Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

Mtikila yupo sawa kabisa, tusitegemee maajabu kwenye bunge la katiba
 
Bora yeye aliyekuwa hapo bungeni kwani ameshuhudia
uozo uliomo hapo na bora amesema lililo moyoini mwake
maana bunge la katiba limechaguliwa kiurafiki wewe
unafikiri yatatoka mambo ya aina gani hapo kama sio
kiurafiki rafiki na kuwekeweana kulindana hapo


Mchungaji Mtikila leo huyu jamaa amekandia bunge lote la katiba na kusema anasikitka soon atalicha bunge hilo mana limechaguliwa kihuni.Nasema hivi wambieni kabsa nimesema hili ni bunge la kihuni limechaguliwa kihuni ndio maana unakutana na mambo ya kishenzi mnayoendelea kuyaona.

Nasema tangia uhuru sijapata kuona bunge la kihuni kama hili.Sitoshangaa maamuzi ya kihuni na kishenzi kutokea siku tunaagana pale nje.Huyo ni rev. Christopher Mtikila.

Source: BBC swahili
 
Na yeye pia ni Muhuni na mshenzi maana yeye pia ni sehemu ya waliochaguliwa kushiriki bunge hili
 
Kama wajumbe wa hilo bunge ni wahuni na washenzi basi ina maana na yeye mwenyewe ni mhuni na mshenzi.
 
Watu wengi huwa wanamuona mtikila kichaa lakini tunaomwelewa tunaona ni mzalendo Wa kweli. Binadamu si mkamilifu. Yapo machache anakosea ila maoni yake mengi ni excellent. Mfano alitetea mgombea binafsi mpaka mahakani watu wakamuona kichao Leo hii kila mmoja anataka haki ya mgombea binafsi. Amekua akidai nchi ya Tanganyika watu wakamwona mjinga leo hii ni swala lililo kwenye rasimu. Amepinga rushwa na takrima kwa kipindi Fulani ilipokuwa imebarikiwa wakati Wa mkapa watu wakamcheka wewee muda si mrefu baadae takrima ilifutwa. Etc etc kuna mengi sana huyu mh anafanya yakupongeza
 
Kama wabunge wote wa bunge la katiba ni wahuni basi hata yeye ni mhuni na ndio maana amechaguliwa kujiunga na machizi wenzake

Huyu ni mjanja aliyegundua kuwa yupo na wahuni, na ndo maana katoka mapema kujichanganua na wahuni
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Hajasema anaikubali chama chake, kasema anamkubali Mtikila, lkn pia wingi wa wanachama siyo sababu ya kutoikubali chama kama kiko makini, ukumbe hata hivyo vyama vyenye wanachama wengi ni mkusanyiko wa mwanachama mmoja mmoja.
 
Mabadiliko huletwa na watu wachache, muogope sana mtu anayekuwa na msimamo wake pamoja na wingi wa wapinzani wake.
 
Chadema na Sisiemu linapokuja suala la posho ni kweli lao ni moja.Mtikila ni jasiri na wala siyo mwoga.namtegemea sana kwenye bunge hili la katiba.
 
namkumbuka huyu rev. Mtikila katika miaka ya tisini alikuwa anadai katiba na tanganyika irudishwe, watu wengi walidhania ni chizi kutokana na lugha yake. Leo yale mawazo yake ndiyo yanapiganiwa na wengi. Huyu jamaa huwa ni mtaifa sana, ila bahati mbaya watu wengi hawamuelewi. Nakumbuka alishaipeleka serikali mahakamani akidai mgombea binafsi, alivyoshinda ile kesi pinda akampotezea. Leo hii tunapigania mgombea binafsi.

.ningeboreka sana kama mtikila angekosa bunge hili. Hii ni sehemu tuu ya viburudisho kaeni mkao wa kula wiki ijayo ataachia santuri mpya ya tanganyika atakaye mpinga subiri uone mlipuko
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Acha ufyatu wewe wanachama 150 watabaki kuwa wanachama na ukweli utabaki kuwa ukweli. Watu 150 mbona wengi sana coz siku zote mapinduzi huanzia kwa mtu mmoja tu. Hakuna himaya iliyodumu zaidi ya zama zake katika historia ya dunia.
 
Nakukubali sana Mtikila.

Tukipata watu 8 kama wewe tunaibomoa sisiem.
 
Haha Watanzania pamoja na wewe wagumu kulewa, tunajadili katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Zanzibar wanakuja na katiba yao, ya tanganyika hiko wapi? hili tujadili zote mbili tupate moja kamili, Watanzania wengi ni washabiki tuu si cdm wala ccm, na ndo maana unaoNa Mtikila Hana washabiki wengi wala wafuasi, hila wapo wachache wanaomkubali, hajawaia hata siku moja kushindwa kesi zidi ya serikali why tusimkubali?
 
Maneno ya Mtikila ni makali kidogo.Lakini ukweli unabaki pale pale wajumbe kudai fedha zaidi za posho ni kuwasaliti watanzania wa kawaida.
 
Back
Top Bottom