Mtindo wa kuita miundombinu majina ya watu binafsi pamoja na maraisi ukomeshwe, unaleta kutukuza watu isivyostahili wanapotimiza wajibu wao

Nili shangaa hilo Daraja kuli ita Mfugale (mita 300 tu) na vibao vyake vipo. Wakati hilo ni Daraja la kawaida tu wala siyo Fly over wala siyo Express Road.
Tembelea majirani zetu Kenya. Hivyo ni vitu vya kawaida. Fly over zao zina run 2KM to 10Km.

Pia @TANROADS tuna omba muendeleze utamaduni wa kuandika majina ya Vijiji au Mitaa barabarani. Ina pendeza kwa utalii. Siyo kusumbua kuuliza uliza watu kwenye gari.

Shule zote, madaraja, Majengo, nk majina yake yawe ya eneo husika kutunza Historia ya maeneo. Siyo eti LUKUVI, TULIA, akati mchango wao ktk nchi una zidiwa na Mwl wa Primary aliye staafu kwa Heshima.
 
Baraka zake Mungu baba mwenyezi, Baba, Mwana na Roho mtakatifu, zikae nawe mleta mada daima na milele. Amina.
Hee Mkuu, sistahli hayo kwa maoni kidogo kama haya. Napaswa kuwajibika zaidi kupata mtazamo wako kama huu ulio very positive. Hata hivyo asante sana.
 
Tunahitaji hili lifikishwe Bungeni, maana linazidi kupamba moto sasa imekuwa vurugu. Nasikia majina ya mitaa watu hata walitoa fedha ili mitaa iitwe kwa majina yao. Yaani kuna ufisadi mkubwa umefanyka kwenye kutoa majina ya mitaa kwenye huu mradi wa anuani za makazi. Ujinga mwingine huu wa watu kupenda kutukuzwa
 
Kwenye suala la anuani za makazi, ikiwa mtaa wako umepewa jina la mtu fulani bila vigezo vinavyoeleweka hebu tutaarifu hapa pia. Kuna watu nasikia walikuwa wakitoa fedha mitaa iitwe kwa majina yao
 
USA kuna uwanja wa ndege unaitwa JFK, jina la rais wao aliyeuwawa mwaka 1963.

Senegal wana uwanja mkubwa wa mpira unaitwa Leopold Senghor ni wa miaka na miaka.

Huwezi kukwepa kuipa mitaa au barabara majina ya watu maarufu, jitahidi ulitazame suala hili kwa mtazamo chanya utaelewa kwa kina kwanini majina yanatumika katika kutambulisha vitu vyenye umuhimu.
 
Wanapopenda kutukuzwa wewe binafsi unapungukiwa na nini?. Maisha haya ni mafupi sana na hakuna ajuaye ataondoka lini juu ya uso wa dunia.
 
Mkuu acha kunisikitisha. Tunafanya hivi kwa kuwa USA, Senegal na kwingineko wanafanya hivi, ndio sababu? Kwa nini tunakataa ushoga basi, ambao USA, Canada, nk nk wanafanya?

Yaani kama nchi hatuwezi kuwa na msimamo wetu ili kina USA na Senegal watuige?

Ila nimedokeza, majina ya kikoloni tuyaache. Ila tusiendeleze hii tabia.
 
Bora wawe wanaweka majina yale ya eneo husika na kwa mbali majina ya viongozi wanaopendwa na watz wote kama magufuli.
 
Magufuli alikaa madarakani kwa miaka 5 tu ila ana karibia vitu 10 tayari vina majina yake

Kuna daraja linaitwa Magufuli huko Morogoro, Stendi ya Magufuli, kuna mji wa Serikali unaitwa Magufuli City, kuns kivuko cha Busisi nacho wanakiita Magufuli
Angeendelea kuwepo hata jina la nchi lingebadilishwa na kitwa Jamuhuri ya Magufuli, mwanzili wa hiyo kampeni angekuwa Job Ndugai pale mjengoni na meza zingegongwa kwa kusindikizwa na nderemo, vifijo na vigeregere.
 
Vitu vinafanywa na watu na ndio wamiliki wa hayo majina. Usilitazame hili suala kwa mtazamo wa kisiasa wa ndani ya TZ, litazame kidunia. Ushoga na suala la majina ni vitu viwili tofauti kabisa.

Majina yanapokuwa hai maana yake hata maarifa ya wenye majina yanaendelea kuwa hai, Einstein mpaka leo hii ni mwanasayansi aliyegundua formula nyingi tu, kuna ubaya gani eneo fulani au barabara fulani ikapewa jina lake katika kumuenzi?.

Barack Obama ni rais wa kwanza mweusi kuiongoza USA kuna ubaya gani watanzania watakaokuja kuishi miaka ya 2035-45 wakaendelea kumtambua kila wanapopita pale mbele ya ikulu, kwamba alikuwepo mtu anaitwa Obama na akaongoza Marekani?.

Injinia aliyejenga flyover ya kwanza nchini, kuna ubaya gani akaendelea kuheshimika kwa aliyoyafanya kupitia jina lake?. Punguza hizi siasa nyingi jikite kwenye uzalendo.
 
Hata ile fly over ya John Kijazi ibadilishwe, iitwe Mkwawa flyover kutambua mchango wake wa kupambana na Wakoloni
Kwanini iitwe Mkwawa kwani Dar haikuwa na machifu wake wa kiazararamo na Kikwere????!!! Mara mia ingeitwa Kikwete flyover kidoooooogo ingeleta maana, au unaonaje
 
Wanapopenda kutukuzwa wewe binafsi unapungukiwa na nini?. Maisha haya ni mafupi sana na hakuna ajuaye ataondoka lini juu ya uso wa dunia.
Mkuu, watu wenye maswali kama haya ni mzigo katika jamii. Kama yeye amebaka mtoto wewe unapungukiwa ninii? Siku moja utaniambia kama mke wangu amebakwa wewe unapungukiwa nini?
 
Injinia aliyejenga flyover ya kwanza nchini, kuna ubaya gani akaendelea kuheshimika kwa aliyoyafanya kupitia jina lake?. Punguza hizi siasa nyingi jikite kwenye uzalendo.
Hee, vipi tukimuita mke wako Mrs wa jina la mwanaume wa kwanza alietembea nae, si lojiki hiyohiyo?
 
Hiyo ya Mfugale mi ndo iliniacha hoi
Mfugale anastahiki,kasanifu na kusimamia madaraja zaidi ya buku nchini..nyerere aliyepewa uhuru na wazungu vitu kila Kona anapewa yeye,akina mkwawa,milambo,kinjekitile,isike,abushiri,kheri,Sykes nk hawapewi chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…