Mtoto aliyefariki, arudishiwa uhai baada ya kuombewa!

Mtoto aliyefariki, arudishiwa uhai baada ya kuombewa!

Suala la watumishi kutokubalika makwao sio la msingi.....
Kwa sababu, wanaokuja kuhubiri huku mjini kwetu Sumbawanga na viunga vyake sio wenyeji wa mjini kwetu.
Nimehudhuria kwenye mikutano/makongamano kadhaa na kuona viwete wakiponywa wengi tu.....ILA cha ajabu; hakuna pahala nimeenda wenyeji wakawa wanamfaham hata kiwete mmoja aliyeponywa.....
KWA NINI WAHUBIRI WENYE NGUVU YA UPONYAJI HAWAENDI KUWAHUBIRIA WAGONJWA MAHOSPITALI NA KUWAPONYA AMBAO NDIO WENYE UHITAJI MKUBWA KULIKO WATU WALIOKO MTAANI???
Rafiki, unayoyaona huko Sumbawanga, hayawakilishi mambo yanayofanyika dunia nzima. Ndio sababu Waswahili walisema: "Tembea Uone." Ukikaa sehemu moja tu unaweza kufikiri dunia yote iko hivyohivyo. Kuna wahubiri wengi wanaoenda mahospitalini kuwahubiri wagonjwa. Na wagonjwa wenye imani wanapona wanaposikia mahubiri hayo. Kama hujawaona huko, haimaanishi kuwa hawaendi. Zipo pia ministries ambazo pamoja na kuhubiri Injili zimeanzisha kabisa hospitali. Mtu anatibiwa kwa dawa za kawaida lakini pia anafanyiwa maombi/sala
 
Hili ni tukio la ajabu na kweli lililofanyika huko Congo miaka kadhaa iliyopita.

Ilikuwa hivi: Mtoto mdogo aliumwa na nyoka mwenye sumu kali, akakata pumzi. Hakupumua kwa takriban masaa matatu. Kisayansi mtu asipopumua kwa muda huo mrefu, anapaswa kufa au kupata uharibifu mkubwa wa ubongo.

Mama yake alimbeba mtoto huyo hadi kwa Mhubiri wa Injili. Mhubiri akamuombea kwa Jina la Yesu. Ghafla mtoto akaanza kupumua tena. Hakupata madhara yoyote ya ubongo. Alikua mzima hadi akawa Mchungaji baadaye!

Hakika “Yesu Kristo ni yeye yule jana, na leo, na hata milele.” (Waebrania 13:8). Yesu alifanya miujiza mingi zamani, na hata sasa bado anaendelea kufanya kwa wote waaminio.

Source: Christianity Today

Biblia inasema: “Watatokea manabii wa uongo… watafanya ishara na maajabu” (Mathayo 24:24) . Hivyo hata Biblia yako inasema: miujiza peke yake si uthibitisho wa ukweli.

Bwana Yesu alisema: “Wengi wataniambia… tulifanya miujiza kwa jina lako… nami nitawaambia sikuwajua” (Mathayo 7:22-23)

Hapa wazi: inaonyesha kuwa kufanya miujiza si kuwa kwenye ukweli.

Hadithi yako haina uthibitisho :​

Haina: rekodi ya hospitali wala ushahidi wa kitabibu wala uthibitisho huru. Ni simulizi tu . Imani ya kweli haihitaji hadithi zisizothibitishwa.​

Kama unategemea hadithi za miujiza kuthibitisha imani yako, basi msingi wako ni dhaifu sana.

Miujiza inayosimuliwa bila ushahidi inaweza kusisimua lakini haiwezi kuthibitisha kwamba unachokiamini ni kweli.
 
Hili ni tukio la ajabu na kweli lililofanyika huko Congo miaka kadhaa iliyopita.

Ilikuwa hivi: Mtoto mdogo aliumwa na nyoka mwenye sumu kali, akakata pumzi. Hakupumua kwa takriban masaa matatu. Kisayansi mtu asipopumua kwa muda huo mrefu, anapaswa kufa au kupata uharibifu mkubwa wa ubongo.

Mama yake alimbeba mtoto huyo hadi kwa Mhubiri wa Injili. Mhubiri akamuombea kwa Jina la Yesu. Ghafla mtoto akaanza kupumua tena. Hakupata madhara yoyote ya ubongo. Alikua mzima hadi akawa Mchungaji baadaye!

Hakika “Yesu Kristo ni yeye yule jana, na leo, na hata milele.” (Waebrania 13:8). Yesu alifanya miujiza mingi zamani, na hata sasa bado anaendelea kufanya kwa wote waaminio.

Source: Christianity Today

View: https://www.youtube.com/watch?v=9g6TSmtK6Ec
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=PSYYmUos_ZU
 
"...kwa Mungu yote yanawezekana.” (Mathayo 19:26)

Yesu alisema: “Mimi ndimi ufufuo na uzima…” (Yohana 11:25)

Hivyo ndugu yangu, kama una jambo linalokusumbua, mkimbilie Yesu sasa, anaweza kukutendea muujiza.(Marko 5:36). Ameahidi hivyo katika Yohana 14:13 akisema: “Lolote mtakaloliomba kwa jina langu, hilo nitalifanya…”

Unachofanya hapa ni kuchukua aya chache na kuzipotosha ili zionekane Yesu ndiye Mungu lakini Biblia yako inakupinga .”

“Kwa Mungu yote yanawezekana” lakini Yesu si Mungu​

Aya yako (Mathayo 19:26) inasema kwa Mungu, si “kwa Yesu”. Na Yesu mwenyewe anasema: “Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu uliyemtuma” (Yohana 17:3). Hapa ni wazi: Mungu ni mwingine na Yesu ni aliyetumwa
Kwa nini unamchanganya aliyemtuma na aliyetumwa???????????

“Mimi ndimi ufufuo na uzima” haimaanishi yeye ni Mungu​

Yesu pia alisema: “Siwezi kufanya neno lolote kwa nafsi yangu” (Yohana 5:30). Sasa huyo anayesema hana uwezo binafsi ndiye Mungu? Hapo hoja yako inavunjika moja kwa moja.

Kuhusu kuomba kwa jina la Yesu​

“Lolote mtakaloliomba kwa jina langu…” (Yohana 14:13) Hapo si kusema Yesu ndiye Mungu bali ni mamlaka aliyopewa , Kwa sababu Biblia inasema: “Amepewa mamlaka…” (Mathayo 28:18) . Aliyepewa mamlaka si sawa na mwenye mamlaka kwa asili (Mungu)

Yesu mwenyewe ana Mungu juu yake​

“Mungu wangu na Mungu wenu” (Yohana 20:17), Hata baada ya kufufuka bado anasema hivyo . Mungu hawezi kuwa na Mungu juu yake hili hulijibu kila mara lakini unalikwepa.

Unachofanya ni kuchagua aya zinazokuvutia na kupuuza zile zinazobomoa hoja yako.

Aya zako hazithibitishi Yesu ni Mungu zinathibitisha kuwa ni mjumbe aliyepewa mamlaka na Mungu.

USIPOTOSHE WATU TAFADHALI
 
Back
Top Bottom