurahisha nafsi bila kusahau ulimi/pua/masikio n.k
 
Nitaipokea kwa mikono yote miwili na kwa moyo mkunjufu kabisa kwani kukataa zawadi si uungwana.

Mwenzio kukufikiria na kutumia muda wake kwenda kutafuta na hatimaye kuinunua hiyo zawadi si jambo dogo la kuletea masikhara.

Wewe unaonaje?

....hayo maneno kuntu kabisa, nime ya bold, nimeyapaka rangi na kuyapigia msitari watu wayasome na kuyaelewa hapa, mtihani huu.
 
Sasa hapo itategemea. Itategemea na kama na mimi nami nimeshampa ya kwake. Kama nitakuwa nimeshampa kutakuwa hakuna haja tena ya mimi kurudisha maana nikifanya hivyo na yeye akifanya hivyo baada tena ya kupokea ya kwangu hatutamaliza kupeana hizo zawadi na itakuwa si kupeana zawadi tena bali utageuka kuwa ni mchezo na kupoteza kabisa maana.

Ila mimi kwa jinsi nilivyo, nikishampa mtu zawadi huwa sitegemei wala kutarajia kuwa na yeye atanipa zawadi. Huwa napata faraja ya kuridhisha kabisa pale nisikiapo 'akhsante Ngabu'.

Fair enough.

Ila hiyo ya kupeana na kurudishiana mbona poa tu, kama ile ya kusindikizana mpaka jogoo anawika.We hutaki?
 
....hayo maneno kuntu kabisa, nime ya bold, nimeyapaka rangi na kuyapigia msitari watu wayasome na kuyaelewa hapa, mtihani huu.

Kamanda, mimi naelewa fika kabisa mtihani ulio nao.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Sasa Mbu unataka nikwambie ujikwamua ufikie bei?
Hamna ulazima, zawadi sio lazima ilingane bei na uliyopewa wewe.We jikune mpaka pale mkono unapofika tu basi, muhimu tafuta kitu kizuri kitakachofurahisha nafsi bila kusahau ulimi/pua/masikio n.k

...so Lizzy kwa ushauri wako unaniambia nitafute zawadi itayonifurahisha mimi nafsi yangu, sio yeye?
dahhh, nitakuwa kama sijamtendea haki aisee...au?

...hizi zawadi nyingine mtihani kutunukiwa...aarrgghhh!
 
....hayo maneno kuntu kabisa, nime ya bold, nimeyapaka rangi na kuyapigia msitari watu wayasome na kuyaelewa hapa, mtihani huu.
Sasa Mbu si na wewe unatumia muda wako kwenda dukani kumtafutia kitu kizuri?Hapo ulipopigia mstari bei haijawekwa kama kigezo hivyo sio muhimu sana, muhimu ni zawadi yenyewe.
 
...Mkuu Mbu mtafutie kitu kama hiki wala si bei mbaya kabisa 🙂🙂

b_326she141198_0.jpg
 
...so Lizzy kwa ushauri wako unaniambia nitafute zawadi itayonifurahisha mimi nafsi yangu, sio yeye?
dahhh, nitakuwa kama sijamtendea haki aisee...au?

...hizi zawadi nyingine mtihani kutunukiwa...aarrgghhh!

Hahahahaha ufurahishe nafsi yako kwani ni zawadi yako Mbu?Labda kama angekua ndie SoulMate. . . . ila kwasababu sie inatakiwa uitafute ukiwa na furaha ya mwanadada mawazoni.
 
Sasa Mbu si na wewe unatumia muda wako kwenda dukani kumtafutia kitu kizuri?Hapo ulipopigia mstari bei haijawekwa kama kigezo hivyo sio muhimu sana, muhimu ni zawadi yenyewe.

Lizzy sikiliza, watu tunafana lakini pia hatufanani. Kuna watu ukiwanunulia zawadi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuangalia kimetoka wapi halafu wanaenda kuchuguza bei.

Kwa hiyo mimi nauelewa kabisa mtihani alionao Mbu. Wewe unaweza usielewe kwa sababu ni mdada.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...Mkuu Mbu mtafutie kitu kama hiki wala si bei mbaya kabisa 🙂🙂

b_326she141198_0.jpg

....khaaaa....counterfeit ya mchina ee kaka....hahahah...!

Unajua kaka, huku ukubwani nimejifunza zawadi inakuwa kama deni vile,
yaani unapewa kitu lakini ujue utakilipia kwa namna moja au nyingine...

...huu mwiba kaka, nataka niuchomoe kabla ya wikiendi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lizzy sikiliza, watu tunafana lakini pia hatufanani. Kuna watu ukiwanunulia zawadi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuangalia kimetoka wapi halafu wanaenda kuchuguza bei.

Kwa hiyo mimi nauelewa kabisa mtihani alionao Mbu. Wewe unaweza usielewa kwa sababu ni mdada.
Hahahaha,kama yeye alivyochungulia?
Sasa mtu utafanyaje?Ubaki na wallet isiyo na kitu kisa unaogopa mwenzio akienda kuchunguza bei?

Hapo ndipo zawadi inapopoteza maana, mtu anapotoa zaidi ya alicho tayari kutoa!!
 
....khaaaa....counterfeit ya mchina ee kaka....hahahah...!

Unajua kaka, huku ukubwani nimejifunza zawadi inakuwa kama deni vile,
yaani unapewa kitu lakini ujue utakilipia kwa namna moja au nyingine...

...huu mwiba kaka, nataka niuchomoe kabla ya wikiendi!

...Kila la heri Mkuu mie nimeshamaliza "kulipa deni" la zawadi nilizozipata 🙂🙂....Si unajua vya mchina bei poa kabisa 🙂🙂...Siku ndiyo zinayoyoma hivyo Mkuu na kesho na kesho kutwa umati utakaokutana nao katika shopping za "lala salama" unaweza kujuta.
 
Lizzy sikiliza, watu tunafana lakini pia hatufanani. Kuna watu ukiwanunulia zawadi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuangalia kimetoka wapi halafu wanaenda kuchuguza bei.

Kwa hiyo mimi nauelewa kabisa mtihani alionao Mbu. Wewe unaweza usielewa kwa sababu ni mdada.

...aaahhh? siku hizi hakuna cha wa'wake wala wa'ume bana, ukipewa zawadi jua umetwishwa deni...!
yaani Lizzy utakubali upewe zawadi bure bure tu? hahaha....

...halafu kuna wengine akikupa zawadi siku ya valentine, unakumbushiwa kuilipa siku ya pasaka, siku ya iddi, na krismasi....! never ending aisee...
 
Basi tuanze kusindikizana bila kukoma, au tuzawadiane?Lolz

Hiyo ya kusindikizana pasipo kikomo imenikumbusha mbali sana...enzi za sekondari. Kuna mshikaji alikuwa anafukuzia (sitasema lile jina usolipenda la d...mu) msichana flani hivi.

Walikuwa kila wakitoka twisheni wanasindikizana...wakifika kwa mmoja yule aliyefika kwao anamsindikiza tena mwenzake....lol.
 
...aaahhh? siku hizi hakuna cha wa'wake wala wa'ume bana, ukipewa zawadi jua umetwishwa deni...!
yaani Lizzy utakubali upewe zawadi bure bure tu? hahaha....

...halafu kuna wengine akikupa zawadi siku ya valentine, unakumbushiwa kuilipa siku ya pasaka, siku ya iddi, na krismasi....! never ending aisee...

Sasa kuna wale ambao usipowapa zawadi (wakati wao walikupa) watamwambia kila wamjuaye. Yaani haya mazawadi wakati mwingine yanakuwa pasua kichwa.

Sasa kamanda uliweza kweli kulala kwa utulivu?
 
Back
Top Bottom