Mtoto chini ya miaka 10 kumkatisha usingizi kisa masomo uchwara; Saa 11 Alfajiri?

Yaani kinaniudhi hiki kitendo!!!!
 
Tulisoma montessori kama elimu ya awali .
Shuleni ni saa mbili , Saa nne Tulikunywa uji , baadae ya hapo ni michezo ,kulikuwa na michezo mingi ni wewe tuu uchague unataka mchezo Gani ,ndani ya kisaa kimoja tulimaliza na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Shule ya upili Napo ilikuwa hivyo hivyo La kwanza na la pili Kurudi ni saa nne.

Tatizo wakati huu mzazi kamchoka mwanae ako na 2 yrs anasema huyu kanishinda ni bora akashinde huko shule, Bila kujua au KWA makusudi tunatengeneza Jamii mbovu kabisa kuwahi kutokea .
 
Yupo darasa la ngapi mkuu?

Shuleni hamna lockers?

Awe anabeba safari za somo alilopewa homework pekeee na ufunguo wake?

Kwenye kikao cha wazazi kapendekeze hili.
 
Mwanangu pia standard 1 ila huo mzigo anaobeba natamani kulia mavitabu yote madaftari, maji, diary yaani ni mateso kwa kweli, walimu pangeni ratiba watt wawe wanabeba vitabu na madaftari ya siku husika tu daaaah
 
Muhimu elimu iwe standard kwenye shule zote za awali na kila eneo au mtaa kuwepo na shule ya chekechea na msingi, hii itaondoa ulazima wa mzazi kumpeleka mtoto shule ya mbali tofauti na eneo alilopo kwa kigezo cha ubora wa elimu.
 
Umesema ukweli kabisa,watoto wa wenzetu anaingia anapiga maziwa,uji wanapumzika akimaliza ndani ya darasa masaa ma2 tu breakfast sandwhich,maziwa,maji.
Baada ya hapo michezo nje huko kila mtoto anafanya yake.
Wakimalkza ndank tena lunch tayari wanapiga wanamaliza,saa 1+ wana vyumba ni kulala tu.
Wakiamka nje tena kucheza,wakirudi kidogo darasani alafu wanapewa matunda ,youghot,
wanapumzika
Hapo wazazi wanafika wanachukua watoto huko nje playground kwenda nyumbani.
Kesho program inaendelea.
Mtoto haboreki na shule.
 
Mkuu umekomaa na msosi tuuh .

Ipo vizuri lakini.

Nafikiri ni vyema kutumia mfumo wa montessori kufundishia hapo ni wa kitambo kidogo.
 
Mkuu umekomaa na msosi tuuh .

Ipo vizuri lakini.

Nafikiri ni vyema kutumia mfumo wa montessori kufundishia hapo ni wa kitambo kidogo.
Ndio ilivyo siku zote, sie wengine tumekulia enzi za shule zetu za kata
askreem na mabumunda na vibama.
Darasani sa moja, sa nne break mtajijua wenyewe wamama wauza wako nje pale hukosi kitu hela yako tu.
mnarudi darasa mpk sa saba lunch kila mtu kwao km huna lunch box unakimbia home km sio mbali unapiga menyu.
unageuza sa nane darasa tena mpk sa kumi ukitoka ndio unaenda kuonana na wazazi jioni.
Mda wa michezo chandimu ilikua mabinti rede.
Tumekua wagumu mpk leo.
 
Mkuu umekomaa na msosi tuuh .

Ipo vizuri lakini.

Nafikiri ni vyema kutumia mfumo wa montessori kufundishia hapo ni wa kitambo kidogo.
Ushasema Montesori najua uko wapi.hao ndo ratiba zao hizo
 
Hamna vikao vya wazazi mkatafuta njia bora ya kutatua hilo?
 
Mwanangu pia standard 1 ila huo mzigo anaobeba natamani kulia mavitabu yote madaftari, maji, diary yaani ni mateso kwa kweli, walimu pangeni ratiba watt wawe wanabeba vitabu na madaftari ya siku husika tu daaaah
Nendeni mkazungumze shuleni, mtafute suluhisho. Msiishie kulia lia mitandaoni tu.
 
Mi ningemzuia, shule asomayo dogo, yeye anakuja na daftari la homework tu, mengine wanaacha shule
Na ndivyo inatakiwa, mzazi chukua hatua usiwe mtu wa kulalamika tu. Ndio tunajenga taifa la walalamikaji tu wasioweza kuchukua hatua hata kwa mambo madogo. Kuna vikao vya wazazi, nendeni mkazungumze mtafute suluhu za changamoto hizo.

Usiishie tu kumuonea mtoto huruma maana hiyo huruma haimsaidii.
 
Tumekuwa mazoba, twaona sifa watoto kubeba mizigo mikubwa, kuamka mapema kujazana kwenye school bus
 
Tumekuwa mazoba, twaona sifa watoto kubeba mizigo mikubwa, kuamka mapema kujazana kwenye school bus
Na huo ndio tunaona usasa na maendeleo. Na waweza kuta hata huo muda wa kwenda huko shule hawana, alivyomuandikisha ndio mara ya mwisho. Au labda mpaka aitwe.

Hivi unajua kufuatilia maendeleo ya mtoto kwa ukaribu kunawastua hata walimu kufanya nafasi yao ipasavyo! Mfano itokee wazazi kama kumi wote wameenda shule kulalamikia suala la kuwabebesha watoto mabegi makubwa kila siku unadhani walimu hawatostuka na kutafuta namna?
 
Tatizo wabongo wengi vichwa maji, wanachoamini ukiangaika na ukipitia maisha magumu ndo unafanikiwa

Wanavitesa tu vitoto vyao na ata hamna la maana zaid ya sifa za kijinga
 
Wazazi hawana ushirikiano, hata kwenye PTA kuna wazazi wanakuwa upande wa shule/walimu. Kuna ratiba zinawabana sana wanafunzi ila wazazi wanaona ni sawa wakati kiafya si sawa
 
Wazazi hawana ushirikiano, hata kwenye PTA kuna wazazi wanakuwa upande wa shule/walimu. Kuna ratiba zinawabana sana wanafunzi ila wazazi wanaona ni sawa wakati kiafya si sawa
Wanaona ni sawa kwasababu zinawapa muda wa kutosha kufanya mambo yao maana watoto ni mizigo nyumbani. Tumesahau kabisa nafasi zetu kama wazazi yaani. Ndio maana hata likizo ya mwezi mmoja mzazi bado anatamani shule ifunguliwe haraka kero iondoke nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…