Mtoto abakwa hadi kufa Mbagala, Mwili watupwa kwenye pagala

Mtoto abakwa hadi kufa Mbagala, Mwili watupwa kwenye pagala

Mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano umekutwa umetupwa kwenye pagala lililo Mbagala Kichemchem, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa watu walioushuhudia mwili huo kwenye pagala hilo, mwili huo una viashiria vya mtoto huyo kubakwa kisha mwili huo kutelekezwa kwenye pagala hilo.

Soma Pia: Mbeya: Mtoto wa darasa la nne shule ya msingi Mkapa alawitiwa na mwenzie wa darasa la saba

Chanzo: Azam TV
NGUVU ZILIZOTUMIKA MBEYA ZINGETUMIKA KATIKA KUKABILIANA NA WAHALIFU WA MATUKIO HAYA TUNGEKUWA MBALI
 
Why Mbagala ?, sijawahi kusikia mambo haya Masaki, Upanga ama sehemu kama hizo.

Umaskini ni chanzo cha maovi haya. Vitoto vya miaka 3 hadi 12 vinatembea tembea hovyo hovyo hadi saa tatu ama nne usiku - Mzazi mmoja yupo bar ama kijiwe cha kahawa huku mwingime anauza samaki gengeni.
 
Kinachotisha ni kwamba, ukifikiria tunawezaje kuzuia haya matukio unakosa majibu.
Tutazuia vipi ilhali waliopewa dhamana wanabariki haya matukio, kuna binti umri wa miaka 7 alibakwa na kulawitiwa huko kiwalani wiki 3 zilizopita na polisi buguruni ndo walikuwa mstari wa mbele kusaidia mtuhumiwa na wazazi wake namna ya kukwepa mkono wa sheria na ikibidi kesi iwageukie wazazi wa binti, hii serikali mfu imeoza hata funza hawaitamani tena
 
Back
Top Bottom