Mtoto aliyeibwa wodini baada ya kuzaliwa apatikana, akutwa amelala kwa anayetuhumiwa kumuiba

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amelipongeza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Msalala Mkoani Shinyanga na wananchi kwa kazi kubwa waliyoifanya kufanikiwa kupatikana kwa mtoto mchanga aliyeibiwa wodini katika Kituo cha Afya Lunguya Halmashauri ya Msalala.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 18,2022 Kiswaga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama amelishukuru Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Msalala kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kuhakikisha mtoto huyo anapatikana akiwa na afya njema.

"Vilevile tunawashukuru wananchi wote walio shirikiana na Polisi kuwezesha taarifa muhimu za kupatikana kwa mtoto. Nawaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa Polisi ili tuendelee kuiweka Wilaya yetu katika tulivu na yenye amani",amesema Kiswaga.

Amesema tarehe 1/2/2022 majira ya saa 05:30 kwenye Kituo cha Afya Lunguya kilicho ndani ya Halmashauri ya Msalala mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na siku moja tu tangu kuzaliwa aliibwa akiwa kitandani.

"Mnamo tarehe 30/01/2022 majira ya saa 10:00 mama wa mtoto huyo aitwaye Bertha Augustino (20) mkazi wa Ntambarare Kata ya Segese akitokea Zahanati ya Segese na kupelekwa Kituo cha Afya Lunguya kwa Rufaa, alifanyiwa upasuaji na kujifungua mtoto huyo wa kiume na kubakia wodini kwa uangalizi zaidi wa kitabibu.

Mama huyo akiwa pale wodini kabla na baada ya kujifungua alionekana akipewa huduma zingine na mwanamke mmoja mnene, mweusi, mwenye macho ya makengeza ambaye wauguzi walipotaka kujua mwanamke huyo ana uhusiano gani na mzazi, Mama na Baba wa mtoto walieleza kuwa hawamfahamu.

Ndipo ghafla siku hiyo ya tarehe 1/2/2022 majira ya saa 05:30 ilikuja kubainika mtoto huyo ameibwa na mwanamke aliyekuwa akimhudumia mama wa mtoto naye ametoweka.

Jeshi la Polisi lilianza upelelezi wa tukio hilo mara moja ambako waliweza kufika Geita, Sengerema, Kasulu, Masumbwe na Kahama katika ufuatiliaji wao.

Tarehe 16/2/2022 saa 23:30 usiku huko Kijiji cha Kakumbi Kata ya Lubunga Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita askari wa Polisi Msalala walifanikiwa kumkamata mwanamke mmoja aitwaye Rehema Said (47) mkazi wa Lubunga akiwa amelala ndani mwake na mtoto mchanga wa kiume.

Ndugu wanahabari, baada ya kufikishwa Polisi Bugarama Wilaya ya Kipolisi Msalala, wazazi wa mtoto walimtambua mtoto wao na pia mwanamke huyo alitambuliwa kuwa ndiye aliyekuwa akimsaidia mama wa mtoto na kumuiba pale Kituo cha Afya Lunguya.

Amesema Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu upelelezi wa kesi hii utakapokamilika.

Source: Malunde blog
 
Daaah hapa sayansi ya asili ilihusika! Yaanni anakutwa na mtoto? Kama hajitambuwi vile, Mungu ni mwema kwao wamchao
 
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe mkoani Geita, Rehema Saidi (47) kwa tuhuma ya kuiba mtoto mchanga wa siku 20 katika Kituo cha Afya Lunguya kilichoko Halmashauri ya Msalala mkoani hapa.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga (ACP) Joseph Haule, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Februari 17, mwaka huu, akiwa na mtoto huyo baada ya kufanyika kwa upelelezi.

Alisema tukio hilo lilitokea Februari mosi, mwaka huu, majira ya saa 11 jioni kwenye Kituo cha Afya Lunguya.

Kamanda Haule alisema mtoto huyo ambaye ni wa kiume aliibiwa kitandani na kupatikana wilayani Mbogwe mkoani Geita akiwa mikononi mwa mtuhumiwa huyo.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Betha Augustino (21), alivishukuru vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto wake.

“Ninafuraha kumpata mwanangu, naipongeza serikali hususani Jeshi la Polisi na vyombo vya habari kwa kuchapisha habari zilizosababisha mwanangu kupatikana kwani watu wengi wamenipigia simu baada ya kusoma taarifa hizo,”alisema Augustino.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Novelt Furaha aliomba serikali kuimarisha ulinzi katika vituo vya afya, zahanati na Hosptali ya Wilaya ili kudhibiti matukio ya wizi wa watoto hususani katika wodi za kujifungulia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala, Dk. Joseph Muyeye, alikili kutokea tukio la wizi katika kituo cha afya hicho na kwamba mtoto huyo amechunguzwa afya yake na kukutwa yupo vizuri.

Alisema aliyemuiba mtoto huyo alikuwa anamnywesha maziwa ya ng’ombe hivyo wamewashauri wazazi hao waendelee kumnywesha maziwa hayo bila kumbadilishia.

Alisema ili kuendelea kudhibiti vitendo vya aina hiyo wameweka madaftari maalum ya kusaini unapoingia na kutoka katika wodi zote zilizoko katika vituo vya afya.

Nipashe
 
Mtu kama huyu anatakiwa ahojiwe amefanya hilo jambo kwa makusudio gani.

Apimwe akili na kama itaonekana yupo stable then kuna watoto vichang huwa wanaokotwa wanatupwa huko majalalani akapewe.

Kuna watu wamepata shida ya vizazi hawezi kupata mtoto. Wanawake bila mtoto kwake hajakamilika. So ni better kuwasaidia maana unakuta amepatwa na mfadhaiko tu
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amelipongeza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Msalala Mkoani Shinyanga na wananchi kwa kazi kubwa waliyoifanya kufanikiwa kupatikana kwa mtoto mchanga aliyeibiwa wodini katika Kituo cha Afya Lunguya Halmashauri ya Msalala.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 18,2022 Kiswaga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama amelishukuru Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Msalala kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kuhakikisha mtoto huyo anapatikana akiwa na afya njema.

"Vilevile tunawashukuru wananchi wote walio shirikiana na Polisi kuwezesha taarifa muhimu za kupatikana kwa mtoto. Nawaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa Polisi ili tuendelee kuiweka Wilaya yetu katika tulivu na yenye amani",amesema Kiswaga.

Amesema tarehe 1/2/2022 majira ya saa 05:30 kwenye Kituo cha Afya Lunguya kilicho ndani ya Halmashauri ya Msalala mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na siku moja tu tangu kuzaliwa aliibwa akiwa kitandani.

"Mnamo tarehe 30/01/2022 majira ya saa 10:00 mama wa mtoto huyo aitwaye Bertha Augustino (20) mkazi wa Ntambarare Kata ya Segese akitokea Zahanati ya Segese na kupelekwa Kituo cha Afya Lunguya kwa Rufaa, alifanyiwa upasuaji na kujifungua mtoto huyo wa kiume na kubakia wodini kwa uangalizi zaidi wa kitabibu.

Mama huyo akiwa pale wodini kabla na baada ya kujifungua alionekana akipewa huduma zingine na mwanamke mmoja mnene, mweusi, mwenye macho ya makengeza ambaye wauguzi walipotaka kujua mwanamke huyo ana uhusiano gani na mzazi, Mama na Baba wa mtoto walieleza kuwa hawamfahamu.

Ndipo ghafla siku hiyo ya tarehe 1/2/2022 majira ya saa 05:30 ilikuja kubainika mtoto huyo ameibwa na mwanamke aliyekuwa akimhudumia mama wa mtoto naye ametoweka.

Jeshi la Polisi lilianza upelelezi wa tukio hilo mara moja ambako waliweza kufika Geita, Sengerema, Kasulu, Masumbwe na Kahama katika ufuatiliaji wao.

Tarehe 16/2/2022 saa 23:30 usiku huko Kijiji cha Kakumbi Kata ya Lubunga Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita askari wa Polisi Msalala walifanikiwa kumkamata mwanamke mmoja aitwaye Rehema Said (47) mkazi wa Lubunga akiwa amelala ndani mwake na mtoto mchanga wa kiume.

Ndugu wanahabari, baada ya kufikishwa Polisi Bugarama Wilaya ya Kipolisi Msalala, wazazi wa mtoto walimtambua mtoto wao na pia mwanamke huyo alitambuliwa kuwa ndiye aliyekuwa akimsaidia mama wa mtoto na kumuiba pale Kituo cha Afya Lunguya.

Amesema Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu upelelezi wa kesi hii utakapokamilika.

Source: Malunde blog
Uzazi ushakua kilengele hasa kwa 30+ dadas
 
Nawaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa Polisi ili tuendelee kuiweka Wilaya yetu katika tulivu na yenye amani",amesema Kiswaga.
Alitakiwa pia kusema "Lakini polisi nao waache tabia ya kuwaonea wananchi"
 
Mtu kama huyu anatakiwa ahojiwe amefanya hilo jambo kwa makusudio gani.

Apimwe akili na kama itaonekana yupo stable then kuna watoto vichang huwa wanaokotwa wanatupwa huko majalalani akapewe.

Kuna watu wamepata shida ya vizazi hawezi kupata mtoto. Wanawake bila mtoto kwake hajakamilika. So ni better kuwasaidia maana unakuta amepatwa na mfadhaiko tu
Sahih
 
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala, Dk. Joseph Muyeye.....Alisema aliyemuiba mtoto huyo alikuwa anamnywesha maziwa ya ng’ombe hivyo wamewashauri wazazi hao waendelee kumnywesha maziwa hayo bila kumbadilishia.
Mtoto wa siku 20 anawezaje ku digest maziwa ya ng'ombe?

Daktari wa Halmashauri chizi.
 
Back
Top Bottom