Mtindo mpya wa trafiki kula rushwa (picha)

Mtindo mpya wa trafiki kula rushwa (picha)

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Pichani ni kaka mtanashati anayejifanya muuza magazeti, hapa ni mataa ya Morocco (Kinondoni) daladala zinazotoka maeneo ya Shoppers/Kawe/Msasani zinasimamishwa na Askari kisha kondakta anashuka na kumalizana na na huyo kaka muuza magazeti.

Mheshimiwa alisema watoa taarifa tutalindwa hivyo sitegemei vitisho wala uzi huu kufutwa. Picha ya kwanza amenyoosha mkono juu kupeana ishara na Askari ambao wako upande wa mpiga picha. Picha ya pili anapanga fedha alizoweka katikati ya gazeti

2A7709F8-4170-4F72-B9CF-12534529382B.jpeg

26DD0FAE-F0B2-4FCA-BE05-B718D94453FA.jpeg

A1F8A625-414E-4AE0-80F8-B33F323A6EE8.jpeg

7DBCDA84-63E8-4779-8539-0974DC6192C4.png
 
Pia pale veta Chang'ombe yupo jamaa mwengine kama huyo. Nae anauza magazeti. Ndo anachukua pesa ya mabao kutoka kwa makonda wa daladala.
 
...Ubunifu😀😀,sasa huyo jamaa na yeye anapiga panga kimtindo maisha yanasonga...
 
Mi naona mapichapicha tu, huyo kondakta aliyeshuka na hela yuko wapi? mijitu mingine mna roho mbaya hata pa kuanzia hamjui!! we kwako ni msafi sana? waacheni wapate ya kiwi
Sina hakika kama ni kweli.Ila kama ni kweli si kitu kizuri cha kushabikia. Imagine trafiki ameruhusu Dereva wa gari la abiria ambaye amelewa chakali kwa kupewa elfu mbili, halafu dereva akaingiza gari baharini, unadhani hiyo kiwi unayoipigia debe itakuwa na thamani kuliko roho za watu?
 
Njoo njia ya Mbezi - Goba asubuhi ushuhudie jinsi wanavyozikusanya shs 1500/- kwa kila daladala. Kuna sehemu pana msikiti wanapaita kwa Ulomi. Yaani mpaka raha. Daladala inapigwa mkono, konda anashuka fasta kashika buku abiria mnaona, kisha anarudi fasta. KAMA UNATAKA KUONA KONDAKTA ANASALIMIANA KWA VIGANJA NA TRAFIKI NJOO HUKU. HAWAOGOPI UVIKO-19
 
Tuache unafiki hakuna dereva asiyetoa kitu kidogo kwa traffic endapo anakutwa na kosa.
Hapa tunashadadia kisa tupo mtandaoni.
 
Njoo njia ya Mbezi - Goba asubuhi ushuhudie jinsi wanavyozikusanya shs 1500/- kwa kila daladala. Kuna sehemu pana msikiti wanapaita kwa Ulomi. Yaani mpaka raha. Daladala inapigwa mkono, konda anashuka fasta kashika buku abiria mnaona, kisha anarudi fasta. KAMA UNATAKA KUONA KONDAKTA ANASALIMIANA KWA VIGANJA NA TRAFIKI NJOO HUKU. HAWAOGOPI UVIKO-19
Kitaa changu hiki dar
 
Kinacho sikitisha zaidi yale mabwanyenye ya kwenye ile taasisi yakuzuia mlungula yame jazana ofisi yakisubiri yapelekewe taarifa kama hizi, huku yakiwa ubunifu na weledi wa kupambana na mlungula....
 
Back
Top Bottom