Mtoto aliyefariki, arudishiwa uhai baada ya kuombewa!


Sasa hivi sehemu ya ulimwengu umemuacha Mungu na kukimbilia kwenye Miujiza na ndio sababu kila kukicha Makanisa yana anzishwa na watenda miujiza...
Wale wachungaji wasomi, wanaofundisha neno la Mungu siku hizi nafasi yao ni ndogo kwani watu; wanakimbilia kwa wale ...walio pata maarifa ya kutenda miujiza kwa namna yeyote ile....
Ndio sababu Rwanda imefunga makanisha takriban 4000 ya ubabaishaji...
Hivi umewahi kujiuliza; Mbona viwete wakikombolewa hakuna hata mmoja anayetambulika kwenye eneo husika? wote wanakuwa ni watoka mbali???
Au hao watenda Miujiza kwanini wasiende pale Muhimbili (Moi), wagojwa wamejaa wengi tu wana mwamini Yesu; wakawaombea wakapona viungo vyao? wanakuja huku mtaani kuponyesha watu wasiofahamika kwenye eneo husika???
 
Mliosoma Neuroscience, mpooo? Mbona kimya?
As per clinical neuroscience or neurocritical care, oxygen deprivation in the body is referred to as hypoxia. Within approximately 3–5 minutes of oxygen deprivation, neuronal injury begins to occur.
Between 5–10 minutes, there is a high risk of severe and irreversible brain damage or death.
Beyond this period, survival without significant neurological impairment is extremely unlikely.
 
Hahaa. Anatafuta mke, au wewe ndio unamtafutia?
Mwambie apige magoti aombe kwa BWANA. Mke mwenye busara hatafutwi mitandaoni.
Mithali 19:14

Halafu unamdhalilisha kweli. Unasema kana kanisa...kanatafuta...
Kana kanisa maana yake kaigizaji kapokapo.. nitapeli kama huyo mfufuaji uliemleta
 
Usiiite chai habari ya kweli. Badala yake tulia, usome kwa makini mistari inayoambatana na habari hiyo, ujifunze nguvu na uwezo wa Mungu wa kufufua wafu. Si umekiri mwenyewe kwamba JF ni kama darasa kwako? Keep learning
Yaani ni keep learning upuuzi na uongo.. Africa tutaendelea baki daima kwa akili kama zako..
Watu wapo wanakesha wakifanya tafiti ngumu na nzito zakumsaidia mwanadamu..
Viazi mnakuja na stori za kufufuana, huyo mchungaji wenu si mumpeleke mochwari
 
Duh, bado tu kuna watu hawajui tofauti ya dini na Injili?! Kazi kwelikweli

Hivi umewahi kujiuliza; Mbona viwete wakikombolewa kwenye hiyo mikutano ya watenda miujiza hakuna hata mmoja anayetambulika kwenye eneo husika? wote wanakuwa ni watoka mbali???
Kama ulikuwa hujui; tafuta kama kuna mkutano wowote ambapo kiwete anayetambulika mtaani aliponywa?
 
Ndugu yangu Shytown
Dunia hii sio kijiji kama wengi wanavyosema. Tembelea nchi mbalimbali katika makanisa yaliyojaa nguvu ya Mungu, utakutana na miujiza ya kweli. Hilo unalolisema lipo kwa sababu iliishatabiriwa kuwa siku za mwisho watatokea manabii wa uongo na watu wanaofanya miujiza feki. Hata hivyo, miujiza ya kweli ipo, ila huwezi kuiona kama unakaa sehemu moja tu.
 
OK, sijui kama nimekuelewa. Maandiko yanasema katika Mathayo 13:57
"Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”

Hiyo maana yake ni kwamba mara nyingi Mtumishi wa Mungu hatambuliwi thamani yake na watu wake wa karibu. Hivyo inawezekana kabisa watu kutoka mbali ndio wanaopokea miujiza kwenye mkutano, kwa sababu walisikia habari za Mtumishi huyo wakamkubali, na kwenda kwake kuombewa, na kwa imani yao wakapata uponyaji/ukombozi. Wale wanaoishi karibu naye kwa sababu wanamfahamu, wanampuuza, hivyo hawawezi kupokea miujiza. Miujiza haifanyiki mtu asipokuwa na imani.

Hata Yesu kuna mahali alienda lakini hakuwaponya watu wengi kwa sababu hawakumwamini (Mathayo 13:58). Walikuwa wanamdharau na kusema; "Huyu si mwana wa yule seremala?" (Mathayo 13:55).
 
Wewe una miaka mingapi? Labda tuanzie hapo. Nimekuuliza hivyo kwa sababu kama wewe ni wa mwaka 2000 inawezekana kabisa kuna wahubiri wengine ambao hawapo duniani leo, hukuwahi kuwasikia wala kuona matendo ya miujiza waliyofanya. Mimi nimeshuhudia viwete wengi tu walioponywa na wenyeji wanawafahamu wazi watu hao walioponywa.

Ila nisisitize tena, nyakati hizi ni nyakati za mwisho. Kuna manabii wengi wa uongo kama ilivyotabiriwa. Hawa manabii wa uongo, wanaweza kusema wanatenda miujiza lakini ni miujiza feki. Hivyo inawezekana kabisa wakaja na watu wao waliojifanya viwete halafu baada ya kuombewa wakajifanya wamepona.

Lakini nimesema pia kwamba mara nyingi Watumishi wa kweli wa Mungu huwa hawakubaliki katika maeneo yao. Hivyo inawezekana kabisa wanaopona wakawa ni watu wa kutoka mbali tu, wasiofahamika na wenyeji. Mpaka hapo bado hujanipata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…