Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Wenzetu wenye maarifa zaidi yetu huwa hawabomoi bali hutenga eneo jipya na kujenga majengo mengine kupanıua hospitali.Kumeingia mtindo mpya wa kujitafutia miradi. Sasa mkurugenzi wa Muhimbili anataka kuanzisha mradi wa upigaji eti Muhimbili ibomolewe na kujegwa upya wakati kuna vijana hawana hata mabweni ya kulala.
Kwani kuna tatizo gani ya maeneo ya kujenga mpaka wakabomoe hospitali! Kwanini basi pasibakie kufanywa chuo cha afya na waongeze wanafunzi kwenye sehemu nyingine muhimu! Wenzetu wana hospital mpaka za makontena eti sisi tunalalamika majengo ni ya kizamani! Wakati tunategemea misaada kwenye dawa na chanjo.
Mtindo huu vilevile upo kwenye viwanja vya mpira na Zanzibar nako wanafanya haya.
View attachment 2714027
Ukitembea nchi hizo wanatupatia hiyo mikopo utaona hospitali nyingi kubwa zimepanuliwa na huku majengo ya zamani yakibaki palepale.