Hili ni tukio la ajabu na kweli lililofanyika huko Congo miaka kadhaa iliyopita.
Ilikuwa hivi: Mtoto mdogo aliumwa na nyoka mwenye sumu kali, akakata pumzi. Hakupumua kwa takriban masaa matatu. Kisayansi mtu asipopumua kwa muda huo mrefu, anapaswa kufa au kupata uharibifu mkubwa wa ubongo.
Mama yake alimbeba mtoto huyo hadi kwa Mhubiri wa Injili. Mhubiri akamuombea kwa Jina la Yesu. Ghafla mtoto akaanza kupumua tena. Hakupata madhara yoyote ya ubongo. Alikua mzima hadi akawa Mchungaji baadaye!
Hakika “Yesu Kristo ni yeye yule jana, na leo, na hata milele.” (Waebrania 13:8). Yesu alifanya miujiza mingi zamani, na hata sasa bado anaendelea kufanya kwa wote waaminio.
Source: Christianity Today
Sasa hivi sehemu ya ulimwengu umemuacha Mungu na kukimbilia kwenye Miujiza na ndio sababu kila kukicha Makanisa yana anzishwa na watenda miujiza...
Wale wachungaji wasomi, wanaofundisha neno la Mungu siku hizi nafasi yao ni ndogo kwani watu; wanakimbilia kwa wale ...walio pata maarifa ya kutenda miujiza kwa namna yeyote ile....
Ndio sababu Rwanda imefunga makanisha takriban 4000 ya ubabaishaji...
Hivi umewahi kujiuliza; Mbona viwete wakikombolewa hakuna hata mmoja anayetambulika kwenye eneo husika? wote wanakuwa ni watoka mbali???
Au hao watenda Miujiza kwanini wasiende pale Muhimbili (Moi), wagojwa wamejaa wengi tu wana mwamini Yesu; wakawaombea wakapona viungo vyao? wanakuja huku mtaani kuponyesha watu wasiofahamika kwenye eneo husika???