Mtoto chini ya miaka 10 kumkatisha usingizi kisa masomo uchwara; Saa 11 Alfajiri?

Mtoto chini ya miaka 10 kumkatisha usingizi kisa masomo uchwara; Saa 11 Alfajiri?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Shida zako zisikufanye uwe Mpumbavu kiasi hicho mpaka umtese mtoto wako WA kumzaa mwenyewe. Yeye anamakosa gani gani umtese hivyo.
Yaani matatizo yako ya maisha unavyodhani yalisababishwa na wewe kutokusoma ndio unahamishia hasira na Mateso yote Kwa mtoto, huo ni upumbavu!
Aliyekuambia mtoto chini ya miaka kumi kumrokisha Alfajiri yote kabla ya Giza kuisha ahangaike kwenye magari ati ndio kumjengea msingi wa elimu ni Nani?

Acha kutesa watoto, nakuhakikishia hakuna watakalopata Huko mbeleni, ni kuwaumiza tuu. Sasa mtoto wa chini ya miaka kumi unamdamsha kisa elimu, elimu ipi hiyo hasa? Elimu yenyewe isingeruhusu kupokea watoto wadogo kiasi hicho.

Mtoto chini ya miaka sita anatakiwa apelekwe shule saa mbili, kumaanisha saa moja awe ameamka, na sio hiyo Saa kumi na moja.
Mtafutie mtoto shule ya karibu, sio lazima asome shule iliyombali mpaka apande magari.

Wazazi hawajielewi,
Waalimu wanaowapokea watoto nao hawajielewi,
Hao wenye shule wao wanachojali ni pesa tuu.
Kama ingekuwa ni bure unafikiri ingekuwa hivyo?

Mtoto wako mwenyewe,
Pesa yako mwenyewe bado uteseke, na umtese mwanao kisa vitu vya ajabu ajabu!

Taikon nawahakikishia hakuna la maana huko katika Elimu katika umri huo mpaka muwadamshe Alfajiri na mapema kiasi hicho.

Mtoto wa miaka 7-10 angalau huyu aamshwe kuanzia 12:30, ili Saa moja na nusu awe shuleni afanye walau usafi, saa mbili aanze masomo. Asome walau Kwa masaa sita tuu yenye Breki mbili. Saa nane au saa Tisa awe anarudi nyumbani.

Nitashangaa mtu amesoma tena Kwa kiwango cha Degree moja kwenda mbele ati anaruhusu vitoto vyake na kuvidamsha(kuviamsha) Alfajiri na mapema ati viende shule. Hiyo ni Dalili ya kutokuelimika, kuwa punguani,

Mambo ya muhimu katika umri wa miaka 10 Kurudi chini Kwa mtoto;
1. USINGIZI na LISHE
2. UPENDO NA MALEZI YA MZAZI(Sio mwalimu au mtu yeyote)
3. MICHEZO.

Usingizi ndio Jambo la Kwanza la kulizingatia Kwa mtoto aliyechini ya miaka 10 kuliko Jambo lolote baada ya Lishe.
Mtoto wa miaka hiyo atapaswa alale walau masaa 12 Kwa siku. 10 alale usiku, mawili alale mchana.

Huo ni umri wa mtoto Kula lishe kamili ili kuijenga Afya ya Mwili na akili,
Mtoto hata umpe lishe Bora Kama hapati usingizi wa kutosha hawezi kuwa Active hata ufanyeje, atakuwa kama zoba, atakuwa mzito Kama simu za kichina. Lishe kisha usingizi.

Baadaye michezo, michezo inamruhusu mtoto kuiona dunia vile Akili yake utakavyo, michezo humfanya mtoto ajifunze, pia kupitia michezo mzazi utagundua mtoto wako anakipaji na uwezo gani.
Sasa mtoto wa miaka 2-10 kaenda shule tangu saa 11 anarudi jioni amejichokea hivi huyo atakuwa mtoto au kitu gani, hivi utamjua mtoto wako anauwezo gani au anakipaji gani?

Unakuta mzazi bila aibu ati anaambiwa tabia ya Mtoto wake mwenyewe wa kumzaa na mwalimu alafu nalo(mzazi) linashangaa, halijui tabia za mtoto wake, wewe ni mzazi au mpuuzi tuu. Hivi unajua maana ya Baba? Hivi unajua maana ya Mama?
Hakuna Baba wala mama WA hivyo.

Mtoto kabla hajakabidhiwa ulimwenguni lazima mzazi umpe malezi na upendo ndani ya miaka 10, miaka kumi inatosha kabisa kumfanya mtoto vile ulivyokuwa unataka, kuanzia anazaliwa mpaka anafikisha miaka 10 mtoto lazima 90% ya elimu aitolee kwako na sio shuleni.

Shule muhimu kuliko yote ni shule ya wazazi, hizo shule watoto wanazovalishwa Sare hutoa 10% ya elimu ya maisha ya binadamu, lakini wazazi mtoto huchukua 90% ya elimu.
Shule ya wazazi ni halisi, wakati elimu ya shuleni unayo wapeleka watoto wako ni Nadharia tupu zaidi ya Asilimia 90.

Mambo mengi mtoto atakayojifunza kwenye maisha ya nyumbani ni applicable wakati ya huko shuleni waendako ni irrelevant kabisa na mazingira.

Mtoto aliyepata malezi ya wazazi kamili, ataishi na ataweza kuyakabili mazingira hata Kama asipoajiriwa tofauti na mtoto aliyesoma mashule mpaka akawa profesa, akikosa Ajira mazingira yatamshinda tuu.

Acheni kutesa watoto.
Sisi wengine tumeshasoma kidogo tunajua, hatuna la maana na hata nyie mnatuona, labda mkiona tumeajiriwa na tunapata viposho na tumishahara ndio mnadhani watoto wenu wakisoma watakuwa Kama sisi, si ndivyo,

Nani aliwaambia Sisi tulikuwa tunadamshwa Alfajiri kiasi hiki.

Taikon nikiwa Nursery shuleni nilikuwa napelekwa saa moja unusu, hapo ninamiaka mitano, na nilipaswa kusoma Kwa mwaka mmoja tuu niingie Darasa la Kwanza, saa sita hao tunarudi nyumbani.
Saa 12 kamili nilianza kuwahi shule nilipofika sekondari, tena labda nilikuwa nawahi ili nisome Ile Asubuhi kabla ya Usafi kuanza hapo nitasoma mpaka saa moja nikiwa nimefanya Usafi eneo langu. Kabla sijaanza kuleta usumbufu na Kupiga Stori na washikaji.

Alfajiri na mapema hiyo Saa tisa au saa kumi hapo watu tumeshakuwa watu wazima, aidha ni Kidato cha tatu mpaka cha sita ndio tunaamka Kupiga msuli, hiyo itaenda mpaka saa 11 unusu, tunaenda Kupiga Tizi kwa kukimbia mchaka mchaka, saa 12 mnaenda kuoga, wengine wanafanya Usafi kwenye Maeneo Yao, saa moja watu wapo darasani wanafanya homework wengine wanasoma, huku wasio na mood wanapiga Stori tukisubiri Kengele ya paredi.
Saa mbili juu ya alama, vipindi vinaanza, mbona rahisi Sana hivyo.
Hivyo ndivyo wengi wetu tulivyokuwa tunasoma, siye tuliobahatika kupasua anga la shule mpaka vyuo vikuu.

Sasa nashangaa mtoto chini ya miaka 10 anapewaje mamizigo ambayo hata mwanafunzi wa Kidato cha sita asingekuwa na muda nayo?
Ninyi wazazi mnajifanya mnauchungu na elimu, mbona mnachokifanya ni kinyume na elimu yenyewe?

Badilikeni, hiyo Elimu mnatowatesa nayo watoto wenu haitawasaidia Kwa lolote hapo baadaye, mnawatesa, mnawapotezea muda watoto, na chakusikitisha mnapoteza pesa na nguvu zenu bure.

Taikon nimemaliza.

Kwa sasa Taikon ameajiriwa Kama Konda wa Mabasi ya njano.
 
Kwema Wakuu!

Shida zako zisikufanye uwe Mpumbavu kiasi hicho mpaka umtese mtoto wako WA kumzaa mwenyewe. Yeye anamakosa gani gani umtese hivyo.
Yaani matatizo yako ya maisha unavyodhani yalisababishwa na wewe kutokusoma ndio unahamishia hasira na Mateso yote Kwa mtoto, huo ni upumbavu!
Aliyekuambia mtoto chini ya miaka kumi kumrokisha Alfajiri yote kabla ya Giza kuisha ahangaike kwenye magari ati ndio kumjengea msingi wa elimu
Ujumbe wako mzuri jitahidi uwe unaandika kwa ufupi
 
Tatizo walimu mkuu, walimu wanajifanya want uchungu Ili wapige pesa kutokana na program mbalimbali wanazozianzisha
 
Nakutana na mtotot mdogo kamshika mkono mwenzie wanapanda daladala...muhimbili hiyo. Unawauliza wanaishia wapi wanajibu gongo LA mboto..


Sasa najiuliza hiyo mzazi hakuona shule huko gomz au mamia ya shule zote hayafundishi vema hadi amlete muhimbili..hawa watoto asubuhi wanaamka SAA ngapi ili wafike shule kabla ya SAA mbili kuepuka adhabu?

Yani mzazi upo na amani tu mtoto wa miaka 10 anahangaika kuvuka mataa mjini kila siku agombanie daladala mwenyewe?
 
Na nyie wa mabus ya njano, nauliza mmeacha ile tabia yenu mbaya? usiulize ipi maana unaijua.

Miaka ya nyuma kabla ya bus za mwendokasi tulikuwa tunapanda magari saa kumi na moja alfajiri na hao watoto.

Wanalala kwenye bus mpaka konda awaamshe kuuliza unashuka wapi na huwa wanabeba mabegi makuuubwa, sijui miaka hii.
 
Kwa dar vitoto vinapata shida sana vinasinzia noma Kwa kweli hata st kayumba nimelala 11 naona vinapita kuwahi magari
 
Me nikiona begi analobeba mtoto wangu namuhurumia, begi zito utafikiri kabeba mawe. Humo ndani kuna madaftari ya masomo yote na vitabu vya masomo yote, diary na dictionary.
Nimemuuliza huko shule hakuna ratiba ili ubebe vitabu na madaftari kwa kufuatana na ratiba ya siku husika, anasema wanatakiwa kubeba vyote hivyo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Me nikiona begi analobeba mtoto wangu namuhurumia, begi zito utafikiri kabeba mawe. Humo ndani kuna madaftari ya masomo yote na vitabu vya masomo yote, diary na dictionary.
Nimemuuliza huko shule hakuna ratiba ili ubebe vitabu na madaftari kwa kufuatana na ratiba ya siku husika, anasema wanatakiwa kubeba vyote hivyo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Kama mzazi umeliacha au umechukua hatua gani?
 
Unakuta dogo anakaa mbezi au kibamba halafu anasoma bunge au olympio nyie!![emoji15] Duuh
 
Na nyie wa mabus ya njano, nauliza mmeacha ile tabia yenu mbaya? usiulize ipi maana unaijua.

Miaka ya nyuma kabla ya bus za mwendokasi tulikuwa tunapanda magari saa kumi na moja alfajiri na hao watoto.

Wanalala kwenye bus mpaka konda awaamshe kuuliza unashuka wapi na huwa wanabeba mabegi makuuubwa, sijui miaka hii.


😀😀😀😀

Acha hasira Mamaa
 
Back
Top Bottom