Mtoto anarithi akili ya kuzaliwa kwa baba au kwa mama?

akili anarithi kwa baba sisi familia yetu kuna kaka yetu wa kwanza ni baba tofauti na sisi tuliobaki na akili ni tofauti vilevile na tumeshare mama.
 

Kama hali hyo ni kweli.. Nahisi sisi vijana wa enzi za instagram hiz tutapata watoto matahira.. Unamkuta demu yupo instagram anafanya kazi ya kutukana kwenye page za watu.. Tu. Kuanzia asubuhi mpaka jioni..
 
Akili hurithiwa aisee hyo haina ubishi kuna baadhi ya koo watu wake wana akili sana na ni successfully sana in all aspect of life ni nature yao. Ndo mana zamani kabla ya ndoa wazazi waliangalia background ya familia kabla ya ndoa.
Hvi vtu vya kurithi vipo sana tu kabla ya kupata mwezi lazima Ku consider factor nyingi tu
 
Wavulana mostly wanachukua akili zao kutoka kwa Mama kwasababa ile "X" chromosome lazima itoke kwa mama.Na gene ya intelligence ipo embedded humo

Baba anatoa Y na inakuwa XY

Kwa wasichana anaweza kurithi kutoka kwa baba au mama kwasababu wote hawa wawili wana uwezo wa kutoa "X" chromosome na kutengeneza XX
 

Nimefanya a quick google search nimegundua kuwa approximately 50% ya our intelligence is inherited from parents - bado naendelea kutafuta kama mzazi mmoja anaweza kuwa na percentage gani kwa mwanae over the other parent.

Link: http://www.dailymail.co.uk/sciencet...intelligence-inherited-researchers-claim.html


Otherwise, kama alivyosema Paulo Sergio De Souz ni jukumu la wazazi kuhakikisha the rest 50% inapaliliwa na wao...'nurture'...which calls more for your thread..wewe babu na huyu kijana de souz.

See pic for more info...
 

Attachments

  • 1437818098760.jpg
    47.8 KB · Views: 265
Last edited by a moderator:

Nami hii nilisikia miaka mingi iliyopita nikadhani labda kuna utafiti mwingine zaidi ya huu. % kubwa ni kutoka kwa mama.
 

Mimi mtoto wangu sikumpa chochote zidi ya maziwa ya mama yake kwamiez 6 mfululizo sasa ana akili nyingi sana,ameweza kutumia smartphone yangu toka alipofikisha mwaka 1,had watu wanashangaa
 
Mimi mtoto wangu sikumpa chochote zidi ya maziwa ya mama yake kwamiez 6 mfululizo sasa ana akili nyingi sana,ameweza kutumia smartphone yangu toka alipofikisha mwaka 1,had watu wanashangaa

Palilia hiyo kitu na usimshangae wala kuruhusu watu wamshangae coz akianza kujifeel special ujinga utamuingia na atajiona amefika. Akiwa mtoto hivyo hivyo mtreat kama mtu mzima kitoto kitoto lakini na pia kumuongezea challenges zaidi mf; gadgets complicated kidogo, kumzungumzisha maneno kama mtu mzima na si kama mtoto ili awe na challenge ya kuongea kiufasaha, Buni michezo inayostimulate yeye kujua vitu zaidi, kaa nae kwenye laptop ukiwa unafanya kazi zako, tafuta toys za herufi na namba badala ya vigari au midoli. Mjenge apende kujifunza bila kuchoka. Usimcheke anapokosea na badala yake msahihishe kawaida tu n.k
 
Mwl wangu wa bios alinambia uridhi unatoka kwa mama coz during fertilization sperm kinachoingia ni kichwa tu,lkn yai la mwanamke linarutubishwa lote so 75% ni kutoka kwa mama
 

Asante kwaushaur mzuri
 
Mwl wangu wa bios alinambia uridhi unatoka kwa mama coz during fertilization sperm kinachoingia ni kichwa tu,lkn yai la mwanamke linarutubishwa lote so 75% ni kutoka kwa mama

Huyo mwalimu anatakiwa kufutwa kazi mara moja!
 

Mkuu hii ni profession ya watu wanaofanya genetics na sasa tumeenda kwenye genomics.

InshaAllah nikipata nafasi tukumbushane tupige nondo kidogo.

But the bottom line remains that parents pass equal amount of genes to their children.
 

Ulichokisema hapo nami nilishakisema mara nyingi sana humu. Kwamba, wazazi wote wawili huchangia kwa asilimia sawa kwa mtoto.

Na kuhusu urithi wa akili, mtoto anaweza kurithi toka kwa mzazi yeyote yule, awe baba au mama, babu au bibi, shangazi au mjomba.

Hakuna guarantee kwamba kama baba na mama wana akili nyingi basi mtoto naye atakuwa na akili nyingi, ingawa uwezekano wa hivyo utakuwa mkubwa zaidi kuliko uwezekano wa mtoto kutokuwa na akili.

Na nimeshalishuhudia hilo [la mama na baba kuwa na akili lakini watoto wao hamna kitu kabisa].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…