Mtoto ateketea kwa moto ndani ya nyumba iliyoungua

Mtoto ateketea kwa moto ndani ya nyumba iliyoungua

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Simanzi imeikumba familia moja wilayani Moshi Vijijini baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, Francis David, kupoteza maisha kwa kuteketea ndani ya nyumba iliyoshika moto katika Kitongoji cha Mwitini, Kijiji cha Mwasi Kusini, Kata ya Uru Mashariki.

Tukio hilo limetokea Mei 26, 2026 majira ya saa 9:04 alasiri huku juhudi za uokoaji zikifanywa na Jeshi la Zimamoto pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema baada ya moto kuzimwa, mwili wa mtoto huyo ulikutwa umeungua chini ya kitanda ndani ya chumba kilichoteketea.

Mwili huo ulikabidhiwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha tukio hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda, moshi mkubwa ulionekana ukitoka ndani ya nyumba hiyo inayomilikiwa na Lumishael Temba kabla majirani hawajaanza kutoa msaada.

Moto huo uliteketeza chumba kimoja na baadhi ya samani, huku vyumba vingine, stoo, jiko na vyoo viwili vikifanikiwa kuokolewa. Jeshi la Zimamoto limesema uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo ya moto.

20260527_172945.jpg
 
Poleni Sana Sana
Francis Apumzike Kwa Amani
 
Mmmh namhurumia mtoto mateso aliyopitia.
Ukiwaza sana unaweza jiuliza kuangaika kote huku kuna maana gani kama kufa kupo tena vifo vingine vya kikatili
 
Back
Top Bottom